Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

Pole Mkuu, Lakini inaonesha mwenyewe ndio unaupenda huo umasikini,

1) kwanini usitafute spare time ukamfuata huyo mchungaji na kumlilia hilo jambo lako?! Ili atizame anakusaidiaje?

2) kwanini usiwafuate hao jamaa zako waliojipata ukawalilia hilo jambo lako?!
washkaji nime wasendia Cv.
nilipo wauliza kuhusu mishe wanadai mambo saiz hayajakaa sawa
 
Hongera mkuu kwa kuiona hii tofauti na ikakusumbua. Hii ni hatua muhimu sana katika ukuaji wako! Tengeneza ukaribu na hawa vijana wenzako na uwe tayari kuanzia chini na kufanya kazi kwa juhudi,maarifa na uaminifu mkubwa. Kama wewe ni mwalimu acha mara moja kwa sababu hiyo kada kwa nchi yetu imetelekezwa!
 
Hongera mkuu kwa kuiona hii tofauti na ikakusumbua. Hii ni hatua muhimu sana katika ukuaji wako! Tengeneza ukaribu na hawa vijana wenzako na uwe tayari kuanzia chini na kufanya kazi kwa juhudi,maarifa na uaminifu mkubwa. Kama wewe ni mwalimu acha mara moja kwa sababu hiyo kada kwa nchi yetu imetelekezwa!
ahsante chief, ndio mimi ni mwalimu wa kiswahili na civics
 
Nimerudi nyumbani huu mwisho wa mwaka kama ilivyo jadi yetu tulio wengi.

Nimewakuta Baba na mama hali si shwari, nikicheki madogo all eyes on me, na mmoja anashughulikia mikopo ya elimu ya juu mwaka huu ila mambo bado tafrani.

Juzi tulivyoenda ibadani kukatokea mchango wa ujenzi na ukarabati wa nyumba ya ibada, daah washikaji wa rika yangu wamechangia mifuko ya cement 200, mmoja katoa cheque ya milioni 10 katika maongezi yake anamiliki kampuni ya clearing and forwarding huko mjini. Mwingine kaahidi tipa 20 za mchanga.

Hakika ibada ilifaana sana, mchungaji aliwaita wazazi wa wale washikaji pale madhabahuni na kutamka kwamba hakika mumezaa chema sana na MUNGU amebariki uzao wenu.

Hali ile ilinifanya nijiulize maswali yasiyo na mwisho kuhusu hatma ya maisha yangu pamoja na wazazi wangu.

Mungu why najitafuta lakini sijipati? Dunia hii ni ya wachache? Wazazi wangu wataishi katika umasikini huu wa kutisha hadi lini?

wakati narudi nyumbani na mama yangu kwa mguu, nikawa napitwa na wana wakiwa kwenye tinted za Black athlete crown, Ford ranger, Subaru nk, wakati mimi naendelea kupita kando ya barabara kukwepa tope la mvua hizi.
Utakufa Kwa kihoro... hapo ulipo ndio mtafuto wako... jichanganye Sasa kuiga kunya Kwa tembo yakukute.... Ridhika na unachopata kama unaamini Mungu. Wakati wa Mungu ndio wakati sahihi ilifika zamu yako utajipata .
 
Ww siyo masikini,shida unajilinganisha na wngine,maisha siyo ushindan kaka utapoteza focus na unachokifanya utaanz kutamani vya watu!!

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Umasikini hauvumiliki.
Hali ya wazazi wako ikiwa hoi, na huna cha kusaidia .

Hakika mwanaume wa kweli huwezi kuwa na amani
 
Back
Top Bottom