Urusi inafanya "plot twisting" kwenye hii issue ya shambulizi la kigaidi.
Siku chache zilizopita, Putin alirudia yale madai yaliyokuwa yakisambaa awali kabisa kuwa magaidi walikuwa wakikimbilia Ukraine. Akatuachia swali tujiulize kwamba ni kwa nini walitaka kwenda Ukraine.
Saa kadhaa baadaye, mshirika wa karibu wa Putin, rais wa Belarus, Alexander Lukashenko, akadai kwamba magaidi walikuwa wakielekea Belarus kwanza ila walikutana na vizuizi (vituo vya ukaguzi ama checkpoints) ndipo wakabadili njia ili kuelekea Ukraine. Na akasema kuwa atatoa ushirikiano wa kiintelijensia kwa Urusi kuhusiana na hilo.
Hii statement ya Mzee Lukashenko inaonekana kuleta mkanganyiko mkubwa ukilinganisha na kauli za viongozi mbalimbali wa Urusi.
Pia, saa chache baadaye, mkurugenzi wa FSB (hili ni shirika la ujasusi la Urusi), akadai [bila uthibitisho] kuwa Marekani, Uingereza na Ukraine ndio walioratibu na kuwezesha shambulizi la Moscow huku Ukraine ikitajwa kama mhusika wa kutoa mafunzo kwa "magaidi" katika eneo lisilojulikana ndani ya Mashariki ya Kati.
Hiyo statement pekee inaonesha uzembe wa hali ya juu na ingetosha wakati uleule kumfuta kazi huyo mkurugenzi.
Hilo la watuhumiwa kwenda Ukraine "kupokea zawadi" ni jipya katika mtiririko wa matukio na huenda tukasikia mengine mengi zaidi ya haya.
Madai karibu yote kuhusu Ukraine kuhusika yanasemekana yametokana na kauli za wale watuhumiwa wa ugaidi mara baada ya kufanyiwa mahojiano. Tatizo ni kwamba, kauli zinazotokana na watuhumiwa waliopitia mateso wakati wanahojiwa huwa sio za kuaminika kwa namna yoyote ile.