Wasanii walioitwa na Katambi leo wamesamehewa bado Anko T na Niffer ambao hawakufika

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobas Katambi amesema wasanii na watu maarufu waliotikia wito wa kwenda kwenye kikao nae wamesamehewa makosa mbalimbali waliyokuwa nayo huku Jeniffer Jovin na Twalibu Bakari Anko T kutosamehewa kutokana na kutofika katika kikao hicho.

Katambi amesema hayo Septemba 2, 2026 akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho ambapo amesema wasanii hao walikuwa na mashtaka mbalimbali lakini Wizara hiyo imekaa na waliowashtaki na kuzungumza nao juu ya kuwasamehe lakini pia wasanii na watu hao maarufu leo wamepewa elimu kwani wako waliokiri kuwa makosa waliyokuwa wanayoyafanya hasa mitandaoni hawakuwa wakifahamu ni kosa kisheria.

Soma Pia: https://www.jamiiforums.com/threads/katambi-awaita-dudubaya-pipytida-kwenye-kikao-maalum.2468461/

Ameeleza kuwa Anko T na Noel(Mwanamitindo wa msanii Diamond Platnumz) wamesema wapo nje ya nchi huku wakitakiwa kurudi nchini.​
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobas Katambi amesema wasanii na watu maarufu waliotikia wito wa kwenda kwenye kikao nae wamesamehewa makosa mbalimbali waliyokuwa nayo huku Jeniffer Jovin na Twalibu Bakari Anko T kutosamehewa kutokana na kutofika katika kikao hicho.

Katambi amesema hayo Septemba 2, 2026 akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho ambapo amesema wasanii hao walikuwa na mashtaka mbalimbali lakini Wizara hiyo imekaa na waliowashtaki na kuzungumza nao juu ya kuwasamehe lakini pia wasanii na watu hao maarufu leo wamepewa elimu kwani wako waliokiri kuwa makosa waliyokuwa wanayoyafanya hasa mitandaoni hawakuwa wakifahamu ni kosa kisheria.

Ameeleza kuwa Anko T na Noel(Mwanamitindo wa msanii Diamond Platnumz) wamesema wapo nje ya nchi huku wakitakiwa kurudi nchini.​
Niffer ni msanii wa kitu gani?
Na amekosa nini?
 
Back
Top Bottom