Wasifu/Biography wa Ali Masoud (Masoud Kipanya)

Wasifu/Biography wa Ali Masoud (Masoud Kipanya)

Huyu jamaa nimekuwa nikimfuatilia muda mrefu ...........Aisee huyu jamaa ni kichwa sana......Yani unaweza ukachukua threads kibao za JF na comments za watu, lakini yeye akaweza kuyapresent kwa mchoro mmoja tu.......

Matatizo mengi sana ya kijamii amekuwa akiyawakiisha katika michoro yake......Na kuna muda inahitaji akili ya ziada kuweza kuelewa michoro yake..............Michoro yake mingi imejaa Sarcasm na inakosoa kila penye kosa bila kujali ni upande wa serikali wala upinzani.............

Kuna muda anaweza akatoa mchoro wake ukauchukulia poa mpaka baada ya muda ndo unaelewa alichokimaanisha.....Mfano ile ishu ya Sefue kutumbuliwa.....

Nikawaza kuwa huyu jamaa anapaswa kupewa degree ya heshima na vyuo vyetu hapa Tz.....

Hebu mwenye kumjua vizuri historia yake kielimu aitupie hapa ili tumfahamu kwa undani.....Jamaa ni kichwa sana...


Interview Kipanya na Bongo Celebrity.com July, 2007



KWA KINA NA MASOUD KIPANYA(KP)


Ukiiona katuni yake gazetini, huhitaji kutambulishwa au kusaka sana jina la mchoraji hata pale anapokuwa hajaweka sahihi yake. Taswira yenyewe ya katuni itakueleza. Ni katuni ambayo imekuwa sehemu ya maisha ya watanzania kwa miaka mingi sasa. Wengi wetu tunamfahamu kama Masoud Kipanya. Lakini je hilo ni jina lake halisi? Alianza lini shughuli za uchoraji?

BongoCelebrity leo ina furaha kuwaleteeni mahojiano ya kina na Masoud Kipanya, maarufu pia kama KP, mchora katuni maarufu, mtangazaji wa CLOUDS FM na pia mbunifu mahiri wa mitindo (fashion designer). Katika mahojiano haya, pamoja na kuweka bayana maswali mawili yaliyoulizwa hapo juu, KP anaongelea zaidi maisha yake kama mchora katuni zikiwemo kasheshe alizowahi kukumbana nazo, mtizamo wake kuhusu jamii au nchi zinazoendelea kama yetu ya Tanzania, anatoa ushauri kwa wanaotaka kuwa wachoraji kama yeye na zaidi ya yote anao ujumbe maalumu kwa Watanzania kuhusu viwalo vya KP vitakavyokuwa sokoni hivi karibuni.Yafuatayo ni mahojiano yenyewe;

BC: Awali ya yote, hebu tueleze Kipanya ni jina lako halisi au ni jina la katuni wako? Na kama ni jina lako halisi kwanini uliamua kulitumia kwa ajili ya katuni wako maarufu kama KIPANYA?

KP: Jina langu halisi ni Ali Masoud, jina la Kipanya ni matokeo ya katuni ya Kipanya niliyoibuni karibu miaka 13 iliyopita.

BC: Kwa ufupi unaweza kutuambia ulianza lini na kivipi kuchora katuni au vikaragosi kama ambavyo wengine wanaziita?

KP: Mapenzi ya kuchora yalianza nilipokuwa darasa la pili, na nilianza kwa kuiga tu katuni za ndani na za nje kama ilivyo kawaida kwa yoyote anayeanza kufanya kitu, ila professionally nilianza rasmi mwaka 1988, huo ndio mwaka ambao katuni yangu ya kwanza ilitoka katika gazeti la Heko.

BC: Je unatoka katika familia ya wasanii au wachoraji? Unao ndugu zako ambao nao ni wachoraji?

KP: Hapana, bahati mbaya katika familia yetu hakukuwa na mchoraji kabla yangu, isipokuwa baada ya mimi kuna mdogo wangu ambaye tayari ameshaanza kuja juu katika fani ya katuni, ila baba na mama yangu ni watu ambao ingawa si wachoraji, lakini mfumo wa maisha yao inatosha kabisa kusema nao pia ni wasanii.

