Wasichana wa kiislamu wamekamatwa wakiwa wamefungiwa kwenye nyumba Dodoma, inayosadikika kupewa elimu ya dini

Wasichana wa kiislamu wamekamatwa wakiwa wamefungiwa kwenye nyumba Dodoma, inayosadikika kupewa elimu ya dini

yaani kumbe issue ya kutumia namba ilikuja baada ya ndugu zake huyu mzee kuomba wapendelewe wakiamini majina yakiwepo wanaonewa, lakini bado tu wanashika mkia. namwuliza kwani wasahihishaji ni wakristo peke yake, anashindwa kujibu ati kuna research, research against who? kwahiyo hiyo research ilionyesha mitihani walisahihisha waalimu wakristo peke yake wakawafelisha wanafunzi waislam au ni nini sasa?

au mnaonaje tuiombe serikali kwenye mitihani yao wawawekee 100% wote ila wengine wasio walalamishi wasahihishiwe kwa kawaida, waende sekondary nako waamue kufanya mtihani au hata kutofanya ila wapate marks 100%, form six na vyuo pia wasapitishe tu kwa kuwapa marks za bure ili waridhike.

siku zote nimeeleza, malalamiko kama haya wanayo hawa ndugu katika imani wa manzese na buguruni ambao mtoto akizaliwa anawaza madrassa tu ila elimu dunia anategemea apeleke kayumba, imeisha hiyo. wale ndugu katika imani wa masaki, mikocheni, mbezi beach n.k watoto wao hawana hayo mambo ya ajabu na wanafaulu mno. wewe mimi mtoto akizaliwa na kufika miaka 4 ninachowaza ni aende chekechea wakati Mohamed said anawaza aanze madrassa, muda ule anapoteza madrassa mimi wa kwangu anajifunza kusoma. wakija kuingia wote darasa la kwanza wa kwangu ameshazoea ana mumkari wa mambo ya shule wakati yule mwingine anawaza tu madrassa shule kidogo sana. unafikiri ukimweka darasa moja atamshinda mwanangu kweli? never, mfumo wa imani yenu sio friendly kwa elimu dunia, khapo ndipo mood alipobugi, na kwa hakika uislam halisi hauwezi kuikubali elimu dunia hasa ya wamagaribi, shida ni kwamba iliyopo ndio hiyo tu hakuna elimu ya waarabu, hawana, bure kabisa. imani sio friendly kwa elimu dunia wakati mnaishi kwa kutegemea elimu dunia. hata wale bokoharam ambao wanapinga elim ya magharibi, bunduki wanatumia iliyotengenezwa na mtu aliyesoma elimu ya magharibi, nguo wanavaa technolojia ya magharibi, simu wanazotumia kila kitu vinatokana na elimu dunia na hapohapo wao wanapinga elimu dunia, kama sio upumbavu ni nini hiyo sasa? dini gani hiyo?


Imani ni shambulio la akili
 
dodoma misikiti imechipuka ghafla sana na inafadhiliwa na watu wa nje

ifatiliwe sana
kuna tishio kubwa la kiusalama huko mbele

nb
dodoma ndio mji mkuu wa kiselikali
miundo mbinu yote iko pale maandalizi yankuingamiza nchi hapo ni uwekezJi kama huo kwa miaka mingi ijayo


tushtuke ile misikiti

dar ikulu imehama kuikwepa zanzibar lakin sasa naona adui anatuwahi hatua mbili zaid
Usipende kutengeneza chuki na kudhihirisha ujinga, kwa hiyo uwepo wa misikiti ndio inapelekea tishio la usalama. Dar kuna misikiti zaidi ya 1000 taja tishio moja tu linalotokana na uwepo wa hiyo misikiti.
Muislam akitetea/kujifunza dini yake anaitwa gaidi. Tubadilike tusiwe na mawazo mgando
 
Mam...
Mimi nimeeleza tatizo hili kama ninavyolijua.
Sikulazimishi kukabaliana na mimi.

