Wasichana 3,333 warejeshwa shule, ni waliokataliwa na serikali ya hayati Magufuli

Wasichana 3,333 warejeshwa shule, ni waliokataliwa na serikali ya hayati Magufuli

HONGERA AWAMU YA SITA, UNANYIMA HAKI ZA KIMSINGI WATOTO 3,333 HUU ULIKUWA NI UFASHISTI NA UKATILI WA HALI YA KIWANGO CHA JUU KABISA NA UKANDAMIZAJI ULIOPITILIZA.
Alivyokua anaitafuta mimba hakujua mbele kuna kikwazo cha kuendelea kusoma? Magufuli alikuwa sahihi kabisa.
 
Hauwezi kuwachanganya wazazi na watoto wakae wasome pamoja,mtatuharibia watoto wetu ilitakiwa mjengewe madarasa yenu
Kwahiyo unaona kua na taifa la wajinga ni bora kuliko kua na wanafunzi wazazi.Nchi lazima liende na yote kwa pamoja.kuelimisha jamii yake na kulea watoto wanaozaliwa kwenye taifa husika.Tusijifanye tuna misimamo sana wakati mambo mengine tu ya kawaida yametushinda.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Huu ni ujinga kurudisha watu ambao walishajifungua shule. Hapa hapana tunataka kiwafundisha mabinti kuwa kugegedwa wakiwa shule ni sawa tuu maana ata wakizaa fresh tuu.

Ila wapuuzi wakubwa ni wazazi. Maana hawa wazazi ndio wanakubaliana na huu ujinga na kuwasaidia hao watoto wao kulea vijukuu. Hapa marehemu alikuwa sahihi kabisa.
Ujinga ni huu yakuona kuzaa ni kosa ila kukosa elimu sio kosa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Asante mama samia kwa kuwapatia haki yao y kikatiba.
 
Kuna watu wanaotetea legasi watanuna sana kwa hili
 
Team haki meno nje ! Mkimalza hapo nendeni mkalitazame na lile la kuwafunga baba wa hao watoto! Hamuoni ni kumnyima mtoto haki ya kumjua babaake? Halafu tuanze kuangalia series yetu.
 
Wasichana 3,333 sawa na 111% wenye umri kati ya miaka 13 hadi 21 waliokatisha masomo ya elimu ya sekondari kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokana na mazingira magumu, kupata ujauzito na ndoa za utotoni wamerejeshwa shuleni mwaka 2021/2022.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima(TEWW), Dk Michael Ng’umbi ameyasema hayo wakati akielezea shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti ya 2022/2023.

“Tutajitahidi mwaka huu mwingine tujitahidi tupate namba hiyo hiyo ili waanze tena Januari mwakani,” amesema.

Dk Ng’umbi amesema programu hiyo ni kwa ajili ya wale waliokatiza masomo kwa wanafunzi wa sekondari tu.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali ambalo linajishughuliasha na Wanawake na Watoto (Wowap), Fatma Toufiq amesema hatua hiyo ni kubwa ya kuwawezesha wasichana hao kutimiza ndoto zao walizozikatisha kwasababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata ujauzito kutokana na kutokuwa na elimu sahihi ya afya ya uzazi.

“Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kubali watoto hawa waweze kurejea shuleni. Hawa wamekuwa majasiri, hawakuogopa kunyanyapaliwa. Wanachotakiwa kufanya ni kufuata mambo yaliyowapeleka pale, wasirudie tena makosa kwasababu kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa ndio kosa,”amesema Fatuma ambaye pia ni mbunge wa viti maalum.

Novemba 2021, aliyekuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alitangaza uamuzi wa Serikali wakuruhusu wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliokatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali kurejea shuleni.

Miaka yote tangu Uhuru 1961 msichana wa shule au chuo cha elimu akipata ujauzito ilikuwa ndio mwisho wa yeye kusoma. Kama mwaka huu au mwaka jana wanaruhusiwa kuendelea na masomo ni jambo jipya labda zuri. Cha ajabu hapa anasemwa Maghufuli ndiye aliyekataa wasiendelee na masomo. Kwa vyovyote vile kama wanafikia 3,000 watakuwepo na wa awamu za kabla ya Maghufuli. Je shule za madhehebu ya dini nao wameanza kuruhusu wanafunzi waliopata ujauzito shuleni kuendelea na masomo? Sidhani kama wataruhusu. Na kama hawaruhusu unaonaje serikali kujifanya kuwa na huruma kwa raia kuliko dini zenye lengo la kuwaongoza watu kumwona Mungu?
 
Watasoma wenyewe au watasoma na hao ambao bado kujifungua ?
 
Back
Top Bottom