Wasichana wa kiislamu wamekamatwa wakiwa wamefungiwa kwenye nyumba Dodoma, inayosadikika kupewa elimu ya dini

Acha Umbea na Uzushi wewe...weka hapa hiyo taarufa ya uchunguzi na Utafiti

Usupoweka wewe ni MWONGO kama kawaida yako
 
Mwongo huyo Mzee hujamjua tu....ila anapaswa hata kuona Aibu kwa umri wake huo
 
acha kupotosha , sio sahihi kukatisha masomo ya watoto , msiwe wapumbav kias hicho hao Iran na saudia wanasomesha wasichana wao kwan nyie mna dini zenu nyingine mbali na hz za wasaudia na Iran?
Mpumbavu ni wewe ambaye umekurupuka kunijibu bila kunielewa
 
Hizo ni hekaya za Abunuas.
 
Huyu Mzee hata kusoma post zake huwa sipendi maana amejaa udini na uongo tu
 
Hakuna kitu kama hicho. Kawadanganye wasiokujua
 
Walianzisha harakati za kudai uhuru sawa lakini hawakuwa na elimu Dunia ndio maana wakamhitaji mtu anayeona mbali mwenyeelimu ya kutosha yaani Kambarage wa Butiama
 
Walianzisha harakati za kudai uhuru sawa lakini hawakuwa na elimu Dunia ndio maana wakamhitaji mtu anayeona mbali mwenyeelimu ya kutosha yaani Kambarage wa Butiama
Niz...
Unahitaji kuijua historia ya uhuru wa Tanganyika ili kuweza kuchangia kwa uhakika.

Wote walioasisi African Association mwaka wa 1929 walikuwa na elimu kwa kiwango cha wakati wao.

Halikadhalika mabadiliko makubwa yalipofanyika ndani ya TAA mwaka wa 1950 viongozi waliokuwapo wakati huo walikuwa wameelimika kwa kiwango cha nyakati hizo.

Alikuwapo Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Wilbard Mwanjisi na mdogo wake Roland Mwanjisi, Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Luciano Tsere, John Keto, Thomas Saudtz Plantan, Schneider Abdillah Plantan, Ramadhani Mashado Plantan, Erica Fiah, Clement Mohamed Mtamila, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo na katika majimbo walikuwapo wazalendo wengi kama hawa, Kanda ya Ziwa kulikuwa na Paul Bomani, Ali Migeyo, Sued Kagasheki.

Hawa walikuwa wameelimika vya kutosha.
TAA hakikuwa chama kinachoongozwa na watu wajinga.

Wala kilichomfanya Julius Nyerere apewe uongozi wa TAA mwaka wa 1953 si elimu yake pekee.

TAA ilimuhitaji kiongozi Mkristo akamate nafasi ya juu ili kuleta umoja wa Watanganyika vinginevyo laiti kiongozi wa harakati za uhuru angekuwa Muislam vuguvugu lote lile lingechukua sura kuwa ni Waislam peke yao ndiyo wanaochochea wananchi kudai uhuru.

Hili lingesababisha kwa Waingereza kuwashawishi Wakristo na wao waunde chama chao.

Tanganyika ingeingia katika siasa za kudai uhuru ikiwa imegawanyika.

Huu ndiyo ulikuwa msimamo na fikra ya Hamza Mwapachu mtu aliyemwingiza Nyerere katika harakati za uhuru Dar es Salaam kupitia kwa Abdul Sykes.

Wakati Nyerere alinafika Dar es Salaam mwaka wa 1952 hawa ndiyo walikuwa viongozi wa TAA wakiendesha mambo kupitia TAA Political Subcommittee: Dr. Vedasto Kyaruzi (President), Abdul Sykes (Secretary), Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Hii ndiyo historia ambayo wengi hamuifahamu.

Ukitaka kuijua historia ya uhuru wa Tanganyika nakushauri usome kitabu cha Abdul Sykes.

 
Hakuna kitu kama hicho. Kawadanganye wasiokujua
Niz...
Ikiwa huamini sawa.

