Wasichana 3,333 warejeshwa shule, ni waliokataliwa na serikali ya hayati Magufuli

Wasichana 3,333 warejeshwa shule, ni waliokataliwa na serikali ya hayati Magufuli

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wasichana 3,333 sawa na 111% wenye umri kati ya miaka 13 hadi 21 waliokatisha masomo ya elimu ya sekondari kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokana na mazingira magumu, kupata ujauzito na ndoa za utotoni wamerejeshwa shuleni mwaka 2021/2022.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima(TEWW), Dk Michael Ng’umbi ameyasema hayo wakati akielezea shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti ya 2022/2023.

“Tutajitahidi mwaka huu mwingine tujitahidi tupate namba hiyo hiyo ili waanze tena Januari mwakani,” amesema.

Dkt. Ng’umbi amesema programu hiyo ni kwa ajili ya wale waliokatiza masomo kwa wanafunzi wa sekondari tu.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali ambalo linajishughuliasha na Wanawake na Watoto (Wowap), Fatma Toufiq amesema hatua hiyo ni kubwa ya kuwawezesha wasichana hao kutimiza ndoto zao walizozikatisha kwasababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata ujauzito kutokana na kutokuwa na elimu sahihi ya afya ya uzazi.

“Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kubali watoto hawa waweze kurejea shuleni. Hawa wamekuwa majasiri, hawakuogopa kunyanyapaliwa. Wanachotakiwa kufanya ni kufuata mambo yaliyowapeleka pale, wasirudie tena makosa kwasababu kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa ndio kosa,”amesema Fatuma ambaye pia ni mbunge wa viti maalum.

Novemba 2021, aliyekuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alitangaza uamuzi wa Serikali wakuruhusu wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliokatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali kurejea shuleni.
 
Halafu wengi wao huwa hawana future nzuri ya kuendelea na elimu! Ila ni kufundisha umalaya tu mabinti waliojitunza!
Huu ni ujinga kurudisha watu ambao walishajifungua shule. Hapa hapana tunataka kiwafundisha mabinti kuwa kugegedwa wakiwa shule ni sawa tuu maana ata wakizaa fresh tuu.

Ila wapuuzi wakubwa ni wazazi. Maana hawa wazazi ndio wanakubaliana na huu ujinga na kuwasaidia hao watoto wao kulea vijukuu. Hapa marehemu alikuwa sahihi kabisa.
 
Mtoto wa miaka 17 kushuka chini haifai kumuhukumu kuwa ni malaya na kumtelekeza. Ni umri ambao anahitaji watu wazima wamuongoze katika njia sahihi ya kusahihisha makosa anayoyafanya. Samia yupo sahihi sana.
Hamna kitu kama hicho huyo mtoto alijifunza wapi mambo ya kugegeduana kama sio uzembe wa wazazi wake. Kwanza mie ningetia lockup mzazi yoyote yule ambay binti yake anapata mimba
 
Kwa taarifa yako hao wanaosoma vyuo ni ndo malaya wa kutupwa! Serkali iwape elimu ya Kitendo wajitegemee ila kuzurula vyuo ni kwenda kuongeza umalaya tu!
Idadi ya wahitimu wa kike kwa takwimu za miaka 5 iliyopita inaweza kuwa kwenye laki 6 katika level zote. Malaya uliowashuhudia ni % ngapi ya hao wahitimu?
 
Hamna kitu kama hicho huyo mtoto alijifunza wapi mambo ya kugegeduana kama sio uzembe wa wazazi wake. Kwanza mie ningetia lockup mzazi yoyote yule ambay binti yake anapata mimba
Sawa, huo ni mtazamo wako mzabzab, mwingine ana mtazamo wa kunyonga n.k wazazi wenye mabinti waliopitia hayo wana bahati kuwa watu wenye mitazamo aina yako hawapo katika nafasi za kufanya maamuzi.

Kwa sasa mtazamo wa nchi ni kuwa mabinti wanaopata ujauzito wapate nafasi nyingine ya kusahihisha makosa kwa kuendelea na masomo
 
Trust me twenty years down the line ndio tutakapojua ilikuwa sahihi au lah.
Time will tell
 
Trust me twenty years down the line ndio tutakapojua ilikuwa sahihi au lah.
Time will tell
Twenty years before imetupa malaya wa leo waliopata mimba wakiwa mashuleni wakati huo?
 
Watoto wanamwachia nan? Sababu kuna sheria kidume ukitia mimba msichana mwanafunzi unaenda jela
 
Back
Top Bottom