Wasanii wa sinema punguzeni "Uzungu"

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Wakuu, siku hizi ninapata nafasi ya kutizama TV baada ya kustaafu.

Nimekuwa naangalia chaneli ya Sinema zetu ya king'amuzi cha Azam na kukerwa na huu mtindo wa baadhi ya waigizaji wakijifanya kuongea Kiinglishi sasa kwa wasio kielewa inakuwa haina maana.

Wenzetu huwa wanaweka maandishi kama tafsiri.

Pana hizi kama Mwanamuziki na Bamba to bamba zinakera.
 
Mh hamna kitu kabisaaaaaa
 
Ndiyo maana wanaitwa wasanii, wasanii wa kibongo ni mazwazwa kweli. Mtu hata kama hajuwi kiingereza anaona ufahari kukariri na kutumia hayo maneno ya kiingereza kwenye tamthilia na sinema zao za kichizi. Poleni mnaowafuatilia.
 
Wewe unakitafuta Kifo haraka! Jifunze kuignore ukiwa mstaafu
 
Boss mimi ngoja nikupe siri ya script, katika dialogue kuna reality ambayo inaruhusu kuchapia, kuna utumiaji wa code mixing and switching(hizi kwa kiswahili tutasaidiana) hivyo kwa maana hiyo , huwa hawakosei wanamaanisha wanachokifanya...😊😊😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…