Wasichana watatu kati ya 10 wanaathirika na ndoa za utotoni Tanzania

Wasichana watatu kati ya 10 wanaathirika na ndoa za utotoni Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mkurugenzi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Milisic amesema uchunguzi waliofanya umeonesha wasichana watatu kati ya 10 wenye chini ya miaka 18, wapo kwenye ndoa za utotoni.

Zlatan amesema wanaoathirika zaidi ni wasichana wanaoishi vijijini huku akitaja madhara wanayokumbana nayo kiafya kuwa ni pamoja na Kuathirika Kiuchumi, Kijamii, Kisaikolojia na Kuondolewa Utu wao.

Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii pamoja na Kamati ya Sheria na Katiba kupitia Mkutano wa Bunge unaoendelea Dodoma, zinatarajiwa kujadili kwa pamoja ili kufanya marekebisho ya Sheria ya Ndoa.

Kwa mujibu wa takwimu za UNICEF, inakadiriwa kuwa, wasichana watatu kati ya 10 nchini wanaolewa wakiwa bado watoto, na kuifanya Tanzania kushika nafasi ya 11 kwa ndoa za utotoni duniani.

Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inaweka miaka 18 kuwa umri mdogo ambao wavulana wanaruhusiwa kuoa, lakini imeweka umri wa miaka 15 kwa wasichana kuolewa kwa ridhaa ya wazazi, sheria hiyo wadau wametaka serikali ifanyie marekebisho, kwani inapingana na wakati na haipo wazi, ikishindwa kufafanua mtoto ni nani.
 
  • Kama taifa, tuache kuwa biased kama tunataka ukombozi wa kweli, huko kijijini mtoto anamwoa mtoto.
  • Ndoa za utotoni zinapaswa kukemewa kwa namna mbili: kuoa na kuolewa.
  • Tuwaambiwe viongozi ukweli na waufanyie kazi ili uponyaji wa jamii upatikane: haiwezekani mvulana under 18 aoe (bila kujalisha aliyeolewa ni wa umri gani), kisha tutarajie tutakuwa na familia, jamii imara.
 
Back
Top Bottom