Acha Uvivu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 524
- 131
Tabia ya madada kuacha kucha ndefu bila kupunguza imefikia mahali tuulize kuwa ni kwa kusudi gani hasa. Hivi karibuni nilikuwa safarini toka Tanga wilaya ya Handeni. Kuna dada alipanda kwenye gari ambayo ilijaa sana. Katika harakati za kupanda na kupata nafasi mdada huyo alimparua babu mmoja usoni damu ikaanza kutoka. Madada huu utamaduni wa kukuza kucha ni vema mkaweka wazi kusudi lenu ili watu wasije anza chukia. Kwa nini mnaacha kucha ndefu jamani?