Ila najua Sheikh Yusuf Muhammad alikuwa anasomesha Uislam na kuhifadhisha Qur'an.

Haya ni mambo makubwa yenye heshima ya kipekee katika Uislam.
Kuna watoto wa Kiislam wananyimwa elimu kwa dhulma na hakuna anaelisemea.

Leo tunawasomesha watoto wetu elimu nyingine wewe unakuja na hoja ati wananyimwa elimu.

Angalia hapo chini:

Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu.

Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu.

Asilimia 29 ni wengine.

Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21.
Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe.

Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.

Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu.

Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga.

Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha.

(Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999).


Huyu mzee ni wa kupuuzwa amejawa na udini mpaka anakuwa mjinga.

Ninachomkubali mzee Kikwete japokuwa ni muislam ila alipinga sana suala la udini kwa hili nampa pongezi huyu mzee.

Wazee kama Mohamed Said sio salama sana kwa Taifa letu.
 
Mam...
Hapana Waislam ni raia kama raia wengine.
Tofauti yao na Wengine ni historia yao.

Hapo ndipo anapokuwa makhsusi.

Waislam wamepambana na Wajerumani kwa silaha.
Naamini unaijua historia ya Abdulrauf Songea Mbano.

Naamini unaijua pia historia ya Khadija Mkomanile.

Hawa wamlinyongwa na Wajerumani kama sehemu ya majemadari wa Vita Vya Maji Maji (1905 - 1907).

Naamini unaijua historia ya Abushiri bin Salim na Mtwa Abdallah Mkwawa.

Waislam ndiyo walioasisi African Association 1929 kupambana na Waingereza.

Waislam ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Waislam ndiyo waliomweka Mwalimu Nyerere kuwa kiongozi aongoze harakatiza za uhuru.

Historia hii ilikwepwa hadi mimi nilipoandikia kitabu cha Abdul Sykes.

Ikiwa hujasoma kitabu hiki kisome utashangazwa na mengi ndani ya kitabu hiki.

Kitabu kimebadili historia si ya Julius Nyerere peke yake bali historia nzima ya uhuru wa Tanganyika.

Sasa ukiangalia hizo takwimu katika hotuba ya Kitwana Kondo Bungeni utaona kuna jambo halijakaa vyema.

Au huoni unaona sawa hakuna kasoro?

Hata utoe historia ya wapi wewe huo udini wako Kwa maslahi mapana ya Taifa wala hatuna kazi nao, yaani umekuwa mdini kupitiliza.

Au upewe Nchi uongoze ulete huo usawa unaodai waislam wamepunjwa?
 
Ficha ujinga wako, Sheria ya uislamu hairuhusu hilo jambo Kwa wanawake
Kwakuwa haislamu hawana elimu na akili hata kama sheria hairuhusu wao humezeshwa sumu na ma ustadhi uchwara na kwenda kujiunga na vikundi uchwara ati kupigana jihadi.
 
Hata utoe historia ya wapi wewe huo udini wako Kwa maslahi mapana ya Taifa wala hatuna kazi nao, yaani umekuwa mdini kupitiliza.

Au upewe Nchi uongoze ulete huo usawa unaodai waislam wamepunjwa?
Big...
Sijaandika udini naeleza matatizo yanayokabili nchi yetu.
 
Huyu mzee ni wa kupuuzwa amejawa na udini mpaka anakuwa mjinga.

Ninachomkubali mzee Kikwete japokuwa ni muislam ila alipinga sana suala la udini kwa hili nampa pongezi huyu mzee.

Wazee kama Mohamed Said sio salama sana kwa Taifa letu.
Big...
Si rahisi kupuuza kalamu yangu.
Ingekuwa rahisi mimi kupuuzwa ungeanza wewe.

Wala sijaandika udini.

Niko hapa kwa jina langu halisi na kwa sura na sauti.

Wewe unaandika umejificha.

Niambie sababu ya wewe kuficha jina na uso wako.

