Wasichokijua Wengi Kuhusu Marko 10: 25 katika Biblia

Wasichokijua Wengi Kuhusu Marko 10: 25 katika Biblia

Jana wakati naangalia ile muvi ya Yesu, nimekuja kuona Yesu anaisema iyo kauli wakati wakiwa wanapishana na ngamia mnyama. [emoji16][emoji16]

Balaa hili
 
Hakuna hao watu duniani hapa, (Uwezi kutumikia mabwana wawili). Matajiri hawawezi kuiteka Mbingu, b'coz , fedha zao ukamilisha tamaa zao zote ziwajiazo. Na kila wakifanyacho duniani, kina mapungufu mengi ya Ki-Mungu, bali kimejaa heshima na tabia za Kidunia. Matajiri wanaonekana kama wacha Mungu na wafadhiri wa watu wa Mungu, lakini ukiwa na hekima ya Mungu, utajua wanaikana nguvu ya Mungu na wanakufanya wewe unaowaona au unaesaidiwa na wao kuwa mtumwa wa hao matajiri kifikra na kimaisha( Wanaiba sifa ya Mungu kuwa tegemeo na kuichukua wao Matajiri bila kukuwambia)
Uyasemayo sidhani kama yanaakisi huwalisia...

Wengi watu wa imani tunautafsiri utajiri ktk Hali hasi...lakini tunasahau kuwa tunaviongozi wengi wa dini tena wanatuongoza ktk nyumba za ibada wanautajiri wa kupindukia.

Embu fikiria Hali ya kiuchumi ya wachungaji wengi barani Africa...afu angalia Hali ya wafuasi wao ( waumini).

Njoo tuwaangalie mapadre Hali zao za kiuchumi...afu tuangalie waumini wao.

Kwa kifupi tukiangalia wachungaji na mapadre wengi ni matajiri...

Swali la kujiuliza,je utajiri wao wa Hali??

Nahitimisha kwa kusema...utajiri si dhambi,wala sio kwamba matajiri hawataiona mbingu...wapo watakaoiona mbingu Ila ni wachache.

Kuichukua dunia haimaanishi kujitenga na utafutaji wa pesa,haimaanishi kutokujipenda kula vzur,kuvaa na kuendesha magari mazuri.

Kuichukia dunia ni kujiepusha na matamanio ambayo yanamchukiza Mungu...na kujisahaulisha kwa starehe fupi za kidunia na kusahau majukumu ya kimungu.
 
Uwe Padri, Askofu, Mchungaji, Unatoa pepo, Maadam wewe ni tajiri, unaangukia kwenye kanuni ile ile ya huwezi kumtumikia Mungu na Mali, either uambatane na Mungu au Uambatane na Mali zako. Mungu ni mwaminifu, maneno yetu mengi ya kupambana labda alimaanishe vingine haimsumbui. Kumbuka tajiri kuingia kwenye Ufalme wa Mungu anatakiwa achukue kanuni ya Yesu Kristo ya "Kujitoa Sadaka Yeye Mwenyewe". Yaani amtumikie Mungu yeye sio mali zake. Hakuna mtu mwenye hela nyingi ata kama ni Askofu anaejitoa sadaka kwa Mungu, wengi wanampa Mungu Sadaka ya pesa zao na mali zao na kujiokoa kutoka kwa Mungu. Matajiri siku zote huziokoa na kuziponya nafsi zao zisizurike kwa maana, wana vyeo na Mali, wanazipenda na wana fedha za kuzirinda, masikini yeye huiangamiza nafsi yake maana haoni samani ya dunia (Yesu alisema haiponyae nafsi yake ataingamiza na haingamizae nafsi yake ataiponya), Put Masikini yeye hujimaliza kwa sababu hana fedha wala dhahabu kwahiyo humpa Mungu vyote roho na mwili. KWA BINADAMU HAIWEZEKANI LAKINI KWA MUNGU YOTE YAWEZEKANA. Tuombeane.
 
Mkuu umaskini sio ndo kipimo cha uchamungu....kama ulikuwa hujui umaskini ni nusu ya ukafiri (kukufuru).

Bado hujajua kusudio sahihi wa ule msemo,na huenda ule msemo umekuja sahihishwa na aya hii ktk Qur'an.
2648857_Screenshot_20201226-110422.png

Na si kwamba enzi za mitume hapakuwa na matajiri wakiwaamini mitume...laaa.

