Lazima utakua unatania. Hakuna mtu wa kusikiliza hiyo nadekezwa ya Mbosso, nisamehe ya Zuchu au hiyo Number one ya Rayvanny miaka 10 ijayo, labda wao wenyewe na familia zao. Ila angalia ngoma kama hizi:
Kasuku - Les Wanyika,
Rangi ya chungwa- Tabora Jazz,
Napenda nipate lau nafasi-Kilwa Jazz Band,
Kifo-Remmy Ongalla,
Georgina - Marijani Rajabu,
Mtaa wa saba, Shida & Jogoo la shamba - Mbaraka Mwinshehe,
Embe dodo -them Mushrooms,
SEYA,
Roger Milla - Pepe Kale n.k
Hiyo ni mifano tu ya ngoma ambazo zimedumu vizazi kibao, bado zinaishi mpaka leo, na tuna uhakika tutaondoka na kuziacha pia.
Ukirudi kwenye bongo fleva kuna mawe wadau wameshuka nayo hapo juu, kama starehe, chemsha bongo, mzee wa busara, mtoto wa geti kali, bongo Dsm, mikasi, hili game, zali la mentali, barua, kamanda na nyingine nyingi.