Unahofia usalama wako?
 
Big...
Si rahisi kupuuza kalamu yangu.
Ingekuwa rahisi mimi kupuuzwa ungeanza wewe.

Wala sijaandika udini.

Niko hapa kwa jina langu halisi na kwa sura na sauti.

Wewe unaandika umejificha.

Niambie sababu ya wewe kuficha jina na uso wako.

Unahofia usalama wako?

Hiyo ni sehemu ya uhuru wangu.

Kama ingekuwa ni lazima basi kila mtu kwenye hili jukwaa ungemfahamu kwa majina yake halisi, picha na kila kitu.

Lakini Mexence hajaweka restrictions kama hizo hivyo hiyo ni sehemu ya privacy yangu na ni haki yangu pia.

Kuweka sura na majina halisi bado sio justification ya kusambaza udini usio na tija yoyote kwa Taifa hili la Tanzania.

Na kwa hivyo basi kupuuzwa pia inawezekana maana udini wala hauna maslahi kwa Taifa hili tena katika zama hizi.

Mwana historia lakini historia zako zinalenga chuki na udini baina ya ukristo na uislamu huku ukijaribu kutetea kundi la uislamu kama kundi linalokandamizwa..

Nimepitia Nyuzi zako nyingi hapa jukwaani tena zingine za muda mrefu sana. Wewe una chuki na Nyerere vile vile ni mdini sana.

Kwa mambo hayo huwezi kuwa hazina kwa Taifa hili labda ubadilike.
 
Huyo Ustaadh alipaswa kua jela hadi sasa.

Kuna mwingine huko Bagamoyo yeye anakusanya watoto wadogo na kuwafundisha ushoga na hajachukuliwa hatua yoyote.

Tanzania hakuna sheria kali za kuwalinda watoto.
Keshakamatwa Yuko ndani
 
Mam...
Mbona unachanganya mambo?
Unajua kuwa serikali ilivunja EAMWS ili kuzuia Waislam wasijenge Chuo Kikuu?
Unajua kuwa serikali ilikataa kutoaa kibali kwa OIC kujenga ChuoKikuu Tanzania?
yaliyopita si ndwele Waislamu mumepewa chuo kikuu Cha Morogoro Bure na serikali kile mororogoro Muslim University hakina maprofesa hata Waislamu maprofesa hawataki kwenda kufundisha pale na pia wanachuo kupata shida wamejaa wanzanzibari kiduchu

Chuo mumepewa Waislamu hawataki kwenda kusoma Hicho wamejazana vyuo secular sababu Kiko duni sana kielimu muda mwingi swala Tano tu
 
Singida hii hali imeshamili sana na wazaz wao wanabariki hiko kitu , nlimpata mdada mmoja mzur kwel ila aliponiambia wapo msituni wanafundishwa madrasa nkaona hapa kuna ttzo tyr
Wanaandaliwa kuwa wake wa magaidi wa Alshabab
 
Keshakamatwa Yuko ndani
Shot....
Polisi wamemchukua Sheikh Yusuf Muhammad kwa mahojiano zaidi hawakumchukua kwa kumweka rumande kwani hapakuwa na jinai yoyote pale.

Sina taarifa zaidi lakini naamini yuko nje.

Inafahamika jambo lolote kuhusu Waislam linaamsha hisia kali.

Mfano ndiyo huu tunashuhudia katika kadhia hii.

Tumeelezwa kuwa kosa la madrsa ni nafasi ndogo kwa wanafunzi na wanateka maji kibwawani.

Vitu hivi haviruhusiwi.

Inatakiwa nyumba yenye nafasi na kuweko na mabomba yanayotiririka maji safi.

Kuna mambo huwa yanafurahisha kusikia.

Inanikumbusha Mkuu wa Mkoa mmoja mwanamama wakati wa kipindupindu anawahutubia wananchi Manzese Uzuri anawaambia kuwa lazima wachemshe maji ya kunywa.

