jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Nchi nyingi zilizofanya mapinduzi na kupiga hatua ziliunganishwa na umasikini, unyanyasaji na ufisadi, what else do we need?@jmushi1
Kwa kweli kama taifa vinavyotuunganisha ni vichache kuliko vinavyotugawa.
Ata point tulikuwa tumefikia kuona kama ni wamoja lakini kwa sasa hivi kuna drift kubwa inaendelea kutokea
hasa ya kikabila, kidini, kimitizamo ya chama.
Hapa kuna ulazima kama taifa kuja na kitu kimoja kitakachotuunganisha chenye mantiki
Naona Nyerere alijaribu kutumia lugha ya kiswahili, utani kati ya makabila, vijiji vya ujamaa
Lakini vitu hivi vyote kwa sasa naona mantiki yake inapungua
Mfano utani kati ya makabila, kwa sasa si kiviile maana kuna generation inayokuja ambayo haijui lolote kuhusu makabila yao na wala huo utani hauwezi kuwa na mantiki katika vichwa vyao.
Matatizo haya yote yanatokana na hayo matatu hapo juu.
Leo nasikia kuna maandamano ya wanaharakati, lets see how much it will unite the country.