Walikuwepo matajiri wengi wakiwaamini mitume na walikuwepo maskini wakiwaamini mitume pia na kinyume chake.

Ondoa dhana hii kichwani kwako...utajiri sio dhambi,utajiri sio chanzo cha maovu...kuwa tajiri haimaanishi hauna sifa ya kuwa mfuasi wa Mungu (mcha Mungu).

Embu ilewe kwanza aya hiyo apo juu ndo utanielewa namaanisha nini.
 
Mkuu umaskini sio ndo kipimo cha uchamungu....kama ulikuwa hujui umaskini ni nusu ya ukafiri (kukufuru).

Bado hujajua kusudio sahihi wa ule msemo,na huenda ule msemo umekuja sahihishwa na aya hii ktk Qur'an.View attachment 1659445

Na si kwamba enzi za mitume hapakuwa na matajiri wakiwaamini mitume...laaa.

Walikuwepo matajiri wengi wakiwaamini mitume na walikuwepo maskini wakiwaamini mitume pia na kinyume chake.

Ondoa dhana hii kichwani kwako...utajiri sio dhambi,utajiri sio chanzo cha maovu...kuwa tajiri haimaanishi hauna sifa ya kuwa mfuasi wa Mungu (mcha Mungu).

Embu ilewe kwanza aya hiyo apo juu ndo utanielewa namaanisha nini.
Sawa, unavyoamini wewe. Naeshimu mawazo yako pia.
 
Katika kitabu kitakatifu cha Biblia, Marko 10: 25 inasema: Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

Wanachokielewa wengi, wakiwemo baadhi ya watumishi wa Mungu, ni kwamba ngamia anayezungumziwa hapa ni yule mnyama mwenye nundu kubwa mgongoni, pengine hata wewe kwa miaka mingi umekuwa ukijua hivyo.

Hata hivyo, ngamia iliyomaanishwa hapa, ni kamba! Ndiyo, kamba! Zile kamba nene zinazotumika kuvuta kwa mfano meli iliyozama na kadhalika. Makosa ya tafsiri hii yanaanzia kwenye kufasiri kifungu hiki cha Biblia kutoka kwenye Kiingereza kuja kwenye Kiswahili. Kwa Kiingereza, Mark 10:25 inasomeka hivi: It is easier for a camel to go through the eye of a needle than for a rich person to enter the kingdom of God.

Ukichukua kamusi yako, angalia maana ya neno camel, ya kwanza utaona ni ngamia mnyama lakini kuna maana ya pili ambayo ni hii: Camel: An apparatus for raising a sunken ship, consisting of one or more watertight chests to provide buoyancy. Kwa tafsiri nyepesi, ni kamba nene zinazotumika kuvuta meli iliyozama...

Kwa commoni sense ya kawaida tu, ngamia mnyama anawezaje kufananishwa na kupenya kwenye tundu la sindano? Hakuna uhusiano wowote, lakini kuna uhusiano wa kamba nene kupenya kwenye tundu la sindano kwa sababu kamba nyembamba (uzi) unapenya kirahisi!

Kwa hiyo tunahitimisha kwa kusema, ngamia/camel inayomaanishwa kwenye bible ni kamba. I stand to be corrected!
Hapana mtoa.mada hujaelewa vizuri lugha ya asiliw we
View attachment 1651630
Hapana. Haina maana hiyo. Kule palestina enzi hizo za taifa la Israel kulikuwa na eneo la mlimani ambapo illikuwa ni njia kuelekea malishomomlakoni Ni wanyama wadogo tu hasa kondoo waliweza kupenya katikati ya miamba hiyo iloyokuwa imegusana. Kwenye njia hiyo, ngamia walishindwa kupenya kwa hiyo oakaitwa "tundu la sindano" kwa sababu ya udogo wake. Yesu alipotoa mfano huu was tajiri, alikuwa akimaanisha mahali ambapo ngamia wanashindwa kupenya na sio sindano ya kawaida.
 
Summarization

Hoja ni tatu

1. Ngamia mnyama kupita kwenye tundu la sindano(sindano hapa inamaanisha kifaa). Hii ni hoja kongwe na iliyozoeleka mno. Kifupi hapa tunaona haiwezekan kabisa ngamia kupita kwenye hilo tundu.

