Washington Post: Hakuna namna Rais Magufuli anaweza kujitenga na uwajibikaji kutokana na matendo ya Makonda

Washington Post: Hakuna namna Rais Magufuli anaweza kujitenga na uwajibikaji kutokana na matendo ya Makonda

Magufuli and Makonda are Tweedledee and Tweedledum.

Hakuna maelezo yoyote yale yenye kuingia akilini kwa nini mpaka sasa Makonda hajatumbuliwa ilhali kuna wengine wengi tu ambao wametumbuliwa kiajabuajabu.
Hata mtu ajaze debe la maelezo hayatatosha mkuu. Nadhani kama nchi kuna kitu tunamuogopa Makonda kutuumbua. Nadhani tumevunja chupa ya chai na tunaogopa kusemwa kwa mama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajamvi, hiki kipengele hapo chini, kimo kwenye hii makala ya Washington post inayosema “Democracy Dies in Darkness” ya mwaka 2018

“Makonda and Magufuli are too closely linked for the president to escape responsibility.“-The Washington Post.

Katika makala hiyo ambayo link nimeiweka, mwandishi huyo Rachael Mclellan, amechambuwa vilivyo. Pia wanasema issues ya ushoga CCM wanaitumia kama njama za kisiasa.

Matendo yote mabaya mfano kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda, kushambuliwa kwa Lissu nk vyote vimeorodheshwa humo. Hata CCM kununua wapinzani, ubambikiaji wa kesi kwa upinzani na wafanyabiashara vimetajwa.

Nimeona makala hii ni intersting zaidi baada ya ban aliyopigwa Makonda kuingia US

Kwa vyovyote vile, kumtarget Makonda ni kama vile ujumbe kwa Maghufuli(kwa wale waliokuwa wakijiuliza). Kwa maoni yangu, uchaguzi ujao utakuwa wenye changamoto kubwa sana kwa Taifa letu. Na wafadhili sasa wameshaanza kuona kuwa ccm siyo chama kizuri. Someni wenyewe...

Source: https://www.washingtonpost.com/news...g-schoolgirls-and-killing-opposition-leaders/
Bashite anatumwa na "MTU FURANI" naomba MUMUOMBEEEE!
 
Huyu mpumbavu anatuletea habari ya mwaka 2018??! jinga kabisa, angalia hiyo link ya mwaka gani
Tena ina mwaka na upukupuku, tena wanajiona wasafi, huku Democrats wanadai Russia wamehusika katika uchaguzi wao, bado kuna swala la vitisho kwa Ukraine na viongozi wa FBI na wengineo, kweli nyani haoni kundule...
 
Magufuli focus kwenye plan za kujenga uchumi imara mwache shavu dodo akomae na kutoa taarifa nje akifikiri zitamsaidia, mtakuja mshangae November , nyie mnajua ccm ilivyo na nature ya wananchi wetu,mtapigwa chini hadi muone aibu November labda kama kuna plan ya kuiondoa kwa mabavu,chukueni vibali mfanye siasa majimboni.
 
Hivi juzi iliukuwaje jeshi letu likapokea misaada kutoka kwa maadui wetu?interesting!!!ningekuwa Mimi ningewavurunisha wamarecani waondoke wote nchini!!mipumbafu kabisa.wanajifanya wanagawa dawa za ARVs,Vilainishi,dawa za uzazi wa mpango nk kumbe wanapeleleza nchi yetu.Ngoja tumwite Mungu wetu watakiona cha mtemakuni
 
Mwandishi pia anadai kuwa Maghufuli ameweza kufanya matendo mengi maovu kwa kuwatumia wasaidizi wake bila ya wao kuhusishwa na uhalifu huo...Mfano kumtumia Makonda kufanya mambo machafu nje ya yale ya kiofisi! Na kwamba huwa anajiweka mbali matendo hayo ya spot okra, lakini kumbe yeye ndo yuko nyuma yao! Nimemnukuu hapo chini...

The Washington Post

Pascal Mayalla
Dah!
 
The Washington Post, ndilo gazeti kiongozi la mabeberu duniani!, liliwahi kumngoa hadi rais wa Marekani kwa kwa kuibua ile kashfa ya Watergate iliyomuondoa rais Richard Nixon wa Marekani.

