MTZ 255Dar
JF-Expert Member
- Sep 25, 2018
- 1,149
- 3,963
Msemaji wa White house amesema kwamba miezi michache ijayo Marekani itatuma vifaru aina ya M1 Abrams nchini Ukraine. Wanajeshi wa Ukraine wataanza kupatiwa Mafunzo ya vifaru hivyo nchini Poland kwa muda wa miezi 3.
Hayo yanajiri siku moja baada ya Ujerumani kukubali kutuma vifaru 29 aina ya Leopard 2 nchini Ukraine. Nchi za Poland, Finland na Canada zikiwa tayari zimetuma Maombi rasmi kwa Ujerumani ya kuziruhusu kutuma vifaru vya Leopard nchini Ukraine.
Maoni yangu
Kwanini vifaru vichukue muda mrefu hivyo Kufika Ukraine? Ujerumani imesema Vifaru vyake chapa ya Leopard vitawasili mwezi wa nne nchini Ukraine baada ya Tangazo Hilo huku Vifaru vya Marekani aina ya M1 Abrams vikitarajiwa kuwasili nchini Ukraine mwezi wa 6.
Pia, Marekani ina vifaru vya M1 Abrams zaidi ya 3,000 ambavyo viko Store vinakula vumbi tu havina Kazi. Kwanini watume vifaru 31 tu? Au wanaidharau jeshi la Urusi mpaka lishindwe na vifaru vichache tu vya Magharibi?
Time will tell.