Wasanii wa Nigeria Wana akili sana kuliko hawa wala ubwabwa wa kampeni huku kwetu

Naija bado wana haki ya peaceful demonstarations ambayo tz huko nyuma ilikuwepo ikayeyuka. Wao naija walianza na peaceful demos celebs waka join.
Kumbe walianza wananchi halafu ndo celebs wakajoin? Sasa ni lini hapa wananchi wameanza maandamano ya kupigania jambo?
Maandamano yaliyowahi fanyika uwa yameratibiwa na wanasiasa wenye malengo ya kisiasa tofauti na haya ya hawa wapopo ndiyo maana hata mwanzilishi hajulikani.
Hebu wananchi waandamane tuone kama wasanii hawajaunga mkono, lakini kama hilo halijafanyika kwanini tuwalaumu? Au mnataka waanze wao halafu wananchi ndiyo waje kuunga mkono?
 
Tigershark kakupa mfano hapo. Wananchi wa Naija walianza kwa kukemea SARS na wasanii wakawaunga mkono.
Je, wananchi wa tz walipokemea Akwilina, nk wasanii waliunga mkono?
Wasanii wa bongo hata habari walikuwa hawana!Walikuwepo kuwepo tu kama mazombie!
 
Ubongo upi ndugu? Wewe mbona unaandika pumba nimekaa kimya. Kujifanya points zako zina mashiko kuliko za wengine, mlioandika inatosha sio lazima wasanii wafanye. Na hayo maandishi yenu yamesolve tatizo? Huna akili vile vile..kakojoe ulale
Aisee,akili za hapa na pale ndio kama hizi!Sio lazima kila movement izae matunda hapo hapo,nyingine ni sauti tu kusikika ili pengine jambo fulani lisijirudie!Ikifika watu wakalazimisha matokeo hapo hapo,ndio hivyo kama ya Nigeria yanatokea!Na hiyo huwa ni uamuzi wa mwisho baada ya kila namna ya kufikisha ujumbe kukwama!
Matatizo kwenye jamii ni yetu sote hivyo inatupasa kushirikiana katika kuyatatua!Ukimuachia mwenzako akemee peke yake,ipo siku nawe yatakukuta na watu watakuachia upambane mwenyewe!Na hapo ndio mnageuka taifa la watu wa hovyo ambapo watawala wanaweza kuwafanya lolote na wakaona sawa tu maana wanaongoza maiti!
Wasanii kwa nafasi zao wanaweza kufanya sauti ifike mbali kwa urahisi!Umeona Genevieve ameandika barua ya wazi kwa Bushiri akimsihi kuchukua hatua,ni tofauti kama barua hiyo ingedikwa na mlalahoi asiyejulikana!
Kama ambavyo wasanii wamekuwa wakitumika mfano Masanja anavyoonesha Miradi ya awamu ya 5 ili hadhira kubwa zaidi ione,basi watumie fursa hiyo hiyo kunapokuwa na ukandamizwaji wa haki!Na huko ndio kunaitwa kujitambua!!!!
 
We unachukulia kama maandamano ni kitendo flani cha kishujaa wakati si hivyo. Ni kitu ambacho hata mtoto anatakiwa awe anawezeshwa kufanya bila hofu na alindwe. Kwa hiyo laumu waliosababisha kutokuwepo mazingira wezeshi badala ya kulaumu wanaosita kuonesha hisia zao kwa maandamano.
 

Attachments

  • 20201023_070524.jpg
    67 KB · Views: 2
Kati yangu mimi na wewe nani analaumu? Kwanini umlaumu msanii? wewe nyma ya keyboard umechukua hatua gani kwanza? Mabadiliko uanza na wewe kabla. Anza wewe kwa kuchukua hatua siyo kujificha nyuma ya keyboard na ID fake halafu ujifanye mpigania haki huku ukilaumu wasanii.
 
Inaonekana mimi nawe kila mmoja ana msimamo wake na hatuwezi kubadilishana. Kwa hiyo we baki na lako nami nibaki na langu tusiishie kutoleana vi povu bure!!
 
Inaonekana mimi nawe kila mmoja ana msimamo wake na hatuwezi kubadilishana. Kwa hiyo we baki na lako nami nibaki na langu tusiishie kutoleana vi povu bure!!
Kweli kabisa maana kamwe siwezi kubaliana na watu wenye mtazamo ya kwamba haki zao zitapatikana kwa kungoja wengine wawapiganie.
 
 
Wao wanatweet kuambia watu waandamane wakati wenzao wanauliwa mtaani..
Acha uongo, paroranking, Davido, Burna boy wameingia barabarani, unafikiri akili zao kama akina kiba au diamond
 
Acha uongo, paroranking, Davido, Burna boy wameingia barabarani, unafikiri akili zao kama akina kiba au diamond
Asee mi nilimuona Davido tu tena alikuwa na bodyguards wake in disguise. Wengine wapo Ulaya kazi kutweet tu.
 
Umepaniki wewe ni Alikiba au Ray kigosi?!
 
Zile hashtag na kushinikiza serikali zimeshasahaulika mara hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…