BC: Hivi sasa wewe unastahili kabisa kuitwa “professional cartoonist”. Unadhani lini hasa ulifikia kiwango hicho?


KP: Nadhani pale nilipoanza kuaminika na katuni zangu kuingia magazetini, naweza kusema mwanzoni mwa miaka ya tisini.

BC:Nini raha hasa ya kuwa mchora katuni?

KP:Raha ya kuwa mchora katuni, ama kuwa mchoraji kwa ujumla ni kwamba unaweza kufanya kile ambacho mpiga mpicha hawezi kufanya, yani unaweza kufanya mbingu ikawa ardhi na ardhi ikawa mbingu, unaweza kumfanya Bush ama Kikwete waonekane wana miguu kama spoku za baiskeli nk.

BC:Ni vikwazo gani unavyokumbana navyo kama mchora katuni? Na je huwa unavivuka namna gani?

KP:Kikwazo kikubwa kwangu ni censorship. Kwa wasioelewa, censorship ni ile hali ambayo unachora katuni halafu kabla haijachapishwa inapitiwa na kama itaonekana ina madhara kwa mtu ama jamii Fulani, basi itarekebishwa ama isichapishwe kabisa. Hayo yamenitokea mara nyingi tu katika maisha yangu nikiwa katika magazeti mbalimbali. Mara nyingi censorship hutokea pale inapoonekana unachora katuni zinazosumbua mioyo ya walengwa hususan wanasiasa wasiopenda kukosolewa.

BC: Katika maisha yako kama mchora katuni ni lazima umeshakumbana na mengi. Je kuna tukio lolote ambalo hutokaa ulisahau kamwe? Ilikuwaje?

KP: Matukio yako mengi, kwa uchache tu, nakumbuka siku niliyomchora mtu mnene akiwa amemshika kamba iliyomfunga mbwa ambaye ameandikwa ‘polisi’, maana ya katuni hii ukiangalia kwa haraka haraka ni kwamba jeshi la polisi haliko kwa manufaa ya umma bali kwa manufaa ya watu wachache hasa viongozi wa chama tawala.Hiki kilikuwa ni kile kipindi ambacho wapinzani walikuwa wakibughudhiwa na polisi kila walipotaka kufanya mikutano yao ya hadhara. La pili ni wakati ule mbunge mmoja aliyejulikana kwa jina la Tuntemeke Sanga alipokuwa anaumwa, nilichora katuni inayomuonyesha mheshimiwa Sanga akiwa amelazwa huku akiwa ametundikiwa damu, halafu pembeni yuko serikali akiwa amegeukia upande mwingine huku akivuta sigara kana kwamba hajali, bahati mbaya siku iliyofuata Mzee Sanga akafariki, naikumbuka siku hiyo vizuri, aliyekuwa katibu wa bunge wa wakati huo, Mzee Mlawa, alivamia ofisi za gazeti la majira, bahati nzuri, wakati anaingia mimi nikawa natoka, na pengine kutokana na umbo langu, hakuweza kudhani kwamba pengine huyu ndio masoud kipanya. Kilichoendelea kati yake na mhariri wangu kwa kweli sikukifahamu.

BC: Unaye mchora katuni yeyote ambaye alichangia uamuzi wako wa kuwa mchora katuni?


KP:
Kwa kweli kama msanii, naweza kusema wasanii wengi niliokuwa nikitazama kazi zao wakati ule walini-inspire niweze kupiga hatua.


BC: Maendeleo ya tekinolojia duniani yanabadilisha kila kitu kadri siku zinavyokwenda. Tofauti na hapo zamani ambapo wachoraji mlitumia zaidi kalamu na karatasi siku hizi mnatumia kompyuta nk.Wewe unatumia vifaa gani katika kufanikisha kazi zako?


KP:
Pamoja na kukua kwa teknolojia, bado kuchora kwa kutumia mkono, kalamu na karatasi ndio mtindo unaoendelea kutumika, kompyuta inatumika tu katika kuboresha kazi ya msanii.

