Wasanii wetu wengi bado hawajui kufanya Biashara na makampuni

Wasanii wetu wengi bado hawajui kufanya Biashara na makampuni

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Kuna vitu wanavyo wasomi, halafu wao wanakwenda kuwapa wasanii ama watu maarufu ambao si wasomi, mwisho wa siku wanakuja kupiga pesa.

Tatizo la wasanii wa Kibongo? Wanaajiri wasomi lakini hawa wasomi wanakuwa na tamaa ya pesa, wanachokitaka ni msanii kuingiza pesa, wagawane na kisha wachukue chao na kusepa, kumbe kulikuwa na jambo zuri la kumsaidia msanii na mwisho wa siku akapiga pesa ndefu.

Ndiyo!

Huu ni ujanja ambao wasanii wa Kibongo ama Afrika kwa ujumla hawawezi kuufanya kwa sababu wanafikiria pesa kwanza kabla ya kitu chochote. Unamuona P Diddy, wakati alipofuatwa na kinywaji cha Ciroc ili afanye matangazo, akasema yeye hataki kulipwa bali anataka hisa. Akapewa hisa, naye akawa na umiliki kwenye kampuni.

Baadaye naye 50 Cent alifuatwa na kampuni ya kinywaji cha VitaminWater na kumwambia walitaka afanye matangazo na angelipwa. Yeye alichowaambia ni kupewa hisa, wakakubaliana pesa, halafu akasema hizo pesa ziwekwe kwenye hisa, baadaye kampuni ilipouzwa kwa Coca Cola, 50 akapata dola milioni 100. Pesa ambayo ni kubwa mara hata zaidi ya kumi ya kile ambacho angelipwa.

Mwaka 2005 jamaa mmoja mchoraji alipewa kazi ya kwenda kuchora katika jengo la kampuni ya Facebook, alipomaliza kazi yake akatakiwa kulipwa dola 60,000 lakini yeye akasema hizo ziingizwe kwenye hisa, leo hii amefikisha dola milioni 200.

Ni akili iliyoje?

Mfano leo Pepsi wakimfuata Mondi ama Kiba, wakakubaliana malipo, mathalani milioni 50, halafu wakasema hizo milioni 50 ziwekeni kwenye hisa, miaka mitano baadaye hazitokuwa milioni 50, zitakuwa zaidi ya 150. Hizi ni akili ambazo unashauriwa na watu waliokwenda shule, hili hakushauri meneja kwa kuwa naye kwenye hizo pesa atataka.

Wasanii wajitahidi kuweka hisa kwenye haya makampuni badala ya kuchukua pesa na kwenda kuzitumia. Hisa mara nyingi huwa zinapanda kila siku na hazishuki.

Umepokea mamilioni, nenda kaweka hisa zako pale CRDB ama NMB ana NBC, ama mitandao ya simu, kadiri miaka inavyoenda mbele, nawe hisa zako zinaongezeka.

Juzi niliangalia Interview ya yule Mdada aliyeweka Sauti ya "Namba unayopiga haipatikani kwa sasa, jaribu tena baadae" kwenye mtandao wa Tigo.

Yule Mdada hakujua thamani ya sauti yake, ukimsikiliza vizuri utagundua alilipwa mara moja tu, lakini sauti yake inaendelea kutumika miaka mingi bila yeye kufaidika na chochote.

Wasanii wa wenzetu wapo smart sana vichwani japokuwa wamekaa mitaani, mitaa imewalea, ila linapokuja suala la pesa, wanachukua vichwa hatari sana.

Kasome kitabu cha 50 Cent utayaona haya ninayokwambia.
 
Back
Top Bottom