Wasifu wa Godbless Jonathan Lema

Wasifu wa Godbless Jonathan Lema

Pia Godbless Ni mpambanaji na Visionary wa maendeleo. Always haamini katika kushindwa bali siku zote anaamini kuna best alternative. Hii ilimpelekea kuamua kuunda ArDF yaani arusha Development foundation ambayo tayari mwaka huu inalipia watoto 1000 kutoka familia fukara ada shule ya sekondari hasa kwa walnaoanza form one. 2011.

Ana mpango wa kupeleka wanafunzi wa maskini 25 kusoma vyuo mbalimbali vikuu vya nje na tayari amekwisha establish contact na vyuo hivyo.
Ana mpango wa kutumia slabs au vimatofali kujenga barabara za mji badala ya lami.Hii itapunguza 50mil. TZS kwa kila KM 1 ya barabara itakayojengwa. Yuko determined na anayo support kubwa nyuma yake ambayo si tu ya mnaowaona mikutanoni bali hata millionaires wa Arusha ambao ni wafanya biashara na wasomi wakubwa. Nguvu yake ya kujiamini inatokana na support ya walioko nyuma yake na ukweli anaweza
 
167717_1673406368783_1646147558_1560841_1969257_n.jpg


Amani iwe kwenu Great thinkers
Kwa kweli wote tumeona ushujaa uliooneshwa na Mbunge wa Chadema Arusha mjini katika kudai uchaguzi huru wa meya na naibu wake. Katika harakati hizo ilipelekea yeye kupigwa kionevu na polisi hadi kulazwa hospitali. Still hakukata tamaa, na akaanda maandamano makubwa ya kudai haki hiyo ambapo polisi walimkamata pamoja na viongozi wengine wa CDM huku wakimwaga damu za watu wasiokua na hatia. Hili limetikisa nchi na tunaamini lazima uchaguzi urudiwe. Hivyo basi kwa kutambua mchango wa GODBLESS LEMA, tunaomba yeyete mweye kujua background yake atujuze hapa jamvini.

Yuko kwenye miaka ya mwazo ya thelathini hivi..kielimu nadhani hana elimu kubwa ya darasani kwa maana ya madarasa. Ila nimekuwa nikimfuatilia kwa siku za hivi karibuni anaenekana ni kijana mwenye muamko mzuri wa kisiasa na ameiva kwa kweli. Hakati tamaa na emeonyesha ujasiri mkubwa sana hasa ukizingatia elimu na umri wake. Nadhani hawa ndio wale vijana ambao kama wangepata muongozo mzuri zaidi wangeweza kuwa namchango mkubwa katika nchi hii. Binafsi ninamvulia kofia.
 
Na huyu mmbunge wetu lema kitakachomtenganisha na ubunge arusha labda ni kifo na sii eti akose kura!! soo EEH MUNGU mpe maisha marefu aweze kutuletea maendeleo arusha!! PAMOJA SANA KAMANDA WA ARDHI GODBLESS LEMA
 
Mimi nadhani ukiona huna cha kuchangia si lazima uandike wakati mwingine unaweza kuipotezea tu thread kama uhuisani nayo, mdau ameomba cv ya mtu kwa kua yeye anahitaji kumfahamu, lakini baadhi ya wachangiaji wameanza kwa kutoa majibu ya dharau, yasiyohusiana lakini pia wapo waliotoa jibu la moja kwa moja kulingana na maswali. Tuheshimu mada/mawazo/kutoelewa/kuelewa kwa jambo ambalo mtu anahitaju ufafanuzi. Ni hayo tu

Cv ya lema na mazagazaga hayo yote yaliongelewa Hapa wakati wa kampeni za Uchaguzi. Matukio yote na harakati za lema zinaripotiwa na vyombo vya habari. Huyo alikusudia tu kuleta ushirikina hapa.
 
