HOJA Washereheshaji (MCs) hii tabia ya kuchukua video au picha bila idhini na kuzipost kwenye kurasa zenu mnaona ni sawa?

HOJA Washereheshaji (MCs) hii tabia ya kuchukua video au picha bila idhini na kuzipost kwenye kurasa zenu mnaona ni sawa?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Mmekua na tabia ya kuchukua video/picha za waalikwa bila idhini yao na kuzipost kwenye kurasa zenu za mitandao ya kijamii,kwani nyie wenzetu mnaona ni Sawa?

Mimi nimekuja zangu kwenye sherehe mubebezi yupo huko mbali nimemuaga nalala wewe asubuhi asubuhi umeshaanza kunipost

Nacheza ukumbini nimechangamka nimeshameza vyupa vyangu wewe unanichukua video unautangazia ulimwengu🙌🙌🙌🙌🙌

Acheni hizi mambo bhana zinaboa kishenzi!!
Nachukia sana huo upuuzi kwa kweli. Kuna clips kibao zipo instagram na tiktok zina matukio ambayo wahusika hawajaridhia yarushwe. Hii ni uingilia privacy za wahusika!
 
Upo public unapostiwa public

Sasa mc anatangaza vip bznez yake?
 
Bila kufanya hvy mtawajuaje kama wapo, mpostiwe tuu Hakuna namna
 
Nilimpeleka mtoto wangu kupiga picha za bday ya mwaka 1, nikakuta ile studio wamepost picha za mtoto wangu kwenye mitandao ya kijamii.
Yule kaka hatokaa kunisahau..!
Wengi wanafanya hivi. Uelewa mdogo na kuuchukulia vitu simple nafikiri.
 
Kuna defense inaitwa volenti non fit injuria...kitendo cha kwenda kwenye public events means umekubaliana na any harm might arises
Sahihi.

Mfano ww leo ukijiona umeonekana kwenye tv bila ww kujua n rahisi kwenda kuwashtaki hata kama walikualika Ila hakuna makubaliano ya ww kuonekana.

Ila ukienda uwanjani kwenye mechi na ukionekana kwenye tv, huna uwezo wa kuwashtaki.
 
Wanywa vyoda ndio wana tabia za kimbeya mbeya , hata bar utayakuta yanakodoa macho kama bundi kusaka umbeya tu
🤣🤣🤣kuna mlevi uchwara mmoja alinikuta Lounge na Fanta Passion yangu alishika tu akatikisa kichwa kusikitika akapita bila salamu.
 
SASA si umeenda kwenye matukio ya kijamii, wenzako wanapublicise wapate trends ya BIASHARA za, kwani hukujua BIASHARA matangazo, kama HUTAKI kuonekana ungejifungia ndani,

wanaokushauri ushtaki, ingekuwa kakuoiga picha guest then kakupost Hapo ndo ungesema, lkn kwenye sherehe ni watu changanyiken na unajua kwenye sherehe lazima camera ziwepo na zina bajeti yake, so sioni kosa Hapo, kosa ni ww kumdanganya mwenzi wako kuwa upo hospital kumbe upo kwa sherehe
Over
Picha na ulichoandika ni udhalilishaji
 
Back
Top Bottom