Niliweka maoni yangu hapa:
Vijana FM: Wamechangia, wewe je?, lakini sio mbaya nikiyaweka tena...
Binafsi, sipingi kile CCM wanachofanya, ila ningependa kusikia kutoka kwa wahusika nini hasa kilichowafanya kukubali kusaidia chama fulani kwenye kampeni. Kuna mtu amemtaja Nakaaya..lkn na yeye hakutuambia anakubaliana na sera zipi hasa za CHADEMA...
Swali ni hili, je, wanakubali "image" yao itumike kama chombo cha kuwahamasisha Vijana kufuatilia na kujishughulisha na Siasa za chama fulani? Bila shaka jibu ni ndio (kwasababu sasa hivi wako kwenye mabango)!
Lakini ukisikiliza nyimbo za baadhi ya wasanii waliotumiwa utasikia vilio kwa Serikali au viongozi "wanaofanya nao kazi" sasa hivi. Je, wamesahau vilio na kauli zao? Hawa viongozi walizisikia zile nyimbo?
Kuhusu hii 'tactic'..dah, lazima uwanyooshee mikono Sisiem..Wanatisha kusema ule ukweli. Sasa, kazi ipo kwa vyama vingine.
Na mwisho kabisa, vipi suala la Pinda kuwa kamanda wa VIJANA...akitawazwa na Kingunge (kamanda wa VIJANA CCM Kitaifa)???