Kuna vingi vimesemwa humu ni vya kweli lakini pia kuna baadhi wameongeza chumvi kama ile ya ku arrest pregnancy girl, hawawi arrested bali wanafukuzwa shule!, wanaokuwa arrested ni the culprits, mafataki wanaowajaza watoto wetu mimba!. Ile issue ya Tandahimba ni wale wasichana waliopata ujauzito sio kuwa arrested bali walitakiwa kuhojiwa ili wawataje waliowapa ujauzito sheria ichukuwe mkondo wake, lakini kwa kuhofia mafataki kupigwa mvua 30, hivyo waliotiwa mimba kuteseka kwa kuzaa watoto bila malezi ya wenye mimba zao, wazazi wa mabinti walioamua ku collaborate na mafataki, ama wawaoe mabinti zao au watoe matunzo, wakienda jela ni mateso kwa binti yao na majanga kwa familia zao.

Tungekuwa na serious media, tungepata a development kuna yoyote alikuwa arrested?.
P
 
Hivi juzi iliukuwaje jeshi letu likapokea misaada kutoka kwa maadui wetu?interesting!!!ningekuwa Mimi ningewavurunisha wamarecani waondoke wote nchini!!mipumbafu kabisa
Wenzio wanasafisha stoo wee unaita misaada. Wanaingiza Mali mpya updated. Za zamani wanatoa waweke wapi ndiyo hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Article nzuri sana, si kwa sababu inatuambia kipya ambacho wa Tanzania tunaofuatilia mambo hatujui, bali kwa sababu imekusanya mambo mengi pamoja, kwa hadhira ya kimataifa.

Nimependa sana alipoandika kuhusu "plausible deniability". Nimetoka kuongelea "plausible deniability" hapa JF nafikiri siku mbili tu zimepita.

Kwa sasa inabidi Magufuli awe mdogo tu na akubali amechemsha kumuachia Makonda, vonginevyo, watu watajua yeye ndiye anayemtuma.
Kwani Nani ambaye hajui?
 
Pia inadaiwa na mwandishi kuwa Maghufuli anawatumia wakuu wa wilaya na mikoa kupambana na kuwafanyia fujo wapinzani. Haswa sehemu zenye kuwa na viongozi wa upinzani nk. Wanasema wanalipizia kisasi kwa kuwaadhibu watu wa maeneo hayo kwa kuchagua upinzani!

“I find that regional and district commissioners take a more active and violent role in areas where the opposition runs local governments. They make it difficult for opposition governments to effectively deliver public services, thereby simultaneously punishing those who voted for the opposition and discrediting opposition parties.”-The Washington Post.
True story

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa. penyewe
What’s going on? Since 1961, Tanzania has been ruled by the same party, Chama Cha Mapinduzi (CCM). While it has never been a democracy, Tanzania had been better known as a safari tourism destination and as a donor darling. How have things become so repressive so quickly?

The answer lies in the 2015 election of John Magufuli as president. Since then, opposition politicians have been arrested, harassed and beaten. TV offices have been raided and newspapers suspended. Regime critics — journalists, business executives, oppositionpoliticians, student leaders — have been kidnapped, forced into exile or assassinated by “unknown assailants.” Some have never beenseen again. Much more violence outside Dar es Salaam hasn’t been reported, even in the Tanzanian press.
 
Hawa jamaa wanajua madhambi yote ya ccm
Pia inadaiwa na mwandishi kuwa Maghufuli anawatumia wakuu wa wilaya na mikoa kupambana na kuwafanyia fujo wapinzani. Haswa sehemu zenye kuwa na viongozi wa upinzani nk. Wanasema wanalipizia kisasi kwa kuwaadhibu watu wa maeneo hayo kwa kuchagua upinzani!

“I find that regional and district commissioners take a more active and violent role in areas where the opposition runs local governments. They make it difficult for opposition governments to effectively deliver public services, thereby simultaneously punishing those who voted for the opposition and discrediting opposition parties.”-The Washington Post.
 
Back
Top Bottom