Mzee Es,
Mimi sina beef na maoni yako na wala hayawezi kubadilisha kitu kwa mwenye macho. Na kumbuka kwamba hata wewe unaweza kusema swala likaonekana NONSENSE kwao sio iwe wewe tu mjuzi wa kufikiri. Nitarudia kusema kwamba unafanya hasira na hazina kificho kwa sababu hupendi mtu aseme unachosema wewe ni nonsense ila wanachosema wengine. Hili neno kama unapenda kulitumia basi nawe kuwa MUWAZI kukubali linapotumika kwako na hawa jamaa. Na nakuomba unielewe kwamba sisemi unayoandika ni nonsense isipokuwa huna points nzito za kuhalalisha udhanifu unaojenga fikra hizi za udini.
Sam,
Kwanza tafsiri yako imefunga mada hii. Na ikiwa mtu haelewi unachosema hapa basi hawezi kuona deep ndani ya swala hili.
Lets say, JK hakutumia dini kuwa kielelezo cha uchaguzi wake jibu lake rahisi sana. Hawa watu wanafaa kazi ile...
Mkapa alipoingia mwaka 1995 alibadilisha sekretarieti alitangaza mara moja kusitisha uhai wa sekretarieti ya CCM (Miwnyi) wakati huo chini ya Katibu Mkuu - Bw. Lawlence Ghama na kuweka yake mpya. Kwangu binafsi that was a political move kuweka watu waliokuwa upande wake bila kujali dini zao. Kisha Mkapa huyu huyu aliondoa sheria ya kuajiriwa maisha ndani ya chama na kuweka miaka mitano tu. Which was a good move kwa chama chao na ilitakiwa kila mwajiriwa lazima atume application kwa nafasi zake. Aliyofanya JK is the same na hakubadilisha sheria isipokuwa watu. Ikiwa waislaam ndio wanamuunga mkono zaidi ndani ya CCM (mtandao) basi huko CCM kumeisha ingia udini, mnachotakiwa kutueleza sisi ni huo udini ndani ya CCM. Nadhani tutakuwa wazi kukubaliana kwamba tabaka hizi za mitandao zinaongozwa na dini.
Kuhusu Uteuzi wa Mabalozi, JK kawaondoa mabalozi wengine ni waislaam tena wa mkeka na kuweka hao. Mtu kama Mapuri ambaye ambaye alikuwa ktk sekretarieti ya Mkapa kaondolewa huko na kupewa Ubalozi China kwa sababu Mapuri ndani ya Chama alikuwa mtu wa Mkapa.
Hakuna kificho kwamba kuna beef kati ya JK na Mkapa kama tulivyoelezwa na Mzee Es ingawa sioo wazi na ukiangalia swala la balozi wa Italy hili swala lilizungumziwa long time na Mkapa alijua kinachoendelea huko Rome. Soma blog hii ya mshikaji utapata picha kamili
http://kurunzi.blogspot.com/
Na kama kweli JK anatumia udini basi angevuruga Viongozi wote wa ngazi za juu serikalini na mabalozi kwa sababu hawa ndio wawakilishi wa nchi nzima ktk taasisi zote.
Mwisho, umeniuliza kama sasa tuna apply Newton's third law of motion. No brother, labda hukusoma vizuri maelezo yangu. Mimi najaribu kufuata nyayo zenu kimawazo. Yaani kama anavyosema Mzee ES hataki kuona makosa yakitendeka leo, kesho iwe kazi kuwaeleza wajukuu. Je, ikiwa dhana yako ni potovu utawambia watoto wako pia makosa yako. Vigumu sana binadamu kula mavi yake mwenyewe na ndicho mnachofanya hapa. Ikiwa waislaam wengi JK ajihadhali lakini ukweli ni wakristu wengi afanye nini? hili ndilo swali langu kwenu. Binafsi nimesema niliyaona yote haya toka mwanzo na sikuyaona kama udini na kunahitajika marekebisho.
Haya sio mageni na ushahidi wenyewe mumeuweka wazi hali ilikuwa ikijulikana hivyo toka awali. Kwa nini msifanye kutafuta ukweli kabla hamjashutumu. Na pia kwa nini msichukulie kuwa uchaguzi ni political move ambayo JK mwenyewe lazima ashauriwe na watu wake (Mtandao) isipokuwa dini.
What does he gain?..ikiwa nchi yetu haina udini!.. Je, yeye mjinga kiasi ambacho anafahamu Pengo na wakristu wanatazama kila move zake. Udini tunao sisi mshikaji hilo kubali...na sisi ndio tutakao karibisha vita vya kidini. Kumbuka mchungaji wa Rwanda ambaye alitangaza redioni kuanzisha mauaji ya Watusi wote huyu hakuwa kiongozi wa serikali bali mchungaji tu na kachagua kabila lake.