BC: Mara nyingi wachora katuni wanakuwa na hadhira (audience) ya aina mbili, wanaochukia na wanaocheka wanapoiona na kuisoma katuni. Unaupenda zaidi upande upi?

KP: Kwangu pande zote ni muhimu na ninazipenda. Kwanini? Wote wananifanya niamini kuwa kazi inafanyika, ukichukia maana yake kazi inafanyika, ukifurahi pia maana yake kazi inafanyika.

BC: Nini maoni yako kuhusu tuhuma kwamba wachora katuni wengi, hususani wanaochora katuni za kisiasa (wewe unachora pia japo sio kila mara) huwa wanaegemea zaidi upande wa mabaya (negatives) zaidi ya mazuri(positives)?

KP: Bahati mbaya sana tunaishi katika mazingira ambayo mustakabali wa maisha yetu unategemea sana maamuzi ya wanasiasa tofauti na nchi kama Japan ambayo mwanasiasa ni mtunzi na msimamizi wa sera tu na mfanyabiashara na mkulima ndio wanaoweza kubashiri mustakabali wa nchi kutokana na trend ya kilimo na biashara kwa ujumla. Kwa nchi kama Tanzania, bahati mbaya, wengi wa hawa wanaopewa dhamana ya kuamua hatma ya maisha yetu wanachokifanya kwa kweli ni madudu tu, na ndio maana wakati wote tunalazimika kuwa negative kwao si kwa chuki bali kuwekana sawa ili na sisi tuweze kuishi kama wanavyoishi wenzetu katika maeneo mengine ya dunia. Sitaki kupoteza muda na nafasi ya safu hii kuanza kuorodhesha dhambi za baadhi ya watendaji wetu, kila mtanzania anafahamu.

BC: Mara kadhaa katuni zimesababisha sokomoko za aina yake kutokana na wengine kuhisi wamekashifiwa kutokana na mchoro wa katuni. Unawezaje kuhakikisha kwamba katuni zako hazisababishi sokomoko au mitafaruku ndani ya jamii?

KP: Sio siri, katika kuchora katuni, umakini wa hali ya juu unatakiwa. Na ili uweze kuwa makini basi ni lazima uwe na talent ya hali ya juu hasa katika upande wa uwezo wa kumchora mtu bila ya kumuandika jina lake mgongoni, na pia lazima uwe na analytical thinking ili uweze kuchambua kitu kwa uwezo bila ya kuonekana umemshambulia mtu. Haya ndiyo yanayoweza kukuokoa katika masokomoko na mitafaruku ya kashfa. Kwa miaka mingi nimekuwa nikiwachora viongozi vibaya lakini hakuna hata siku moja niliyompa mtu nafasi ya kunibana kisheria.

BC:Kwa vijana wadogo wanaotaka kuibuka siku moja na kuwa kama wewe au kufikia hapo ulipo unawapa ushauri gani na wanahitaji vifaa gani kuanza kuzijenga ndoto zao?


KP:
Kujua kuchora pekee hakutoshi kukufanya uwe mchoraji katuni mzuri. Lazima uwe mjuzi katika masuala ya general knowledge, ujuzi wa maarifa huzaliwi nao, unatokana na tabia ya kupenda kusoma na kujua kinachoendelea duniani. Kiu ya kutaka kujua zaidi na kutojifanya mjuaji ndio silaha za kukufikisha katika umahiri katika kuchora katuni.

BC: Pamoja na kuwa mchora katuni maarufu, wewe pia ni mbunifu wa nguo na mitindo (fashion designer) na pia mtangazaji wa Clouds FM. Nini au nani alikushawishi kuingia katika fani hizo?


KP:
Yawezekana dhiki na matatizo ndicho kichocheo cha kumfanya binadamu aweze ku-excel katika maisha, nami pia nataka kuamini kwamba matatizo ndio chanzo cha ubunifu katika kukabaliana na mitihani mbalimbali ya kimaisha, yawezekana ndo maana leo hii mimi ni mchoraji, mtangazaji na mbunifu wa mavazi, pamoja na utashi na upenzi katika fani hizo, bado kiu ya kuwa na financial independence ndio ndoto yangu.

