Wasichana 3,333 warejeshwa shule, ni waliokataliwa na serikali ya hayati Magufuli

Tukisema wanawake ni kundi maalum muwe mnatuelewa sio mnakaza ubongo
 
Way
Watoto wanamwachia nan? Sababu kuna sheria kidume ukitia mimba msichana mwanafunzi unaenda jela
Wanaoruhusiwa kuja na watot na yaya yupo wa kuwaangalia.. akimaliza kisomo anachukua Mtoto nyumbani... Mtoto akisumbua anaitwa toka darasan ambembelezee.. kisomo na kulea pamoja
 
Hiyo itakuwa shule au ustawi wa jamii?
 
Wasichana 3,333 sawa na 111% wenye umri kati ya miaka 13 hadi 21 waliokatisha masomo ya elimu ya sekondari kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokana na mazingira magumu, kupata ujauzito na ndoa za utotoni wamerejeshwa shuleni mwaka 2021/2022.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima(TEWW), Dk Michael Ng’umbi ameyasema hayo wakati akielezea shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti ya 2022/2023.

“Tutajitahidi mwaka huu mwingine tujitahidi tupate namba hiyo hiyo ili waanze tena Januari mwakani,” amesema.

Dk Ng’umbi amesema programu hiyo ni kwa ajili ya wale waliokatiza masomo kwa wanafunzi wa sekondari tu.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali ambalo linajishughuliasha na Wanawake na Watoto (Wowap), Fatma Toufiq amesema hatua hiyo ni kubwa ya kuwawezesha wasichana hao kutimiza ndoto zao walizozikatisha kwasababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata ujauzito kutokana na kutokuwa na elimu sahihi ya afya ya uzazi.

“Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kubali watoto hawa waweze kurejea shuleni. Hawa wamekuwa majasiri, hawakuogopa kunyanyapaliwa. Wanachotakiwa kufanya ni kufuata mambo yaliyowapeleka pale, wasirudie tena makosa kwasababu kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa ndio kosa,”amesema Fatuma ambaye pia ni mbunge wa viti maalum.

Novemba 2021, aliyekuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alitangaza uamuzi wa Serikali wakuruhusu wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliokatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali kurejea shuleni.
Yuko wapi Cyprian Musiba aaligongelea !!
 
Sasa Nimekubali samia alikuwa mpinzani wa JPM
 
Attachments

  • 0556ABBA-6301-47A3-8D0E-A8D421A600C7.jpeg
    0556ABBA-6301-47A3-8D0E-A8D421A600C7.jpeg
    87.7 KB · Views: 2
Back
Top Bottom