Kwa kuwa anajua matatizo ya vijana wengi mkoani humo na yeye binafsi ameshawahi kuwa katika kadhia hiyo, hapana shaka atatumia muda wake wa ubunge kutatua matatizo hayo. Badala ya kupoteza muda kwa shughuli ambazo hazina tija kwa wapiga kura wake!

sawa K hawa ndio aina ya wabunge tunaotaka, wanaishi na wanaowawakilisha hivyo ni rahisi kujua shida na matatizo yao-embu nimbie mbunge anaishi dar halafu ni mwakilishi wa Tandahimba anaweza kuwa mwakilishi mzuri wa hawa watu kweli? anaweza kujua shida zao kwa dhati? Hawa viongozi wetu matawi ya juu hata wanapokwenda huko majimboni kweli wanafika kwa wananchi wa kawaida? Hakuna haja kweli kwenye mchakato huu wa katiba unaoendelea kukawa na kipengele chenye kulazimisha mbunge akaishi na wale anaowawakilisha?
 
Michelle kwa kusafisha majina ya "wanyumbani" kwa kweli nakukubali....Huyu jamaa angekuwa wa kwengine sidhani kama kungelika hapa na CV yake ya ubabaishaji Bin ujanjaujanja....

Ha ha ha h ah haaaaaaaaa KAMARADE, huyu wa nyumbani kwa nani???ila sijasema uongo, nimesema ukweli na kuna sehemu nimekiri kweli mapungufu yake katika biashara na ikanibidi kueleza mazingira ya kufanya biashara ya wachimbaji wadogo au wale wanaouza madini ya wachimbaji wadogo,hakuna msafi 100%,ni ishu ya serikali kuwasaidia hawa watu na kuweka mazingira ambayo hawa vijana wanafaidi jasho lao,lakini kwa hali hii.....Arusha patakuwa pachungu kwa CCM na watu wa CCM wenye mahoteli,ma-apartment,na ardhi kubwa,natamani ningewaleleza ukweli kuhusu hali yao na mali zao if serikali isipowasaidia ndani ya miaka mitano na ndo maana inakuwa ngumu kuachia umeya manake siri zilizoko Manispaa zikitoka patachimbika.
 
Pia Godbless Ni mpambanaji na Visionary wa maendeleo. Always haamini katika kushindwa bali siku zote anaamini kuna best alternative. Hii ilimpelekea kuamua kuunda ArDF yaani arusha Development foundation ambayo tayari mwaka huu inalipia watoto 1000 kutoka familia fukara ada shule ya sekondari hasa kwa walnaoanza form one. 2011.

Ana mpango wa kupeleka wanafunzi wa maskini 25 kusoma vyuo mbalimbali vikuu vya nje na tayari amekwisha establish contact na vyuo hivyo.
Ana mpango wa kutumia slabs au vimatofali kujenga barabara za mji badala ya lami.Hii itapunguza 50mil. TZS kwa kila KM 1 ya barabara itakayojengwa. Yuko determined na anayo support kubwa nyuma yake ambayo si tu ya mnaowaona mikutanoni bali hata millionaires wa Arusha ambao ni wafanya biashara na wasomi wakubwa. Nguvu yake ya kujiamini inatokana na support ya walioko nyuma yake na ukweli anaweza

Well said Mvumbuzi,na wajue pia anao rafiki zake wafanyabiashara Uingereza na Marekani na ndo wameahidi hata ambulance kila kata ambazo Lema amesema zitakuja hivi karibuni.Mungu amsaidie at least na wa hali ya chini wawe na access na huduma nzuri za jamii.
 
hi! pia kuwekwa ndani na kupata misukosuko ya kipolisi kwa Tanzania ni jambo la kawaida kabisa kwa mtu asiyetaka ujinga!!!

binafsi nimeishaibwaga polisi mahakamani katika kesi waliyionifungulia ya trafiki baada ya mimi kugoma kumaliza shauri kienyeji. walijitahidi kunionjesha na selo ili niyumbe. lakini ilichukua almost two years!!!
 
Godbless Lema ni mtoto wa mjini, tapeli turned into politics. Kama ukiweza fanya background check yake pale mahakamani utaona mara ngapi alivyoburuzwa kortini kwa tuhuma kibao za utapeli. Ila demokrasia imechukua mkondo wake na kapewa ubunge na wana Arusha.