BC: Kwa jinsi ulivyo na kazi lukuki ni wazi kwamba una ratiba ngumu ya kila siku. Unaweza kutuambia kwa kifupi ratiba yako katika siku ya kawaida? Yaani unaamka saa ngapi,unalala saa ngapi nk?

KP:Alarm inaniamsha saa 11 alfajiri, naoga, navaa na kuelekea studio. Naanza kipindi saa 12 mpaka 3 asubuhi, baada ya hapo napumzisha akili kwa kama nusu saa kwa kupitia magazeti mbalimbali then naanza kufikiria wazo la katuni, wakati mwingine kama sina wazo hunichukua mpaka nusu saa kudevelop wazo la katuni, by saa 4 asubuhi naanza kuchora editorial cartoon. Huwa natumia mpaka masaa mawili kutegemeana na aina ya katuni, baada ya hapo, saa sita mchana namkabidhi dereva (wa taxi, sio wangu jamani) apaleke katuni ofisi za gazeti la mwananchi kwa ajili ya kesho yake. Baada ya hapo nageukia upande wa illustrations, mara nyingi huwa nina kazi za taasisi mbalimbali za ku-Simplify text into cartoons kwa ajili popular versions za machapisho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
By saa 8 mchana huwa nimemaliza, kama kunakuwa na mikutano ofisini naingia, kwa kifupi by saa 10 jioni nakuwa nimemaliza ingawa wakati mwingine humaliza jioni zaidi, baada ya hapo narudi nyumbani kwa ajili ya kubadilisha nguo then naenda mazoezini. Nikitoka mazoezini huwa sitoki tena nyumbani.

BC: Kwa kumalizia, kuna lolote ambalo ungependa kuwaambia wasomaji na watembeleaji wa tovuti hii?


KP:
Ningependa kuwaomba wasomaji na watembeleaji wa tovuti hii wakae tayari kwa nguo zangu ambazo nafanya launching ya nguo za KP kati ya July na August.

Nawategemea sana watanzania walioko nje ya nchi kunisapoti kwa kununua nguo zangu. Kwa kifupi ni kwamba natengenezea nguo hizi Uturuki, India na China. Kwa hiyo jeans, mashati ya kike na kiume, tops, tshirts, skirts na nk zitakuwa zinapatikana. Nakamilisha taratibu za international banking na wanaosafirisha vifurushi ili utapofika muda walio nje waweze kuzipata kwa urahisi, utaratibu wa oda nitawajulisha kupitia tovuti hii.

BC: Asante sana Masoud Kipanya, tunakutakia kila la kheri katika kazi zako.

KP: SHUKRANI.
 
Huyu jamaa nimekuwa nikimfuatilia muda mrefu ...........Aisee huyu jamaa ni kichwa sana......Yani unaweza ukachukua threads kibao za JF na comments za watu, lakini yeye akaweza kuyapresent kwa mchoro mmoja tu.......

Matatizo mengi sana ya kijamii amekuwa akiyawakiisha katika michoro yake......Na kuna muda inahitaji akili ya ziada kuweza kuelewa michoro yake..............Michoro yake mingi imejaa Sarcasm na inakosoa kila penye kosa bila kujali ni upande wa serikali wala upinzani.............

Kuna muda anaweza akatoa mchoro wake ukauchukulia poa mpaka baada ya muda ndo unaelewa alichokimaanisha.....Mfano ile ishu ya Sefue kutumbuliwa.....

Nikawaza kuwa huyu jamaa anapaswa kupewa degree ya heshima na vyuo vyetu hapa Tz.....

Hebu mwenye kumjua vizuri historia yake kielimu aitupie hapa ili tumfahamu kwa undani.....Jamaa ni kichwa sana...


INTERVIEW YA PILI YA KIPANYA NA BC MWAKA 2008

Kwa wengine bado anaendelea kuwa mchora katuni aliye maarufu zaidi nchini Tanzania.Kwa wengine ni mtangazaji maarufu wa redioni ambaye kila asubuhi huwapa wasikilizaji habari mbalimbali na pia burudani. Lakini kwa wengine,yeye ni mbunifu wa mitindo(fashion designer) ambaye anakuja juu kwa kasi ya aina yake.Huyu si mwingine baliAli Masoud,(pichani) maarufu kama Masoud Kipanya au ukipenda KP.