2. Ngamia kama kamba kupita kwenye tundu la sindano kifaa. Hii ni tafsiri ambayo siyo maarufu sana. Hapa ngamia inamaanisha kamba ambayo ni nene na hutumika kuvitia meli iliyozama au kutia nanga. Pia hapa kimantiki ni ngumu kamba hiyo kupita kwenye matundu ya sindano nyingi tunazozifahamu.

3. Ngamia kama mnyama kupita kwenye mlango wa kuingia mji Jerusalem ambao kwao ulijulikana kama tundu la sindano. Kihistoria inaonyesha ni lango ambalo lilikuwa ni dogo kwa umbile lake hivyo ili kupitisha ngamia ilibidi alazimishwe sana kwa kuwa alikuwa hapiti amesimama na watu ndiyo walitumia nguvu kubwa zaidi kumpitisha. Hapa huenda yesu alitaka kututizamisha kuwa ni kwa unyekekevu wa hali ya juu kwa Mungu ndiyo kitu pekee kinachoweza kumuingiza tajiri mbinguni.

Majumuisho:
Hoja ya tatu hapo inaonyesha kuwa kuna uwezekano wa tajiri kuingia mbinguni tofauti na hoja mbili za awali.

Maoni yangu ya awali kabla sijatafuta maandiko zaidi kuhusu hili yananiaminisha hoja ya tatu ni sahihi kwa sababu
kwanza inaonesha kuna uwezekano wa tajiri kuingia mbinguni tofauti na mbili za awali.

Pili, pamoja na kuwa hoja kuwa ngamia kama kamba inajishikiza kwenye ukweli wenye nguvu kwamba alikuwa anaongea na wavuvi ambao bila shaka walielewa vema maudhui ya kamba hiyo. Ikumbukwe ni kanuni ya mawasiliano kuwa mada lazima izingatie muktadha husika lakini ni hakika bila shaka kama alikuwa anaongea na wakazi wa mji wa yerusalemu basi walijua uwepo wa mlango ulioitwa tundu la sindano. Hivyo Yesu alijua fika wataelewa kwa kuwa wanaujua mji wao.

Kosa lenyewe la tafsiri. Kama ulishawahi kufanya kazi au kusomea maarifa kuhusu taaluma ya tafsiri basi pasi na shaka unaweza kuona kuwa huenda mfasiri alitumia tafsiri sisisi zaidi kulifasiri neno ambalo linaibua kiini cha mjadala yaani hakuzingatia matumizi mapana ya neno hilo kutoka katika jamii ya matini chanzi.

Mjadala uendelee

Hakika unastahili heshima ya kipekee kuweza kudadavua hiyo hoja ya ama NGAMIA au KAMBA kwenye mfano alioutoa Yesu.

Mchambuzi mwingine anafafanua ifuatavyo:

Je! Katika Marko 10:25 Bwana Yesu alimaanisha ngamia mnyama au kamba katika Injili Takatifu ya Marko:10:25 alipowaambia mitume wake kuwa, ni rahisi ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu..

Mwanzilishi wa mjadala amehitimisha tafsiri yake ya aya hiyo kwa kuandika ngamia/camel inayomaanishwa kwenye bible ni kamba.

Baada ya kupitia Biblia Takatifu na baadhi ya nyaraka zenye kutoa ufafanuzi wa aya zenye utata fulani katika Biblia; naomba kutoa mchango wangu zaidi katika mjadala huu kama ifuatavyo:

1. Mafundisho ya Bwana Yesu katika Marko 10:25 yanalingana na Luka 18: 25 na Mathayo 19:24. Katika aya hizi zote, hakubainishwi kama Bwana Yesu alikuwa anaongelea ngamia mnyama au ngamia kamba.

2.THE AFRICAN BIBLE katika ukurasa wa 1766 imelifafanua neno CAMEL kwenye safu ya ufafanuzi ( footnote) kama ifuatavyo: ( tafsiri yangu ya kawaida) " A camel: ngamia kupita kwenye tundu la sindano ni usemi wa mfano kuelezea kile kisichowezekana kibinadamu. Ni Mungu pekee anayeweza kuleta wokovu. Lakini kuacha vyote kwa ajili ya kuingia katika ufalme wa Mungu kuna maana ya kupata zawadi iliyo kuu, sasa na baadaye. Huyo NGAMIA (kwa Kiebrania "GAMAL"), anayeelezwa mara nyingi katika Biblia hutumika kubeba mizigo mizito na kwa usafiri wa watu; na mara nyingi anahusishwa na makabila ya watu wanaohama hama, wa Afrika ya Kaskazini. Huu ni ufafanuzi uliotolewa wa Injili ya Luka 18:25.

