Wasichana wa siku hizi..na kutafuta elimu..........

Nimekuelewa ila ningependa pia uelewe nilicho sema: it is easy for you to say that.
Itapendeza sana kama watu watabadilika sababu SIO VIZURI KUTOA RUSHWA YA NGONO.
Ila dunia hii mtu hawezi kuacha njia fupi tena rahisi just because SIO VIZURI.
Kwa hiyo tunaweza kulalamika hapa, na naweza kukuunga mkono but it won't change a thing.
Sio rahisi kwa mtu kukubali kukosa anacho kitakaka just because sio halali (and you know it).
Watakubali kukikosa ikiwa it is illegal and law and order is applied kila wavukapo mipaka.
Watakubali kikukosa ikiwa there is a strong repressive system katika organisation nzima, na mtu akijua atafutwa etc.
Ila hiyo ya kusema tu sio halali kwa hiyo tuache, sioni kama itasaidia chochote.
 
Nimekuelewa King'asti. Point yangu sio kuwatetea wanao toa rushwa ya ngono bali ni kupanua mtazamo ili tuelewe kwamba kosa halianzii kwao. System ilivyo sasa hivi haiwezi kuponyeshwa na maadili pekee. Hatuwezi kusema it is not morally good na watu wakacha. Na hatuwezi kuwaambia wasichana waache na tukategemea kosa litaisha.
Tatizo limekua institutionalized, linahitaji institutionalized solution.
 

unapolushia ili kosa kwa jamii,ndio na mimi sikubaliani nawewe...sababu kuna wanawake(napenda kuwaita wa shoka) huwa sio rahisi kuingia kwenye mkumbo huu,hawa wanajiamini na kujithamini ivyo kwa jitihada zao wanapambana wenyewe hadi wanapenya na kufikia sehemu nzuri na hawatoki mbinguni wamezaliwa na kukulia kwenye jamii hii unayoikosoa..wanawake wa namna hii huwa wanaheshimika sana na jamii.
 

Mwali uko very wrong...
hebu jiulize Japan na South Korea wako vipi?
kila kitu ni sheria?
hapana.....kuna culture na jamii inavyokubali maambo...

Japan hata music concerts watu wanapanga mstari bila police wala nguvu kuubwa kuwaweka watu kwenye mstari
ni culture aisee
hivi uliona wajapan kwenye Tsunami walivyo behave after Tsunami?
unakumbuka Katrina?
unaweza linganisha?
jiulize why society moja watu wanapatwa na balaa hakuna kuvamia maduka wala kuibiana
wala kulalamika kwa saana...
while wengine ni aibu tupu....jiulize....ni zaidi ya sheria aisee...
Japan mtu akikujulikana mla rushwa anajinyonga kwa aibu..
Africa ndo anaenda kugombea ubunge...go figure...
 
I am not VERY WRONG Boss.
Ukinisoma nimesema maadili yamo, sibishi hapo. Ila maadili peke yake hayatoshi!
Kwani hatuna maadili? Hao wasichana hawajui kua kufanya hivo ni makosa?
Sema maadili yetu yayatoshi kwa kukabiliana na tatizo, kutokana na magnetude ya hali halisi.
Kuna culture zingine zinaonesha kupitia njia ya panya ni ujanja fulani. Mfano mtu akikopa hela benki alafu baada ya miaka 3 aweze kukataa kulipa benki bila kufungwa (kwa njia za kifisadi) ataonekana bonge la mjanja.
Sasa uta enforce hiyo culture?
Kwa vile tumeshindwa kuenforce order and good behavior kupitia maadili, basi tujaribu kutumia rungu la sheria.
 
Wapo, sibishi. Na tunawajua, tunawaheshimu.
Ila ni wangapi kwa mia? Na unadhani wanawake wote ni washoka? Personalities zinapishana.
The Boss kasema ujinga huu (wa rushwa ya ngono) ni threat kwa society nzima.
Kwa hiyo mwanamke akiamua kua mwepesi kuitumia tunatakiwa sisi kama society kutafuta njia za kumziwia kutumia njia hizo,
na sio kumuachia maamuzi ya kua mwanamke wa shoka au mwanamke mwepesi kutumia rushwa ya ngono.
Lazima tuunde system ambapo KILA MWANAMKE, wa shoka au wa jembe, ashindwe kutoa rushwa ya ngono.
 