Hawa watu hawana uwezo wa kuchemsha kibirika kidogo cha chai ya rangi watakuwa na uwezo wa kuchemsha sufuria kubwa ya maji ya kunywa?
 
yaliyopita si ndwele Waislamu mumepewa chuo kikuu Cha Morogoro Bure na serikali kile mororogoro Muslim University hakina maprofesa hata Waislamu maprofesa hawataki kwenda kufundisha pale na pia wanachuo kupata shida wamejaa wanzanzibari kiduchu

Chuo mumepewa Waislamu hawataki kwenda kusoma Hicho wamejazana vyuo secular sababu Kiko duni sana kielimu muda mwingi swala Tano tu
Shot...
Mimi nimefika MUM mara kadhaa na nimewakuta maprofesa.
Mimi sijasikia kuwa Waislam hawapendi kufundisha MUM.

Kujaa Wazanzibari MUM limekuwa tatizo?

Ushachunguza kabila gani wamejaa University of Dar es Salaam na kwengineko?

Kuwa MUM ni duni umetumia kigezo kipi kutambua hilo?

Sala Tano: Alfajir saa 11, Dhuhr saa 7 mchana, L' Asr saa 10 jioni, Maghrib saa 12.30 jua linachwea na Isha saa 2 usiku.

Sala hizi kila moja haizidi dakika 10.
Huo muda mwingi ni upi?
 
Hiyo ni sehemu ya uhuru wangu.

Kama ingekuwa ni lazima basi kila mtu kwenye hili jukwaa ungemfahamu kwa majina yake halisi, picha na kila kitu.

Lakini Mexence hajaweka restrictions kama hizo hivyo hiyo ni sehemu ya privacy yangu na ni haki yangu pia.

Kuweka sura na majina halisi bado sio justification ya kusambaza udini usio na tija yoyote kwa Taifa hili la Tanzania.

Na kwa hivyo basi kupuuzwa pia inawezekana maana udini wala hauna maslahi kwa Taifa hili tena katika zama hizi.

Mwana historia lakini historia zako zinalenga chuki na udini baina ya ukristo na uislamu huku ukijaribu kutetea kundi la uislamu kama kundi linalokandamizwa..

Nimepitia Nyuzi zako nyingi hapa jukwaani tena zingine za muda mrefu sana. Wewe una chuki na Nyerere vile vile ni mdini sana.

Kwa mambo hayo huwezi kuwa hazina kwa Taifa hili labda ubadilike.
Big...
Hakika una uhuru wa kujificha.
Kuficha jina lako na sura yako.

Lakini unajificha tu bila sababu?

Uhuru wa kujificha nami ninao lakini sijifichi na sababu ni kuwa nataka viongozi wetu ikiwa watataka ushahidi wa niandikayo wasipate shida kunipata.

Kupuuzwa haijawezekana.

Nimeshiriki miradi minne ya kuandika historia: Mradi wa Oxford University Press Nairobi na Oxford University Press New York, mradi wa kuandika kitabu cha Julius Kambarage Nyerere na mradi wa kuandika upya historia ya Tanzania wa Rais Magufuli.

Niko vilevile katika Cambridge Journal of African History.

Nimezungumza vyuo hivi: University of Dar-es-Salaam, Sokoine University, State University of Zanzibar, Kenyatta University, University of Ibadan, University of Johannesburg, University of Iowa na Northwestern University hizi mbili za mwisho ni Marekani.

Nimezungumza karibu na vyombo vyote vikubwa vya habari: VoA, Radio Iran, BBC, SABC, DW; halikadhalika vyombo vya hapa nyumbani AZAM, RTD, ITV kwa kuvitaja vichache.

Nimezungumza pia katika taasisi za utafiti wa histioria kama Zentrum Moderner Orient, Berlin Ujerumani.

Nisingeweza kufika huko ingekuwa naandika chuki na udini.


1707541369966.jpeg

VoA Washington DC
1707541497717.png

AZAM TV

 
Back
Top Bottom