Ufafanuzi wa Mathayo 19:24 ni kama ifuatavyo: " Camel": ( Linganisha Marko 10:25; Luka 18:25; Mathayo 23:24). Ngamia ambaye Mafarisayo hummeza wakati wakimchuja mbu(?) . Baadhi ya wadadisi wa maandiko wanatilia shaka kuwa huenda maandiko ya awali yalisomeka kama "KAMILOS" katika lugha ya Kigiriki yakimaanisha KAMBA ( au waya, CABLE). Hata hivyo, sura ya ngamia ( mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano, haielezei ugumu, bali kutowezekana". Hapa pameonyeshwa picha ya mnyama ngamia.

Ufafanuzi wa Marko10:25 kwenye footnote: " Camel: "ni kama ifuatavyo: " Jambo muhimu ambalo Bwana Yesu anataka kusema hapa ni kwamba wokovu ni zawadi kutoka kwa Mungu; nayo haipatikani kwa juhudi za kibinadamu pekee".

2. GRUDEN'S COMPLETE CONCORDANCE TO THE OLD AND NEW TESTAMENT katika kufafanua neno "CAMEL", imeonyesha ifuatavyo katika ukurasa wa 74: "CAMEL": ( Ngamia ndio walikuwa wanyama waliotumika kwa usafiri wa binadamu katika nchi za mashariki kwa kuwa ni wanyama wenye nguvu kuliko farasi na wenye kustahimili zaidi magumu. KWA KUWA SEHEMU KUBWA YA ULIMWENGU WA KI-BIBLIA ILIKUWA AMA JANGWA AU NCHI KAVU/ KAME KATIKA VIPINDI FULANI VYA MWAKA, uwezo wa kipekee wa mnyama ngamia wa kuhimili mazingira magumu ya jangwani, ulikuwa ni wa kipekee. Mara nyingi utajiri wa mtu ulipimwa kwa kigezo cha wanyama ngamia. Ngamia walifugwa kwa ajili ya kufanyishwa kazi au kwa ajili ya usafiri wa haraka; na singa zake zilitumika kutengenezea mavazi ( HAPA ZIKANUKULIWA AYA ZA BIBLIA IKIWAMO HIYO INAYOSEMA :
" Ni rahisi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mbinguni, zikaorodheshwa aya Marko 10:25; Mathayo 19: 24; Luka 18:25 na Mathayo 23:24).

3. THE BIBLE READER'S
ENCYCLOPAEDIA AND CONCORDANCE: Imefafanua jina "CAMEL" kama ifuatavyo: "Camel ( Hebrew: " GAMAL". "Kati ya kumbukumbu za kale kabisa za watu wa mashariki, ngamia alichukuliwa kuwa miongoni mwa vianzo muhimu vya utajiri. Ngamia walipotajwa kwa mara ya kwanza kupatikana huko Misri, Arabuni au Kanaani, wanyama hao walipatikana kwa idadi kubwa na walilinganishwa na kondoo, ng'ombe na punda. Ngamia mwenye nundu moja ndiye ngamia anayeongelewa hapa. Haikuruhusiwa kula nyama ya ngamia, ijapokuwa maziwa yake yalikuwa yakitumika kama chakula kwa kiasi kikubwa. Ngamia walifugwa katika idadi kubwa mno". ...hapa pakaorodheshwa aya za Biblia ikiwemo Mathayo19:24 inayohusu somo tunalolijadili hapa.

