Washindi wa Mchongo Pesa ni halali au uhuni unafanyika?

Washindi wa Mchongo Pesa ni halali au uhuni unafanyika?

Kamali ni kama michezo ya pyramid. Wanakusanya fedha nyingi kwa watu na kumlipa mmoja wa hao waliochangia kiasi fulani cha pesa ambacho kiukweli ni kiduchu. Ile baki inarudi kwao na faida yake ni kubwa sana. Akili mukichwa, kazi yao ni kukusanya tu pesa na kukuhakikishia kuwa waweza kushinda ukicheza zaidi na zaidi. Na kwa bahati mbaya michezo hii hujenga uraibu, ukishaanza kuacha ni kazi, hasa ukiwaona wenzio ambao wamefanikiwa kupata zawadi hizo.
Ni sahihi, huwa wanatumia chambo ya washindi kadhaa ili kuvutia wengine wacheze.

Utasikia fulani ni fundi umeme au machinga kashinda Jack Port ya Milioni 200. Ukiangalia huyo jamaa na status ya kazi yake roho itakuuma kuwa jamaa katusua kirahisi na wewe utachukua uamuzi wa kujiingiza mchezoni.

Maskini bahati mbaya kumbe hujui hao washindi huwa wanapangwa ili kuvutia watu wacheze.

NB: Ukishirikishwa kwenye fursa ujue wewe ni fursa
 
Maisha yamekuwa magumu sana zama hizi.

Kila kitu ni fursa.
 
Mjini watu wanaishi kwa kutumia akili sana.

Cha ajabu sasa wanaoumizwa ni masikini kwani hawana uelewa huo na wanatamani kutoboa haraka, wakiona fursa kama hiyo wanairukia kumbe wanadondokea shimoni.
Jiulize kuhusu ile Jackpot ya Sportspesa. Ina mwaka sasa haijapata Mshindi!
Yaani Watanzania wanabet kwa zaidi ya Jumamosi 52 lakini wanasindwa kupata michezo 13 sawasawa!
Siku akipatikana Mshindi utaambiwa ni Washindi Wawili kwa hiyo inabidi wagawana! Kwa nini kila asipewe zake kama.ilivyo kwa Washindi.wa Mechi 12, 11 na 10?
Ni Uhuni tu kwa kwenda Mbele!
 
Oya kama unahela wewe bet kila mtu Mungu anajua riziki yake ndomana kuna anae bet anashinda mpaka 100m hio ni bahat au riziki yake ilishapangwa na kufanikiwa inataka akili na ujanja. Si bora mtu anaebet kuliko anaekula rushwa uyo akishinda ni jasho lake na anaekula rushwa??. Acha propaganda
Mmmhhh!!!
 
Katika maisha Always Be you and don't compare!!
Huyo anayekula 100m do you know the secret behind mpaka kula kiasi chote hko na Kama Ni ujanja kwann wewe hujawah kula pesa Kama hyo?

Betting ni kamali na hata dini imekataza ndo Mana hata Ali kiba alikataa Kaz ya ku promote betting ila Mwijaku kutokana na Tamaa ya pesa akaamua kuchukua dili fatilia interview zake.

Amnaga riziki ya kucheza kamali Ni sawa na kama kibaka tu anakaba apate ela ambayo siyo halal.

Kama una Kaz komaa nayo ikupe mafanikio Kama huna Muombe Mungu tafuta connection and work hard utatoboa tu hata ss tultoka huko.
Hata dini zenyewe ni kamali tosha.....
 
Mtoa mada nakusihi uendelee kucheza bahati nasibu zetu kwani wikiendi hii kuna mazawadi kibao kwa ajili yako.

mfano, kuna vikombe, t-shirt, bodaboda, bajaji, vifaa vya ujenzi na kubwa kuliko ni mamilioni ya kushindaniwa zaidi ya bilioni 100.
Unasubiri nini mtoa mada, Cheza sasa na uibuke mshindiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Vigezo na masharti kuzingatiwa.
Hata sisi tuna familia, lazima maisha yetu yaendelee kwa kukutegemea.
 
Back
Top Bottom