Ngojera za maisha hazina uhalisia , wengine wanapambana mchana mpaka usiku ila hawana mafanikio , wengine wana mirija ya pesa na wanazipata kwa urahisi ..Kiufupi hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya mafanikio na kupambana.
Kupambania maisha ni kitu ya asili na hakuna binadamu ambaye hapambani ,wale Hadzabe wanapamba kupata chakula kila siku , wanapumzika mara chache ila yale ndiyo maisha ..Mapambano ni jambo la asili bila ya kupambana, sasa wanayosema hao jamaa ni yapi ?
Jamii za kale ndizo zilipambana ili kuishi , ikiwa ni pamoja na kujitafuta vyakula , makazi na ulinzi ..Zamani ilikuwa lazima ufanye shughuli ili ukitaka bidhaa nyingije uipate sio kwa sasa kwa sababu tunatumia centralized economy chini ya Pesa ..SO ili uwe na mafanikio karne hii ni lazima uwe na pesa , haijalishi utaipata vip ....Unaweza kuiba , kudhulumu , kufanya kazi , kutapeli , kuwanyonya wengine ..Zama za kulima au kufuga na kutumia nguvu hazipo , hata ukiangalia hapa bongo biashara zenye mtonyo mrefu ni zile black market . Hizo black market watu wanapiga mshindo , unakuta mtu ana dili phase 4 kwa mwaka ; anaweza kutengeneza mpaka mil 200 na kuendelea meanwhile Mgosi pale kariakoo anamka kila siku alfajiri kubeba mzigo mpaka jioni ana kama 20k maximum . Sasa haouni hakuna uwiano hapo wa mapambano .
Ukikuta matajiri kumi (01) katika uchumi wa pesa huu basi tambua saba(07) wameumiza wengine mpaka kufikia pale , vipo viwanda vinanyonya wengine wao wanatengeneza pesa ndefu ila wanaopambana katika uzalishaji wanapewa kifuta jasho .
Ni mjinga pekee anaweza kuongelea mapambano katika uchumi wa pesa ,hakuna tajiri anatumia nguvu kama walioko chini yake ..Uchumi wa pesa kikubwa uwe na pesa no matter umeipata wapi ila zamani lazima uzalishe ili upate kitu kingine ..