nguluvisonzo
JF-Expert Member
- Dec 27, 2010
- 515
- 71
Jamani jaribuni kumuelewa Masando anasema nini?mbona mnaingiza mada nyingine sasa mnakuwa kama sio great thinkers,mambo ya waarabu ya nini hapa tuongelee yetu,Approach ya Lema ndio inayotakiwa kudai haki kutokana na watawala wa Tanzania walivyoziba masikio yao kwa pamba,wamenogewa mpaka wanaona ni dhambi kuachia madaraka,ni dhambi kwao kuwa wakweli,ni dhambi kwao kuacha kuiba mali ya umma na hata kura,ni dhambi kwao kuona CDM inashika dola,ni dhambi kwao kuona CUF inashika dola,ni dhambi kwao kuona NCCR kushika dola,ni dhambi kwa CDM kuwa chama rasmi bungeni kwa tafsiri walioifuta, sasa ukiangalia vyote hivi mimi ninakubaliana na Msando kuwa iko haja ya kubadili approach ya kudai haki,kwani haki haiombwi.Ukichunguza vizuri kuna mambo ambayo sasa yamelegezwa baada ya CDM kufanya,naomba niwambieni kuna vitu viwili vimefanyika baada ya maandamano ya tarehe 05.01.2011 Arusha,uchaguzi wa meya Mwanza ilibidi ufanyike na mshindi halali kupatikana,maana huko nako CCM walikuwa wanaleta kasheshe wakitaka wao ndio wawe na meya,maandamano sasa hivi yanafanyika baada ya watawala kuona sasa wao ndio wavunja katiba,wangekuwa na uwezo leo wangebadilisha na kuondoa kabisa kipengele kinacho sema ruksa maandamano baada ya kutoa taarifa,na hili alilofanya Lema kwa mtoto wa mkulima nalo ni fundisho kwa watawala na hawatarudia tena kuwa bias na kudhulumu haki ya watanzania.Bado inabidi tuwasaidie wale wote walioamua kujitoa muanga kwa ajili ya taifa letu na vizazi vyetu.Tusiporekebisha mfumo wa utawala leo ndio tutaingia katika machafuko yasio ya lazima,hao wanao hubiri amani amani je tuwaulize kwanini wanafinyanga haki zetu za kuchagua,kuchaguliwa,Elimu, afya na nyinginezo,watawala wa Tanzania sasa hivi ndio wamekuwa mabilionea je wamezipata wapi fedha hizi kama sio kudhulumu haki za watanzania.Wakati umefika sasa kila mtu awe askari wa mwenzake tuwamulike wote mabaladhuli wanoipa umasikini Tanzania yenye kila kitu, maji,chakula,madini,gesi,aridhi,misitu,mbuga za wanyama na watu wa kutosha wenye nguvu ya kuzalisha wanokandamizwa na kudhoofishwa kiafya kwa lazima na watawala wetu ili waneemeke wao na famila zao.Nchi hii inaliwa na viongozi kwa mambo ya hovyo hovyo nani aliwaleta au walijuaje tunataka mashine za kufua umeme au kuendesha shirika letu la Reli,ni viongozi hao ndio waliowaleta Dowans,IPTL,RITES,RICHMOND na wengine wote wanao dhulumu haki yetu hakuna mwingine ni viongozi wetu fuatilieni sana hivi vitu vinavyoitwa ziara ziara za viongozi ndio haya mambo yanakotokea,tusubiri hao wafanyabiashara wa India tulioambiwa watakuja kuwekeza kwetu kuna madudu humo ndani yatakuwapo tu ninavyo hisi,ndio yalikotokea IPTL,kuna mradi ulikuwa uje wa kusafisha maji ya bahari ili kutumiwa na binadamu kwa kunwa huo mradi nilikuwa nasubiri nione watanzani ambavyo tungekamuliwa mpaka tukauke damu na mradi mingine mingine,maana viongozi wetu wamekuwa wepesi wanarubuniwa na wao wanakubali kwa kupewa au Pesa au ubia wa hayo makampuni
Hima sasa tuongeze nguvu tulinde mali zetu na utajili tulio nao kwa manufaa ya Tanzania.
Hima sasa tuongeze nguvu tulinde mali zetu na utajili tulio nao kwa manufaa ya Tanzania.