Nilipata bahati ya kuwa karibu na lema, mbowe, na viongozi wa Chadema mkoa wa arusha wakati wa maandalizi hadi mazishi ya wapigania uhuru. Wakati wa kampeni za Uchaguzi thread zilizokusudia kuwabomoa mbowe na lema ili wasichaguliwe. Nimewahi kuwa karibu kiasi na zitto.
Leo najivunia sana kupata nafasi ya kushirikiana na lema na mbowe japo kidogo kwenye harakati za mazishi ya wapigania uhuru wetu. Natamani kama ningekuwa na nguvu, determination, organizing skills, uzalendo, ufamamu wa kuzitambua na ku deal na dirty politics za serikali na ccm. Angalau robo yao tu. Viongozi wa mkoa pia hasa mwenyekiti, nawatamani kweli kweli.
Team work, team spirit, kujituma kwa nguvu zote kabisa, kazi usiku na mchana bila kulala, upendo, kusikilizana, heshima kwa kila wazo, kujitolea garama kwa Hali na mali, n.k.
Ukumbuke kwamba ile shughuli ya mazishi ya wapigania uhuru ingekuwa ni ya ccm, Leo hii tungeambiwa zilitimuka billioni tano. Lilikuwa ni tukio kubwa sana kwetu sisi tuliobahatika kuwa behind the camera. Pia ukumbuke polisi na ccm walikuwa wanawasiliana live na wafiwa ili maiti zisije NMC.
Nikipata muda nitaanzisha thread ingine kuwasilisha obseration yangu kuhusu maandalizi na mazishi. Ni rahisi kutazama picha hapa janvini na kutoa maoni yako lakini siyo rahisi kujua what it meant and how it feels like kwa wale wahusika wakuu, yaani lema, mbowe, na viongozi wa Chadema arusha.
Lakini nilifurahi zaidi mno kuona, siku ya tukia, machalii walivyokuwa wanawapenda lema, mbowe, na mwenyekiti wa mkoa. Kila walipoonekana watu walitaka kuwabeba. Kumbuka bila lema fujo ingetokea pale mortuary baada ya maiti kuchelewa kutoka kwa zaidi ya saa nne. Wakati machalii walipoanza kupandisha pale mlango wa mortuary, mbowe aliwaambia subirini lema anakuja. Lema alikuwa getini akimanage machalii wengine. Alipoitwa aliwaambiwa twendeni getini tukacheze regge. Walishangilia wakamfuata kama yule mpiga filimbi aliyehamisha panya kwenye mji fulani. Akakaa pale getini akiwakeep busy na regge na nyimbo za sarafina hadi msafara ulipoanza kwenye saa nane mchana