Mam...
Mbona unachanganya mambo?
Unajua kuwa serikali ilivunja EAMWS ili kuzuia Waislam wasijenge Chuo Kikuu?
Unajua kuwa serikali ilikataa kutoaa kibali kwa OIC kujenga ChuoKikuu Tanzania?
Unayajua yaliyokuwa yakifanyika Wizara ya Elimu na NECTA?
Haya ndiyo ninayozungumza mimi.
Kuhusu madrasa ya wasichana Dodoma hakuna kibaya kilichokuwa pale.
Madrasa haina ubaya wowote katika maadili na mafunzo yake.
Tatizo waliloona waliokwenda kukagua ni mazingira.
Haya mazingira wanadai ni duni.
Kipi cha ajabu hapo katika Tanzania hii?
Kuteka maji kwenye kibwawa leo imekuwa kitu cha ajabu?
Kote huko vijijini kuna maji ya bomba?
Halaumiwi mtu kwa kula ugali na papa wa kuchoma kila siku wala hakamatwi kuwa kafanya kosa.
Msongamano katika nyumba ni kosa?
Walichokitafuta hapo hawakukipata Allah katusitiri.
Hakuna mabinti wanaodhalilishwa.
Wanasema walimu watakuwa chini ya polisi na madrasa inafungwa.
Utadhani kuna jinai.
Lakini ndugu yangu una habari kuwa kuna kituo kimegunduliwa kinawafunzi watoto uchafu?
Hebu fananisha madrasa yetu na hiyo ya Wazungu ambao hata kuzungumza na viongozi waliofika hapo walikataa.