Wasanii wanazo pesa wala usidanganywe ila kuna kitu kunaitwa "aliye nacho aongezewe" ..Pia kipindi cha kuumwa hata uwe na billion 1 bank na magonjwa kama hayo ya upumuaji ya kulipia zaidi ya 700k per day na mengi hakuna guarantee ya kupona unaweza kukaa zaidi ya mwaka ...
Kuchangisha ni kuangalia muikito wa mashabiki wake na wadau ,kwa vile msanii ni ishu ya nationalwide na ana mashabiki pande zote ,katika grass root level wewe ukiumwa kama ni mtu wa ofisi watajulishwa wadau wako wa ofisini ,ndugu ,majirani na jamaa maana hawa wanaguswa moja kwa moja ....Ila msanii ni nchi nzima maana mziki unagusa wote.
Huo ndio uafrika kama misiba kila siku ipo mingi ila tunaguswa na ile ya watu tunawafahamu na tuna uhusiano nao wa moja kwa moja...kama kila msiba unakugusa na kulia basi ungekuwa kila siku unalia kwa vile kila siku ajali zinatokea ,watu wanakufa kwa magonjwa .
Unatumia pesa ila kurudi kupona na kurudi kawaida ni ndoto za mchana japo inawezekana ,iyo billion inapukutika huku upo kitandani huingizi chochote kile.
Afya ni mtaji kila siku mnasisitizwa katembeleeni wagonjwa ili kujua umuhimu wa afya yako na uzima.