Leo hii yawezekana kabisa kusema kwamba Masoud ni kijana mjasiriamali ambaye anajaribu kutizama mbali kushinda maelezo. Ni kijana anayependa kujishughulisha kwa bidii na maarifa bila kuchoka wala kukata tamaa.Mwaka jana alitimiza mojawapo ya ndoto zake za muda mrefu kwa kuzindua lebo/nembo ya KP iliyokwenda sambamba na KP Wear.Hivi leo sio ajabu kukutana na watu mitaani waliovalia nguo zenye nembo na ubunifu kutoka kwa KP!

Kwa mara ya pili,hivi karibuni BC ilifanikiwa kupata fursa ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na sio uchoraji katuni wala utangazaji bali ubunifu wa mitindo. Nini kilimsukuma kuingia kwenye fani ya ubunifu wa mitindo?Unataka kuijua falsafa inayomuongoza katika fani hii?Je anahofia kitu gani zaidi linapokuja suala zima la ubunifu wa mitindo?Nini mipango yake ya sasa na baadaye kidogo?Kwa hayo na mengineyo mengi zikiwemo picha za baadhi tu ya viwalo vilivyosheheni ubunifu wake,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Masoud Kipanya,karibu kwa mara ya pili ndani ya BC.Tofauti na tulipofanya mahojiano nawe kwa mara ya kwanza,safari hii tunataka kuongea nawe kuhusu na kazi zako za ubunifu wa mitindo.Kwanza hongera sana kwa kuanzisha lebo ya KP.Mambo yanakwendaje mpaka hivi sasa? Watu wameipokea vipi KP?

KP:Namshukuru sana mola, watu wameipokea vizuri sana sana sana KP ingawa bado kuna wachache ambao wangali wamepigwa na butwaa wakiamini kwamba ninachofanya ni kununua nguo na kuweka lebo. Naomba nitumie nafasi hii kuwaambia kuwa sisi sote, hasa watu weusi, tumepewa uwezo wa hali ya juu kifikra, kinachotukwamisha ni kutojiamini na kujidharau.

BC: Unaweza kutuambia nini kilikusukuma kuanzisha lebo ya KP?Ulifikiaje uamuzi wa kuiita KP?

KP:Ni muda mrefu sana nimekuwa nikitamani kuona mtu ama watu wakiwa wamevaa kitu nilichotengeneza mimi.Na hili lilipata msukumo zaidi katika miaka hii ambayo nimekuwa nikichora. Mara zote tunapochora watu lazima uchore na nguo, hili lilipelekea kutamani kuona mtu wa kweli akiwa amevaa nguo niliyoibuni.

KP imetokana na KIPANYA, na huwezi amini, Marehemu Amina Chifupa ndiye aliyekuwa akinikatisha kwa kuniita KP tulipokuwa katika vipindi vya watoto miaka ya nyuma, hivyo nikaamua kulisajili na kulitumia kama lebo ikiwa na kichwa cha Kipanya mwenyewe.

BC: Kumekuwepo na maswali mengi sana kuhusiana na mchango au involvement nzima ya mbunifu wa mitindo(fashion designer) kama wewe katika zoezi zima la kutengeneza nguo,yaani kuanzia mwanzo mpaka inapofika dukani.Unaweza kutuambia kwa kifupi jinsi wewe mwenyewe, kama Masoud Kipanya, unavyoshiriki katika zoezi zima.

KP:Asante kwa swali zuri ambalo litazidi kuweka wazi mchakato mzima.Ninachofanya ni hivi; kichwani nakuwa na aidia ya dizaini ya kitu husika, iwe ni shati au tshirt au jeans au chochote, kisha nachora katika karatasi na ku-save kwenye cd, kwa kuwa huwa natengenezea nje. Nikifika kule huwa naenda katika masoko makubwa ya material, kisha nachagua huku nikijua kuwa kila material ninayonunua itakwenda kutumika katika mchoro fulani.