Vipi kwa wanaume? Nao sio wezi wa elimu? Naona kama ume-narrow sana huu uzi kwa kwa wasichana kujiuza ili kupata elimu. Lakini ufisadi wa elimu ni mpana sana na hau-relate na ngono tuu. Kuanzia viongozi kuwa na degree feki, wizi wa mitihani, kupeana scholarships na nafasi za kusoma kwa kujuana/kutoa rushwa, vyeti vya kufoji, kudesa, mpaka watoto wadogo kunyimwa haki yao ya msingi ya elimu. Masai School *Tanzania,Africa. | Flickr - Photo Sharing!
 

Faida ipo tena kubwa kama unavyoona kwa dada yetu Vicky Katama aliyeolewa na CCM, unadhani angeimba habari ya shombo!!!
 
The Boss, Mwali et al,

Naona mnaongelea jambo lile lile ingawa mnajiona kama mnatofautiana....

Wasichana wanaotoa ngono kupata elimu ni variable moja tu ya equation...Zipo nyingine nyingi sana!!

Babu DC
 
Ukiona mwanamke anatumia njia mbovu ujue tatizo liko kwenye malezi yake.Si ajabu wazazi wake ni watu wanaopenda shortcuts.
Akishakua mtu mzima, utamwekea utaratibu gani ashindwe? Kwani TAKUKURU si wanakataza rushwa ya ngono? Na je wanaopokea/kuomba rushwa ya ngono ni watu wa namna gani?
 
Faida ipo tena kubwa kama unavyoona kwa dada yetu Vicky Katama aliyeolewa na CCM, unadhani angeimba habari ya shombo!!!

Ile ndoa kwani imeanzia wapi? Darasani au ofisini?
 

Actually nilikuwa nataka nizungumze kwa jamii nzima as whole
but nimejikuta najibu post za watu zaidi....
labda nikuulize EMT kuna viwango vya makosa?vya dhambi?
kujiuza na kununua mithani unaweza sema ipi ni dhambi zaidi?
 
Ile ndoa kwani imeanzia wapi? Darasani au ofisini?
Imeanzia kwa padre huko SAUT, kabla ya kuonwa na wazee na kupewa elimu zaidi na ajira BOT baada ya wanawake na maendeleo!
 
hata walimu wanaangalia msimamo
akimjaribu mwanafunzi anaangalia reaction yake

kuna mmoja aliwahi pewa supp
akagoma kumpa mwalimu mzigo
aka-carry kozi
lakini mwishoni alimwachia
maana hapo alikuwa mwaka wa mwisho

mwalimu huyo huyo
katikati ya mtihani akamtongoza binti
na kumtongoza binti katiktai ya mtihani ni sawa na kumwambia
Be warned
usipokubali una sapp
lakini aliweza kusort out bila kumpa ngono na akafaulu

mi naamini huwa kuna alternatives katika maisha

na kweli kupanga ni kuchagua

 

Mkuu naona kama umeliangalia tatizo kwa upande mmoja tuu. Kwamba tatizo hapa ni tamaa za wasichana kujilengesha kwa walimu. Kwa maana hiyo, wakishajilengesha ruksa walimu kufanya nao mapenzi? Kwani walimu nao hawana ethical obligations za kutofanya mapenzi na wanafunzi wao to the extent ya hata kuwapa mitihani? Nakumbuka hili suala tumeshalijadili kwenye thread moja ya Lizzy.

Inawezekana wala tatizo sio kwa hao wasichana. Ukweli ni kwamba tofauti na zamani, siku hizi hatuna walimu tena. Walimu wengi wa siku hizi hawajui hata majukumu yao. Hawajui ethics za ualimu. Wengine wameishia kuwa walimu baada ya alternatives nyingine kushindikana kutokana na poor qualifications. Tungekuwa na walimu wenye vichwa na wanaoelewa majukumu yao ya ualimu kama zamani mbona ungekuta nao wako kwenye mgomo kama madaktari?

Sorry kama kuna mwalimu wa kizazi kipya hapa.
 
Imeanzia kwa padre huko SAUT, kabla ya kuonwa na wazee na kupewa elimu zaidi na ajira BOT baada ya wanawake na maendeleo!

Aiseee. . . huko ndiko kunaitwa kujitoa na kujitolea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…