Kwa upande mwingine, neno kamba, au kwa Kiingereza "CABLE" au "CORD", hakuna mahali katika Biblia Takatifu ambapo limeonyeshwa kuhusishwa na mafundisho ya Bwana Yesu katika Marko 10:25; Luka 18:25; Mathayo 19:24 au Mathayo 23:24 tofauti na maelezo ya mwanzilishi wa mjadala huu. Hata pale tulipoonyeshwa neno la Kigiriki "KAMILOS" katika ufafanuzi wa The African Bible kama ilivyonukuliwa hapo juu, pameoneshwa mashaka katika usahihi wa tafsiri hiyo. Na kwa kuwa enzi hizo Biblia ilipoandikwa, lugha ya Kiswahili ilikuwa bado haijazaliwa, kwa maoni yangu, ni makosa kusema kuwa Bwana Yesu alikuwa anafundisha juu ya ugumu wa kamba kupenya katika tundu la sindano.

Kinyume chake, na kama tulivyoona katika maandiko yenye kuaminika hapo juu; ni wazi kuwa Bwana Yesu alipokuwa anawafundisha mitume wake kwa kutoa mfano wa urahisi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu kama alivyonukuliwa katika Marko 10:25; Luka 18:25 na Mathayo 19:24, alimaanisha mnyama ngamia na wala siyo "camel" kwa tafsiri ya kamba katika lugha ya Kiswahili.

Kwa hitimisho langu hilo naungana nawe kuwa tundu la sindano lilikuwa ni lango dogo la kuingia mji wa Yerusalem. Yesu hakumaanisha "sindano ya kushonea" kwa kuwa kwa wakati ule na hata wa sasa "sindano" zina ukubwa wa aina tofauti kulingana na ukubwa wa uzi. Na hata hiyo kamba inayotumika kwenye majahazi pia hupitishwa kwenye matundu yenye ukubwa unaostahili.
 
Katika kitabu kitakatifu cha Biblia, Marko 10: 25 inasema: Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

Wanachokielewa wengi, wakiwemo baadhi ya watumishi wa Mungu, ni kwamba ngamia anayezungumziwa hapa ni yule mnyama mwenye nundu kubwa mgongoni, pengine hata wewe kwa miaka mingi umekuwa ukijua hivyo.

Hata hivyo, ngamia iliyomaanishwa hapa, ni kamba! Ndiyo, kamba! Zile kamba nene zinazotumika kuvuta kwa mfano meli iliyozama na kadhalika. Makosa ya tafsiri hii yanaanzia kwenye kufasiri kifungu hiki cha Biblia kutoka kwenye Kiingereza kuja kwenye Kiswahili. Kwa Kiingereza, Mark 10:25 inasomeka hivi: It is easier for a camel to go through the eye of a needle than for a rich person to enter the kingdom of God.

Ukichukua kamusi yako, angalia maana ya neno camel, ya kwanza utaona ni ngamia mnyama lakini kuna maana ya pili ambayo ni hii: Camel: An apparatus for raising a sunken ship, consisting of one or more watertight chests to provide buoyancy. Kwa tafsiri nyepesi, ni kamba nene zinazotumika kuvuta meli iliyozama...

Kwa commoni sense ya kawaida tu, ngamia mnyama anawezaje kufananishwa na kupenya kwenye tundu la sindano? Hakuna uhusiano wowote, lakini kuna uhusiano wa kamba nene kupenya kwenye tundu la sindano kwa sababu kamba nyembamba (uzi) unapenya kirahisi!

Kwa hiyo tunahitimisha kwa kusema, ngamia/camel inayomaanishwa kwenye bible ni kamba. I stand to be corrected!

View attachment 1651630
Kuna mtu aliwahi kusema hivi: ngamia iiliyoongelewa hapa na Yesu, ni milango ya majumba makubwa ya zamani yale yaliyokuwa yanayojengwa kwa architecture ya duara kama uwanja wa mpira, halafu mule ndani kunakuwa na uwazi mkubwa, na majumba hayo yanakuwa na nyumba nyingi zimekaa kwenye mduara. Majumba hayo yalikuwa yanakuwa na milango michache mikubwa (kama gates) na pia milango mingine midogo midogo yenye sura kama tundu la sindano, ambayo ngamia mnyama, alikuwa hawezi kupita kwenye milango hii isipokuwa binadamu peke yake. Ngamia wenyewe walikuwa na uwezo wa kupita kwa kutumia yale mageti yale makubwa tu. Milango hii iliyofanana na matundu ya sindano, ilikuwa inaitwa tundu la sindano. Ukweli ni kuwa tafsri uliyoitoa wewe hapa ndiyo ina uwezekano mkubwa wa kuwa sahihi
 
Back
Top Bottom