Baada ya hapo nakwenda katika factory zinazotengeneza lebo, kuanzia vigozi vya jeans mpaka vifungo vikubwa vya jeans vikiwa na logo ya KP. Then nakwenda viwandani nikiwa na lebo na dizaini ninazotaka.Within a week wananitolea sampo, nikiipitisha wana-produce kwa idadi ninayotaka.Ni zoezi gumu linalohitaji commitment ya hali ya juu.


BC: Kila mbunifu wa mitindo huwa na falsafa au mwongozo wake kuhusiana na sanaa ya mitindo.Unaweza kutuambia yako ni ipi?

KP:Falsafa inayoniongoza au ninayoitumia katika sanaa ya ubunifu wa mavazi ni ukweli usiofichika kwamba fashion design has no rule, one can branch out to where no one has ever thought of reaching.

BC: Ni wabunifu gani wa mitindo,ndani na nje ya Tanzania,ambao unadhani kwa njia moja au nyingine wamechangia kuikuza sanaa yako ya ubunifu wa mitindo?Kivipi?

KP:Wabunifu wa ndani walionitangulia wamenisaidia sana kwa ku-pave the way.Hawa, akiwemo khadija Mwanamboka na Mustafa Hassanali, wamewafanya watanzania wengi japo kwa taratibu kuanza kutuamini. Wa nje wengi wao wamekuwa wakinipa usongo wa kutamani kufanya wanayoyafanya, (sio kutamani kuwa shoga ohooooo!!!)

BC: Nini unakipenda zaidi na nini usichokipenda kuhusiana na kazi yako ya ubunifu wa mitindo?

KP:Kwa kweli nafurahia kila hatua ya kazi ya ubunifu, kinachonikera ni ile hali ya kwenda kuhangaika nchi za watu kutengeneza nguo wakati viwanda tunavyo ingawa vyote vimebinafsishwa na matokeo yake sasa ukiwa na oda ndogo ya $ 20,000 au $40,000 hawakubali kwa vile tu nguo zote wanazotengeneza wana-export kutokana na oda za mamilioni ya dola wanazopata kutoka makampuni makubwa duniani.


BC: Kila binadamu hutokea akawa na rangi(zinaweza kuwa nyingi) anayoipenda zaidi.Kwa upande wako,je kuna rangi fulani ambayo unaipenda zaidi?Kama jibu ni ndio,kwanini?

KP:Brown ni rangi ninayoipenda sana hasa ninapokuwa nafanya painting, naweza nisiwe na sababu za msingi lakini namna ambavyo nikiwa natumia tubes wakati wa kupaint, huwa inanipa raha kuiua kwa mchanganyiko wa rangi za giza ama kuipa nuru kwa mchanganyiko wa rangi zinazowaka.Matokeo ya mchezo wote huu hunipa raha na kunifanya hata kuithamini zaidi rangi ya miili yetu waafrika bila kujutia kwa nini mimi si mweupe.

BC: Hivi karibuni tulipoweka kiunganishi(link) ya tovuti yako yakpwear.com,kumetokea maoni mbalimbali yakionyesha kwamba watu wengi wanalalamika kwamba bei zako kidogo ni kubwa.Baadaye tulipowasiliana ukaweka mambo sawa kwamba bei zilizokuwa kwenye website zilikuwa zimekosewa au kubandikwa tu kwani tovuti bado ipo matengenezoni.Unaweza kuchukua fursa hii kuwaambia wananchi juu ya bei halisi za nguo zako na ni katika mazingira gani bei zingine zinaweza kuwa katika fedha za kigeni?

KP:Kwanza kabisanaomba niwaombe radhi kwa usumbufu uliojitokeza, kwa wale ambao wameshafika dukani kwangu pale Millennium Towers watakubaliana nami kwamba bei zangu ni za kawaida. Naomba nisisitize, jeans ni wastani wa shilingi 30,000 mpaka 36,000 tu, kwa kifupi hakuna nguo ya shilingi 40,000,zote ni chini ya hapo.

