Fantastic Beast
Member
- Feb 18, 2019
- 53
- 539
Kati ya mwaka 2001 mpaka 2014, Balozi Mstaafu Ndugu Siwa alikuwa Afisa Mambo ya Nje, Mkuu katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi iliyoko nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates); Moscow, nchini Urusi na baadaye Berlin, nchini Ujerumani.
Mwaka 2014, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, alimteua Ndugu Ali Idi siwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kigali, nchini Rwanda, nafasi aliyoihudumu mpaka mwaka 2018.
September 2018, aliteuliwa na Hayati Rais John Pombe Magufuli kuwa mwenyekiti wa bodi ya wadhamini NSSF, nafasi ambayo alikuwa anaitumikia mpaka mwaka huu.