Washindi wa Mchongo Pesa ni halali au uhuni unafanyika?

Ni sahihi, huwa wanatumia chambo ya washindi kadhaa ili kuvutia wengine wacheze.

Utasikia fulani ni fundi umeme au machinga kashinda Jack Port ya Milioni 200. Ukiangalia huyo jamaa na status ya kazi yake roho itakuuma kuwa jamaa katusua kirahisi na wewe utachukua uamuzi wa kujiingiza mchezoni.

Maskini bahati mbaya kumbe hujui hao washindi huwa wanapangwa ili kuvutia watu wacheze.

NB: Ukishirikishwa kwenye fursa ujue wewe ni fursa
 
Maisha yamekuwa magumu sana zama hizi.

Kila kitu ni fursa.
 
Mjini watu wanaishi kwa kutumia akili sana.

Cha ajabu sasa wanaoumizwa ni masikini kwani hawana uelewa huo na wanatamani kutoboa haraka, wakiona fursa kama hiyo wanairukia kumbe wanadondokea shimoni.
Jiulize kuhusu ile Jackpot ya Sportspesa. Ina mwaka sasa haijapata Mshindi!
Yaani Watanzania wanabet kwa zaidi ya Jumamosi 52 lakini wanasindwa kupata michezo 13 sawasawa!
Siku akipatikana Mshindi utaambiwa ni Washindi Wawili kwa hiyo inabidi wagawana! Kwa nini kila asipewe zake kama.ilivyo kwa Washindi.wa Mechi 12, 11 na 10?
Ni Uhuni tu kwa kwenda Mbele!
 
Mmmhhh!!!
 
Hata dini zenyewe ni kamali tosha.....
 
Mtoa mada nakusihi uendelee kucheza bahati nasibu zetu kwani wikiendi hii kuna mazawadi kibao kwa ajili yako.

mfano, kuna vikombe, t-shirt, bodaboda, bajaji, vifaa vya ujenzi na kubwa kuliko ni mamilioni ya kushindaniwa zaidi ya bilioni 100.
Unasubiri nini mtoa mada, Cheza sasa na uibuke mshindiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Vigezo na masharti kuzingatiwa.
Hata sisi tuna familia, lazima maisha yetu yaendelee kwa kukutegemea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…