Wasanii ambao hawajui kuimba kabisa lakini bado wanalazimisha kuimba

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,051
Reaction score
12,954
Kumsaidia mtu ni kumwambia ukweli, haijlishi ataupenda au hataupenda ila siku zote ukweli huweka kila kitu huru (Hua napenda sana huu mstari wa Kikiristo wa Yohana 8:32- Utaijua kweli na hiyo kweli itakuweka huru).

Kuna wasanii hawajui kuimba na hawajui kama hawajui kuimba. Mbaya zaidi wanaowazunguka hawawaambii ukweli kua hawajui kuimba.

Hawa wasanii sijui hata wanaimba nini. Mfano Adam Mchomvu, anaimba kwaya, kaswida,vigodoro,mchiriku au kitu gani.

1. Adam Mchomvu.
2. Lavalava.
3. Maromboso.
4. Qeen Darlin.
5. Young killer.(Huyu ashauriwe aachane na mziki, baada ya kubahatisha gambe haitatokea tena kubahatisha).
6. Shilole Kiuno.
7. Snura.
8. Abdul Kiba.
9. Country boy.
10.

Hawa wasanii mlio karibu nao washaurini watafte kazi nyingine ya kufanya. Kazi zipo nyingi, sio kila mtu lazima awe muimbaji. Wengine tubakie tu kama wachezaji na wasikilizaji.

Narudi kuendelea kutoa updates.

Unaweza kuongezea msanii unaeona hajui kuimba lakini bado analazimisha fani.

Nyongeza ya mdau.
 
Mkuu kwa young killer umepotea.... katika watunzi wa mistali fikilishi waliobaki bongo young killer na ngosha wanashika no 2 na 1....

Maana wakina joh wanaimba taarabu siku hizi kina nikki mbishi hawaeleweki
Country weez nae kivuruge tu..

Kama humuelewi young killer basi ni chuki binafsi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…