Jaribu kutumia busara. kumtukana huyu mtu ni kuwatukana watu waliomchagua.
 
umeimalizia vizuri sana post yako.wananchi wamechoka na 'wasomi' waliotegemewa kuleta mabadiliko wamechemsha hivyo wenyenchi wametumia haki yao kumuweka mtu atakayetekeleza wanachokikata.

Mtu mmoja alikuwa anamiliki kiwanda na siku moja alipelekewa majungu na mmoja kati ya maafisa wa kiwanda ngazi za juu kuwa mhasibu wake alikuwa akimwibia na pia hakuwa na elimu. Jibu toka kwa mwajiri lilikuwa rahisi. ‘kama huyu si msomi na ameweza kuiba hizo hela unazosema nikiweka huyo msomi si ndiyo atafunga kiwanda"? so, usomi si kitu bali kuelewa mambo yalivyo na kuwa na commitmet.
 
Shida ya watu wengi wanachanganya usomi na CV. Utasikia wanasema fulani hana CV, wakati wanayemsema anaishi, ana mke au mme, ana biashara zake, n.k. Na mwingine ataambiwa ana CV kali, kisa ana PhD na hajawahi kufanya kazi mahali popote!

Mwaka 1995 James Mbatia wakati anagombea ubunge wa Vunjo mtu mmoja alisimama na kumwambia 'Hatuwezi kukuchagua kwa kuwa hauna CV kwa sababu ulifukuzwa Chuo Kikuu (UDSM)'. Katika kumjibu, Mh. Mbatia alisema "Hata mtoto anayezaliwa na kufa siku hiyo ana CV, sembuse mimi ninayeishi hadi leo?. Basi hata kufukuzwa Chuo Kikuu ni sehemu ya CV"
 
Amesoma kama sikosei advanced Diploma ya HR pale IAA
Ni mume wa Neema Tarimo
Ana watoto wawili
Ni mchaga wa Machame
Ni mfanyabiashara
Amejiunga CHADEMA akitokea TLP,aligombea ubunge kupitia TLP 2005
Dini yake ni mkristo wa dhehebu la Lutheran
...............................................................................
...............................................................................
...............................................................................

Yaani angekosa wasifu wa kuwa mchaga na kale ka ukristo ketu, wasifu huu usinge timia
 
umeimalizia vizuri sana post yako.wananchi wamechoka na 'wasomi' waliotegemewa kuleta mabadiliko wamechemsha hivyo wenyenchi wametumia haki yao kumuweka mtu atakayetekeleza wanachokikata.

hapo kwenye red umechemsha!!ushaambiwa GL ana advanced diploma ya hr...kwani kwako wewe msomi mpaka awe na phd au masters??nieleweshe msomi anaanzia elimu gani??
 
Mi ninavyojua godbleas lema,ni mmachame,wa nronga,ni baba wa watoto 2,kuhusu elimu mi sijui kapataje diploma,mana najua ajafika form 4.aliyesoma nae au anayejua shule aliyesoma atujulishe.
 
Mi ninavyojua godbleas lema,ni mmachame,wa nronga,ni baba wa watoto 2,kuhusu elimu mi sijui kapataje diploma,mana najua ajafika form 4.aliyesoma nae au anayejua shule aliyesoma atujulishe.

naona ulijiunga jf sababu ya umbea tu,kudanganya elimu ni sababu ya kukuondolea ubunge mahakamani lakini sababu hiyo haijatajwa kwa lengo la kumvua ubunge na ipo wazi,rejea kesi ya uchaguzi mwaka 1995 kati ya kihiyo vs nccr-mageuzi
 
Amesoma kama sikosei advanced Diploma ya HR pale IAA
Ni mume wa Neema Tarimo
Ana watoto wawili
Ni mchaga wa Machame
Ni mfanyabiashara
Amejiunga CHADEMA akitokea TLP,aligombea ubunge kupitia TLP 2005
Dini yake ni mkristo wa dhehebu la Lutheran
...............................................................................
...............................................................................
...............................................................................





