Hamna njia rahsi ya kukaa na dada wa kazi na kudumu nae kama UPENDO ukitaka dada wa kazi adumu kwako mpende na mthamini kama unavyojithamini
kwanza tutambue kuwa huyo ni msaidizi wa kazi na sio mfanya kazi,maana yake ni wewe mama unapokua nyumbani huna kazi basi shirikiana na dada kufanya kazi pamoja
lakini pia tafuta kitu cha kumfunga huyo dada wa kazi,yani mfunge awe wako mpk utakapo amua wewe Aende au vinginevyo,Kuna vitu vingi unavyoweza kuvifanya kwa dada wa kazi ukam BLOCK
1.Mpeleke shule ya Ufundi Cherehani/Upishi
Mlipie ada tafuta shule ya bei nafuu kbsa awe anaenda kila j5 au kila jmosi anaenda hko anajifunza mapshi au ufundi kisha anarudi,unakua unampa ahadi akimaliza mafunzo vzr akiweza utamfungulia ofisi ya cherehani,huyo dada atakuaakifanya kazi kwa bdiii sana kwa sababu unampenda lkn pia unamuendeleza,mawazo ya kuku udhi atayaondoa na atakua makini kwa hali kubwa sana ili asikuudhi.
2.Mfungulie biashara Hapo Hapo home
najua hukosi friji mruhusu atengeneze ice cream,mnunulie mahitaji ya ice cream ambayo mahtaji hayazidi hata 10,000 muwekee tangazo hapo nnje kama atauza vi ice cream na barafu,hela itayopatkana Muachie iwe yake"USICHUKUE HATA SENT" tena siku moja moja unaweza ukamtania ukamwambia "dada naomba nikopeshe 500" hawezi kukosa atakupa then utakaa nayo baada ya siku mbili unamrudshia..
Hii tunafanya si kwasababu tunapesa za kuchezea ila tunafanya vitu vya kumfunga huyu dada wa kazi awe wetu milele na daima.
Unaweza mnunulia Gunia la mkaa ukamwambia awe anauza mkaa hapo nnje,muache auze mkaa wake atapanga mkaa wake nnje kisha atarudi ndani kufanya kazi zake,mtu aktaka mkaa atamuita ataenda,Atakua anapata hela za mshahara wake kuptia biashra zake kwakua ww boss upo na unaona biashara zinavyoenda na wewe ndio unaemnunulia vitu Unaweza kbsa kujua hizi biashara zake zinaenda au haziend,Kama umeona haziend ikifka mwsho wa mwezi mpe mshahara wake kama kawaida.
Usiruhusu awaze et biashara mbaya ntakosa hela,hapana hizi biashara n changa la macho kwa dada wetu wa kazi ili awe loyal kwetu Atutunzie watoto wetu,alinde nyumba yetu yenye thamani ya mamilioni,Atunze afya zetu zenye thamani isiyoweza kutamkika,huyu n zaidi ya dada wa kazi lazima tutumie kila mbinu ili kumfanya ajione Kapata BOSS bora.
Njia za kuishi na dada wa kazi zipo nyingi sana ila lazima ukubali kujitoa kwa ajili yake hyo haitoshi pia upendo usio wa kinafki umuonyeshe dada,nakuambia huyu mdada wa kazi siku akikosea ukamtshia kumfukuza Atakulilia mpk utashangaa,na ukimsamehe hatokaa arudie hilo kosa milele.