Kilichotokea katika website ni kwamba iko katika matengenezo ili tuwawezeshe walioko mbali waweze kununua online.Bahati mbaya webmaster wangu akaweka bei zile kama mifano, na sikujua kama zingeweza kuwapotosha watu.

Gharama za nguo zitaongezeka nadhani kidogo kwa wale watakaokuwa wanaagiza kutokea mbali kama America, Ulaya na Asia. Hii itatokana na gharama za shipping ambazo nina hakika wote tunazifahamu, hata hivyo haitofikia bei za kutisha.


BC: Unaweza kutuambia matumizi ya mtandao wa internet yanakusaidiaje au yamekusaidiaje kufikia hapo ulipo kama mbunifu wa mitindo?Unaitumia vipi internet kwa kazi zako za ubunifu wa mitindo?

KP:Internet imenisaidia sana kuzitangaza nguo zangu, blogs na websites kama hii ya Bongo Celebrity zinasomwa na watanzania wengi ndani na nje ya nchi.Na ni kwa kupitia mitandao hii ndipo nitakapoweza kuuza nje ya nchi, kwa hilo nawashukuru wajanja waliotutangulia katika teknolojia na ninyi wenye mitandao hii, Mungu awabariki sana.

BC: Wabunifu wengi wa mitindo wamekuwa wakisikia fahari pindi mtu au watu fulani maarufu wanapoonekana wakiwa wamevaa nguo walizozibuni wao.Kwa upande wako,unajisikiaje unapoona celebrity fulani amevaa nguo zako na ungependa siku moja kumuona celebrity gani ambaye bado hajavaa nguo zako akifanya hivyo?

KP:Kwangu iko tofauti kidogo.Celebrity mmoja si sawa na watu kumi wa kawaida.Hivyo basi kiu yangu ni kuona watu wengi wa kawaida wakivaa nguo zangu.Sina tatizo celebrity akivaa nguo zangu, ila kwangu mtu wa kawaida akiikubali nguo yangu nasikia raha kupita kiasi.

BC: Ni kitu gani unachokihofia zaidi kuhusiana na sanaa au kazi yako nzima ya ubunifu wa mitindo?

KP:Nawahofia zaidi mabingwa wa kufoji!! Ingawa kila kitu kitu kimekuwa registered, bado kuna maeneo ambayo watu wanaweza kufoji kwa quality ya chini na kupelekea kuharibu jina la KP.


BC: Katika muda mfupi tu KP imeanza kutanuka na hivi sasa viwalo vinapatikana mikoani.Wakati huo huo umetudokeza kwamba una mipango ya kuhakikisha kwamba KP inakuwa ya kimataifa zaidi na hivyo kupatikana sehemu nyingi duniani.Unaweza kutueleza kidogo kuhusu mipango hiyo?

KP:Yes, kwa kuanzia ukiachilia mbali mikoani ambako nimekuwa nikisogea kama Dodoma, Mwanza na Mbeya huku mipango ikiwa ukingoni kwa Arusha na Tanga.Nategemea kutumia marafiki zangu walioko sehemu mbalimbali duniani kuwa kama mawakala kwa ajili ya kuwafikishia nguo za KP ndugu zangu watanzania na marafiki zao popote pale ulimwenguni. Pia nawakaribisha watanzania mbalimbali walio na maduka ya nguo nk popote walipo ulimwenguni kuwa wakala wa KP.Wawasiliane nami tuzungumze zaidi.


BC: Unatoa ushauri gani kwa vijana au wabunifu wa mitindo wanaochipukia hivi sasa?

KP: Wasiogope, na wala wasikubali kukatishwa tamaa, na hili haliishii kwa wabunifu tu, kwa fani yoyote ile.Ndoto yoyote uliyokuwa nayo inawezekana kuwa kweli. Usiogope kuchelewa, muhimu ni kuanza.Usiishie kuwa na wazo tu bila ya kulitekeleza.

Katika walet yangu natembea na kipande cha karatasi nilichokikata miaka mitatu nyuma, kimeandikwa…You can not get anywhere unless you start.Anza na utashangaa milango ya kupita itakavyokuwa inafunguka kadri unavyoikaribia.Yaani hamjui ni kiasi gani nayapenda haya maisha.

