Washukiwa wa shambulio la kigaidi la "Crocus" wanasema kwamba walikuwa wakisafiri kwenda Kiev kupokea zawadi waliyoahidiwa

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umeiachia Urusi madhaifu mengi kwenye intelijensia yake ikiwemo kutengwa kimataifa katika masuala ya intelijensia.
Madhaifu yapi? Watu wamefanya tukio la ugaidi wamekamatwa ndani ya siku moja na watuhumiwa wanasema yote baada akili kuwarudia wewe upo Maji Matitu unasema Urusi dhaifu daaah.
 
Utawala wa Putin utafanya kila namna Ukraine ibebe hii lawama ili wahalalishe Vita yao.

Ila uzembe wa FSB yao utafichwa.
 
Utawala wa Putin utafanya kila namna Ukraine ibebe hii lawama ili wahalalishe Vita yao.

Ila uzembe wa FSB yao utafichwa.
Hahaha wewe upo Uyole halafu hautaki Ukraine wahusishwe kwa mapenzi yako yaani Putin akusikilize wewe🤣
 
Waongo hao,ila kipondo watachopata watasema tu data zote,na kule hawauliwi ni kiungo kimoja kimoja wanatambaa nacho.
Wasikilize hapa
Your browser is not able to display this video.
 
Bahati mbaya ni kwamba, uwezekano wa hadhara kuujua ukweli ni mdogo sana kuliko uwezekano wa hadhara kujua kile ambacho serikali ya Urusi inataka hadhara ikijue.
 
Madhaifu yapi? Watu wamefanya tukio la ugaidi wamekamatwa ndani ya siku moja na watuhumiwa wanasema yote baada akili kuwarudia wewe upo Maji Matitu unasema Urusi dhaifu daaah.
Hili tukio la ugaidi lisingetokea na kuleta madhara ambayo yameonekana mpaka sasa endapo intelijensia ingekuwa imara.

Kama ni suala la taarifa za kiintelijensia kabla ya ugaidi wenyewe walipewa ila Putin alizipuuza hadharani kwenye media siku 3 kabla ya tukio la ugaidi.

Ingekuwa ni kwenye nchi za magharibi, raia wangekuwa barabarani hivi sasa kumtaka rais ajiuzulu ama bunge limuondoe kwa kura ya kutokuwa na imani naye (impeachment).
 
Unakumbuka tukio la Sept 11 Marekani? Vipi wananchi waliandamana kutaka Rais Bush ajiuzuru? Au bunge lilipiga kura kutokuwa na imani naye?
 
Unakumbuka tukio la Sept 11? Vipi wananchi waliandamana kutaka Bush ajiuzulu? Au bunge lilipiga kura kutokuwa na imani naye?
Bush hakuwahi kupuuza hadharani taarifa muhimu za kiintelijensia zinazohusu usalama wa raia kama ambavyo Putin amefanya.

Kauli ya rais wa nchi ya kupuuza hadharani taarifa muhimu ambazo zingeweza kutumika kuepusha maafa kwa raia ni kauli inayoonesha uzembe mkubwa katika ofisi ya rais.
 
Jibu swali tukio la Sept 11 Marekani Bush alijiulzilu?
Marekani, Ukraine , Uingereza ndiyo wamehusika na tukio la Urusi imeishajulikana kwa mujibu wa uchunguzi wa Urusi.
 
Bahati mbaya ni kwamba, uwezekano wa hadhara kuujua ukweli ni mdogo sana kuliko uwezekano wa hadhara kujua kile ambacho serikali ya Urusi inataka hadhara ikijue.
Wanajeshi wa Urusi wanarecord live, vikosi vingi vya Urusi vipo independent, ama unafikiri ni kauli ya Putin kwamba mkimkamata tu kata sikio? Si Usa si Urusi wenye uwezo wa kuzuia taarifa zisitoke, nchi zote zina watu wenye inside info wanazo leak.
 
Kwa kiasi kikubwa taarifa tulizopata mpaka sasa ni kutoka kwa watuhumiwa walioteswa. Hatuwezi kuujua ukweli kamili kwa staili hiyo.

Kuna mwanajeshi yeyote aliyerekodi live huo msafara wa watuhumiwa kuelekea Ukraine na ana ushahidi kwamba walikuwa wanaenda kupewa zawadi? Ama ni kauli tu zilizotolewa na watuhumiwa?
 
Hizi taarifa bila shaka umezipata kutoka "RADIO KOMBOLELA"
 
Kwahiyo tuamini za kwako hapo Kimara bonyokwa, kisa unaitwa the great?!!
 
Upo sahihi Sana mkuu. Hao jamaa kutokana kibano walichopewa kwenye interrogation lazima waseme chochote kile ambacho serikali inataka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…