Wasanii wa Tanzania wengi wameishia Kidato cha pili, hawana elimu ndio maana wako hivyo walivyo

Wasanii wa Tanzania wengi wameishia Kidato cha pili, hawana elimu ndio maana wako hivyo walivyo

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Wakuu

Kiukweli hawa wasanii wetu wa Tanzania baadhi sio wote story zao kwenye kujieleza utajua tu wana matatizo vichwani mwao.

Wasanii wengi utasikia niliishia kidato cha pili hata hawaeleweki na ndio maana wanaishi kwa kuigiza hadi wanakufa

Sisemi vibaya lakini mtu ambae hana shule kwa nchi zetu wanakua sio welewa na wana matatizo mengi sana kwenye akili zao.
 
Afadhali hao walio ishia form two wanatengeneza pesa na hawalalamikii serikali kuhusu ajira, wengi wameajiri walio maliza hiyo form four....kikubwa zaidi wanatengeneza pesa ndefu ambazo wewe ulisoma ukiamini ndio chanzo cha kuzipata. Acha dharau.
 
Wameajiri wenye degree kabisa mkuu, dunia hii ya leo bado kuna watu wanaringia vyeti?
 
Je wanapesa kiasi gani hao walioishia form two
 
Namshangaa huyu mtoa mada, wenye vyeti wameacha nyumbani now wanakaanga chips, wanauza ice cream yeye analeta dharau? Wengi waliofika chuo kikuu wanajuta maana wanaona wamepoteza muda wa kuanza kuzisaka pesa.
Yaani acha tu, bora hata hao walioshtuka mapema wakaweka vyeti kabatini, wengine wanakuwa wabishi hadi wanashtukia wanafika umri wa kustaafu bado wana bahasha mkononi.
 
Wewe ulie soma una nini na umeajiri wangapi? Na jamii yako inanufaika vipi na elimu yako?
 
Mleta mada hajasema hawana hela. Amesema hawana uwezo mzuri wa kujieleza.
Sijui kwanini mnampiga mawe!
Wengi wana uwezo mzuri tu wa kujieleza maana wengi wamekutana na watu wa mataifa mbali mbali wamepata exposure nzuri tu kuliko alie na elimu ya chuo kikuu amebaki na bahasha mkononi anakutana na watu wa kitaani kwake mawazo yapo ndani ya box.
 
Back
Top Bottom