Hapa tunabadilishana fikra na kila mtu ana nafasi ya kueleza kile anachokijua.
Inawezekana wewe hujui yaliyotokea baada ya maandamano ya Waislam dhidi ya NECTA kuwa mitihani ilirudiwa kusahihishwa upya na haki ikatendeka.

Faida ya majadiliano ni kuwa wako ambao hawakuwa wanajua haya na sasa baada ya kusoma niliyoandika wamejua.

Hili si suala la mimi kujulikana.
Kufahamika kwa hakika nafahamika sana hapa JF na kwengineko.
 
Pili ajibu walitaka mitihani yasitumike majina zitumike Namba wanajuaje kuwa waislamu waliofeli idadi Yao wakati Namba ndio zinatumika sio majina?
 
Wewe ni mzee wa hovyo na mpotoshaji mkuu unaezeeka na uendawazimu wako.
 
hii haitoi exemption kwamba hawa wasihadhibiwe wote ni waarifu tu.
tunahitaji watoto wetu waende shule.
wawe waisilamu au wakristo na si vinginevyo.
hivyo wanaofanya hivyo hawana haki!
Wakasomee siasa kali?
Wakiumwa watoto wa nani wakawatibu?
Mna wakatisha watoto elimu alafu ndio wanakuwaja kuwa watumwa wa ngono miaka 12 tu?

Mbona wafuasi wa Yesu, wakristo wanafanya elimu ya dini KIFUNGILO GIRLS, CANNOSA, ST FRANCIS MBEYA, ST MARGORETH MOSHI KILIMANJARO, Usa Seminary, MAU SEMINARY, Livingston Sec Tanga, RUBY SEMIANRY, LOMBETA, ST DOCAS huku kote mbona wanafundishwa kuhusu Yesu na wokovu?
 
Hizo ni hekaya za Abunuas.
Niz...
Hapana hapa hakuna utani tunajadili mambo mazito katika jamii yetu.

Angalia picha ya huyu kijana hapo chini yupo na amekutwa na watoto ambao inadaiwa wanafunzwa mambo machafu.


Hizi si hekaya.
Huu ni ukweli.

Huyo hapo chini ni Sheikh Yusuf Muhammad mwalimu anasomesha Uislam na kuhifadhisha Qur'an.


Sheikh Yusuf Muhammad
Haya si hekaya ni mambo yenye kufahamika.

Ila Sheikh Yusuf Muhammad madrasa yake wanafunzi wake wana nafasi ndogo ya kuishi na hawana maji ya bomba.

Lakini kamwe hapo hapafunzwi uchafu.
Tatizo ni madrasa haina maji ya bomba na nafasi ndogo.

Huu ndiyo ukweli.
Angalia picha ya wanafunzi hapo chini:

 
Wewe ni mzee wa hovyo na mpotoshaji mkuu unaezeeka na uendawazimu wako.
Muc...
Bahati mbaya umeghadhibika na unanitukana.

Ungekuwa uko katika hali ya utulivu ungeweza kuandika ukaonyesha yale ambayo napotosha.

Ungefanya hivyo ungetoa nafasi ya wengine kujadili.
 
Muc...
Bahati mbaya umeghadhibika na unanitukana.

Ungekuwa uko katika hali ya utulivu ungeweza kuandika ukaonyesha yale ambayo napotosha.

Ungefanya hivyo ungetoa nafasi ya wengine kujadili.
Unawapotosha waislam wenzako kuwa wanafelishwa kwa makusudi baada ya kuwahusia wasome kwa bidii waache kujifungia ndani kusoma elimu ahera kama hao mabinti
 
Wakifungiwa akina Paulina mnaandika watz.
 
Huyu Mzee hata kusoma post zake huwa sipendi maana amejaa udini na uongo tu
Niz...
Itakuwa bora sana ukaweka hapa yale ambayo unaona ni ya uongo.
Mimi sijaandika udini.

Nimeandika historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo ilifutwa historia ambayo ilijipambanua kwa kuwarudisha katika historia ya Tanganyika Waislam waliopigania uhuru.

Ikiwa hupendi kusoma post zangu si tatizo.
Sina shida ya wasomaji.

Kalamu yangu inasomwa na watu wengi sana.
Nashukuru.

 
We mzee mudi chenga sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…