BC: Asante kwa muda wako KP.Tunakutakia kila la kheri katika kazi zako.
 
Mkuu inawezekana mazingira ndio yanayotofautisha, wale waarabu misikiti mingi kuna mazuria sasa hii yetu mingine mpaka kokoto kwanini mtu asipate sijda komavu.
Nashangaa siku hizi anasjida kubwa usoni!Wakati ameanza kusali ukubwani tu..kitu kinanishangaza sana..watu waliozaliwa Saudi Arabia au Dubai ..ambao huwa wameanza kusali toka wakiwa wadogo hawana sijda, lakini wabongo ambao wameijua dini ukubwani,wanasugua uso makusudi mpaka itokee sijda ili waonekane ni watu wadini.Ajabu sana...
 
Kule twitter kipindi cha kampeni za uchaguzi siku moja aliyakanyaga, akamvaa dada moja na jokes zake. Dada Ana madongo ya maana ilibidi mjomba akae chini tu. Watu wanazidiana viwango!
 
Nashangaa siku hizi anasjida kubwa usoni!Wakati ameanza kusali ukubwani tu..kitu kinanishangaza sana..watu waliozaliwa Saudi Arabia au Dubai ..ambao huwa wameanza kusali toka wakiwa wadogo hawana sijda, lakini wabongo ambao wameijua dini ukubwani,wanasugua uso makusudi mpaka itokee sijda ili waonekane ni watu wadini.Ajabu sana...

Yaelekea sigida yake imekukera sana mkuu
 
YASIYOJULIKANA
Ali Masudi kama jinale lilivyo amejieleza vyema kupitia Bongo Celebrity interview. Lakini naonhezea machache yasiyojulikana.

Fani ya uchoraji katika familia yao ilianzia kwa kaka yake marehemu aitwaye Massudi Ali. Ambaye alimaliza shule ya msingi Mwenge. Alikuwa mchoraji lakini alipomaliza elimu ya msingi hakukiendeleA kipaji chake. Kipanya alikuwa darasa la tano wakati kaka yake anamaliza shule. Kipanya alisoma Kijitomyama primary school....

Kaka yake alisafiri (kuzamia) kwenda Afrika ya Kusini ambapo mdogo wake alipopata misukosuko ya watawala alikimbilia huko na kuishi kwa muda.

Kuhusu elimu ni sawa kamamanavyojieleza kwenye mahojiano yake. Amejibidiisha mno baadaye kusoma kozi mbalimbali.....
 
Karudi Clouds Media eeh? Promo Promo Promo
 
Hahaha nyie jamaa mmenichekesha sana
Hata mimi nimecheka sana hawa jamaa nyoko[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Yaelekea sigida yake imekukera sana mkuu
Kuna watu hawana sijda kabisa usoni,lakini wapo karibu namungu..watu wengiwanatengeneza sijda ili waonekane ni wacha
Sijda inategemea na
1.mahala unaposujudu iwe ngumu au laini
2.ngozi ya mtu coz kuna watu nawajua wanasali tangu wanabaleghe hadi leo hawana hyo sijda ""KAMA HUJAELEWA BILA SHAKA ULILETA HASIRA KWENYE MCHEZO USIOHITAJI HASIRA""
Ngozi ya mtu mweusi ni laini kuliko ya mwarabu? Waarabu wanasujudia kwenye magodoro?
 
Kipanya angekuwa na shule asingerud clouds, clouds hurud wasio na shule tu km kina gadner g habash
 
Mkuu watu wa hivyo hawanaga elimu kubwa zaidi ya kipaji! But watu hawajui kuwa Mchoraji yoyote mwenye kipaji halisi, anawaza zaidi ya mtu wa kawaida, na IQ zao Ni kubwa kuliko watu wa kawaida! Pia wanaweza kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja!
umenena sahihi kabsa kipaji halisi kinabebwa na IQ ilikiweze kuonekana na anaweza akachora kitu yule na elimu yako ukashindwa elewa ila yeye akakueleza kwa maneno machache sanaaa
 
Back
Top Bottom