Heshima kwako Michelle,

Kwanza naomba nikupongeze kwa kujaribu kupotosha jamvi najua si kosa lako bali ushabiki uliopitiliza ambao sasa umekuwa sehemu ya utamaduni wa kizazi chetu pengine kwa kupenda au kuendekeza ushabiki usio na mashiko.
Najua wapo great thinker kibao lakini linapokuja suala hasi kuhusiana na CHADEMA utashangaa akili zinawekwa kwapani.

Bibi/Bwana Michelle umedai Mheshimiwa Godbless Lema kasoma IAA Advance Diploma HRM huo ni uongo wa mchana kweupe IAA hawatoi cource ya HRM.IAA walikuwa wanatoa Advance Diploma za Accounting,Banking & Finance,Procurement & Logistics Management,Economics & Finance,Business Management,Computer Sciences and Information Technology cources zote hizi zimebadilishwa kutoka Advance Diploma na kuwa Bachelor.Inashangaza sana umeweza kujua Lema ana watoto wawili,ni mmachame na jina la mkewe lakini chuo alichosoma huna uhakika ?????.

Mheshimiwa Godbless Lema ni mbunge wa Arusha mjini hakuna haja ya kuendelea kuudanganya umma juu a elimu yake sijui kwa faida ya nani !.Kura zake zilitosha wengi walimchagua great thinker wanajua sababu za ushindi wa wabunge wengi wa CHADEMA Pasco aliwahi kutoa bandiko lake kipindi cha ufunguzi wa bunge binafsi nilikubaliana na hoja zake.

Mheshimiwa Godbless Lema kasoma Kibohehe hadi kidato cha pili [form two] machilii wa Arusha wana msemo "hakutoboza kidato cha nne".Wapigakura wengi wa Arusha hawakutilia maanani suala hilo ndiyo maana ni mbunge haijalishi unapenda au umechukia.CV za wagombea ubunge wa jimbo la Arusha nilizitoa kipindi cha mchakato wa uchaguzi ya Lema ilikuwepo wapenzi wengi wa CHADEMA hapa jamvini walisoma na wanajua ukweli umesimama wapi.Haishangazi hata kidogo kusoma kejeli na maneno ya dharau unapozungumzia suala baya kuhusiana na CHADEMA.

Wapo wabunge wengi wa bunge la sasa ambao CV zao ni ndogo kuliko Mheshimiwa G Lema eg Professor Maji Marefu na Mbunge wa Rorya tofauti yao na Mheshimiwa Godbless Lema ni moja wao wamekiri hadharani mbele ya wapiga kura wao juu ya elimu yao.katiba ya JMT inamtaka mgombea ubunge ajue kusoma na kuandika [kiswahili] sifa ambayo Lema ameifkia na kupitiliza sana sioni sababu za kuudanganya umma.

Matukio ya maandamano na mauaji yaliyotokea Arusha hayana uhusiano na ujasiri wa Mheshimiwa Godbless Lema hata kidogo matukio hayo yana uhusiano na uzembe,ukatili na ubaradhuli wa watawala wanaotumia [vikaragosi] jeshi la polisi kwa faida za kisiasa bahati nzuri matukio haya yamegeuka mwiba usiosahaulika kwa chama tawala wanajua hukumu yake itakuwa nini pindi wananchi watakapopata fursa ya kuchagua wawakilishi wao.Mheshimiwa Godbless Lema kubeba jeneza la wahanga wa maandamano aliyoyaitisha yeye ni sehemu ya wajibu wake kama asingefanya hivyo dunia ingemshangaa,wapo wengi waliobeba majeneza na bado tutabeba majeneza ya ndugu zetu,jamaa na majirani tusisahau majeneza yetu pia hayatakosa wabebaji.
 
Leo yamekugusa imebidi utoke pangoni baada ya miezi 6.....
mangoa
Junior Member

Join Date: Wed Jun 2010
Posts:1
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 PostsRep Power 0
 
He is a friend of mine and without being biased, he very courageous and very determined person believe me

kwa kweli mm simjui mbunge huyu wa arusha, ila kwa matukio ninayoyaona kupitia tv na redio anaonekana ni mtu jasiri sana, mungu amsaidie asonge mbele,tunahitaji watu majasiri kama lema kwa wakati huu ili tuweze kutoka katika minyororo ya utawala thalimu wa CCM.
 
Back
Top Bottom