Wakuu salam,
Tumekuwa tukiona wasanii wakitumika kwenye kampeni na kujiingiza kwenye shughuli za kisiasa ambao karibuni imekuwa too much. Huko nyuma CCM walikuwa na bendi yao ikiongozwa na Hayati Kapt. Komba, kidogo kidogo wasaanii wakaanza kuingizwa kuburudisha, kwa Hayati Magufuli ndio ikawa kama usimikwaji rasmi ya Wasii kuwa chawa.
Wasanii makundi kwa makundi wakanyoosha moja kwa moja CCM na kidogo wakaenda kwa wapinzani.
Tukumbuke wasanii wananguvu kubwa ya ushawishi hasa kwa watu ambao hawajaelimika na kufuata mkumbo ambao ndio wengi. Akimuona tu Diamond anaunga mkono juhudi, au yuko kwa wazee wa babadiliko hata hafakirii mara mbili naye anakuwa chama husika, msanii huyo akipotosha taarifa fulani ni rahisi sana kwa wananchi huyu kukubaliana na alichosema.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mpoto akaanza vizuri na mjomba lakini ukiangalia sasa hivi ni takataka, yaani yeye na Mwijaku ni kama mapacha, tofauti mmoja anafanya upuuzi wake kwa mashairi mwingine anatiririka kwa kuongea kawaida kila anapopata nafasi, wasanii wa maigizo karibu wote ni kichefuchefu, waimbaji kidogo kuna baadhi wanajielewa.
Kwa namna hii, ipi faida ya kuwa na wasanii kama nao kwa namna kubwa wanakuwa sehemu ya upotoshaji?
Najua nyuki wa mama mtakuja, oooh usimpangie mtu, wanafanya wanavyotaka blaaa blaa blaaa, ila wote tunajua wanafanya hivi kwa maslahi binafsi ambayo yakitolewa hutawaona hapo tena, lakini wengine ni rafiki na ndugu zetu na wanasema wazi kabisa naelewa hiki nnachofanya ni upumbavu na napotosha wengi, lakini na mimi nataka niwe na nyumba au gari nzuri kwahiyo potelea pote!
Hawaoni umuhimu wa kuelimisha ili rasilimali hizi zisitumike vibaya kwake bali hata mtoto wake kesho na mjukuu wake keshokutwa afaidike na asije kuishi kwa tabu na umasikini wa kutupwa?
NB: Burudani tunaitaka lakini jukumu la wao kuelemisha jamii kama wasanii na nguvu ya ushawishi waliyonayo ikiishia kwenye uchawa nani ataikomboa jamii?
Au mpaka wageukwe waanze kutaabishwa na utekaji ubishe kwenye milango yao ndio wataamka kutoka kwenye usingizi mzito walionao.
Pia soma:
~
Mwijaku anajikuta nani hasa? Ifike mahala tuanze gomea biashara za chawa wote, unfollow kwenye mambo yao yote!
~
Machawa wanapata wapi pesa? Aristote amjengea ghorofa la kwenda mlinzi wake
~
Samia Challenge: kampeni kwa niaba ya mama?
~
Wasanii wetu tumieni mitandao na umaarufu wenu kukemea utekaji na mauaji yanayoendelea
~
Wasanii wa Tanzania mbona hawakemei utekaji na mauaji yanayoendelea nchini?
~
Nay wa Mitego na Nitasema: Movie ya Chato Part two ni Kizimkazi!
~
Ney wa Mitego aitwa BASATA kujadili wimbo wake wa ‘Nitasema’
~
Kuelekea 2025 - Haya ndiyo makosa ambayo BASATA wanamtuhumu Nay wa Mitego kutokana na wimbo wake wa Nitasema
-
Kuelekea 2025 - Diamond Platnumz: Wana Mbeya mnatakiwa kutembea kifua mbele kwa kumchagua Tulia, tusikubali kulipoteza hili jembe