Wasanii wa Bongo Fleva kwanini mnapiga kelele wakati wa kuimba?

Wasanii wa Bongo Fleva kwanini mnapiga kelele wakati wa kuimba?

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Salaam Wakuu,

1. Ni aibu sana.. Msanii unaingia kuimba unapiga kelele. Kwa kelele hizo, pumzi zinakata hata hajamaliza Beti ya kwanza.

2. Wanalazimisha watu kuweka mikono juu, kupiga vigeregere, kuoiga miluzi nk.

3. Tumelipa kiingilio tuimbiwe, lakini msanii akipanda anamwambia DJ azime muziki tuimbe sisi. Nani kalipa ili aimbiwe.

4. Msanii anapanda jukwaani haimbi badala yake anacheza nyimbo zake. Unajiuliza kaja kuimba au kucheza nyimbo zake.. Yaani ni kama kaleta sura yake watu wamuone.

Kwa tamasha la miaka 30 ya bongo Fleva, Shukrani kwa Jumana nature, Solid Ground Family Daz Baba, Mabaga Flesh, Alikiba, Jua kali, Hard Mad, Luteni Karama wa Gangwe mob na Nwasti.

Kuna wengine walikuwa wanaimba utadhani nyimbo sio zao, hata hawazijui. Pamoja na kuwekewa CD, bado wanashindwa kuifuatisha🤣🤣🤣 .

Je hawakufanya mazoezi. Matako yenu..
 
Hao ni matapeli wa burudani kama wale wa "tuma kwenye namba hii"
20250106_051529.jpg
 
Bora bongo flava honors ya Sugu, hii 30 ya BF ni vurugu. Wasanii wengi kufanya show usiku mmoja ni kupoteza muda wao, wa mashabiki wao na kutoitendea haki sanaa yao.
 
wazo lilikuwa zuri utekelezaji ulikuwa mmbaya, pia hao wakongwe wengi wao walishaacha ku focus na muziki hivyo hata mazoezi ya kuimba wengi wao wameyapiga teke. kwa wengine hiyo ilitokea kama nidondokee tu wao na muziki imebaki kusikiliza tu na sio kuimba
 
Kwa wooote nilimpenda Q chief jamani aliimba yule kaka ooh u hali gani tanita....
Nikilala naotaaa, naota kama unaniita ila nafsi inasiita mpenzi.....
Na haya mashairi niliyatumia zamani kidogo kumtongoza Aika kwenye barua yangu kwake ila isivyo bahati barua ile ikadindokea mikononi mwa mzee kipili naye akanitangaza manzese yote ,changanya na kacheo kangu wakati huo ikawa aibu ya mwaka .

Ila palipo na aibu hapakosi mwanga nikaukimbia mtaa ule nikajichimbia mikoroshini nako nikaja fukuzwa kwa fumanizi la aibu .

Old is gold sasa zimebaki story tu
 
Salaam Wakuu,

1. Ni aibu sana.. Msanii unaingia kuimba unapiga kelele. Kwa kelele hizo, pumzi zinakata hata hajamaliza Beti ya kwanza.
View attachment 3627514
2. Wanalazimisha watu kuweka mikono juu, kupiga vigeregere, kuoiga miluzi nk.

3. Tumelipa kiingilio tuimbiwe, lakini msanii akipanda anamwambia DJ azime muziki tuimbe sisi. Nani kalipa ili aimbiwe.

4. Msanii anapanda jukwaani haimbi badala yake anacheza nyimbo zake. Unajiuliza kaja kuimba au kucheza nyimbo zake.. Yaani ni kama kaleta sura yake watu wamuone.

Kwa tamasha la miaka 30 ya bongo Fleva, Shukrani kwa Jumana nature, Solid Ground Family Daz Baba, Mabaga Flesh, Alikiba, Jua kali, Hard Mad, Luteni Karama wa Gangwe mob na Nwasti.

Kuna wengine walikuwa wanaimba utadhani nyimbo sio zao, hata hawazijui. Pamoja na kuwekewa CD, bado wanashindwa kuifuatisha🤣🤣🤣 .

Je hawakufanya mazoezi. Matako yenu..
View attachment 3627528
Kumbe hii ndiyo ID yako Mr. pimbi hater wa Ally na Harmo
 
Bongo unalipia kiingilio cha kumuona msanii live na sio kuimba live .Siwezi kulipia kiingilio halafu niambiwe tuimbe wote, washa tochi,kushoto kulia ,piga kelele,nyanyua mikono juu. Inavyoonekana kwao kuwa msanii ni kurekodi studio tu basi maana masauti yao ni mabaya wakiimba live.
 
Umesahau kushika na kushikishwa kende sijui ndo wanakumbuka mistari

Mike Iko mdomoni mkono mmoja unapelekwa kendeni wanaudhi sana hawa jamaa
 
Back
Top Bottom