Mam...
Mimi nimeeleza tatizo hili kama ninavyolijua.
Sikulazimishi kukabaliana na mimi.
Ila najua Sheikh Yusuf Muhammad alikuwa anasomesha Uislam na kuhifadhisha Qur'an.
Haya ni mambo makubwa yenye heshima ya kipekee katika Uislam.
Kuna watoto wa Kiislam wananyimwa elimu kwa dhulma na hakuna anaelisemea.
Leo tunawasomesha watoto wetu elimu nyingine wewe unakuja na hoja ati wananyimwa elimu.
Angalia hapo chini:
Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu.
Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu.
Asilimia 29 ni wengine.
Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21.
Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe.
Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.
Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu.
Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga.
Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha.
(Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999).
Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999 Mohamed Said February 17, 2015 0 Annur Na.187- Feb....
mohamedsaidsalum.blogspot.com