Wasifu wa Godbless Jonathan Lema

Wasifu wa Godbless Jonathan Lema

Kiherehere tu hicho, yaani wako kwenye mabasi yao bado wanaingia stendi badala ya kwenda Lumumba

Huwa hawana aibu hao. Sijui mtu anakatizaje mitaani huku ametinga kijani na njano na mkononi amebeba tochi kwa sababu ya mgao wa umeme!!
 
CCM hawasafishiki tatizo wanaoga maji yenye tope na kujipaka oil chafu eti ni mafuta halafu wanaulizana hivi tunang'aa?halafu style hiyo unaiita kujivua gamba kichekesho na watazomewa sana tu wananchi si wajinga kama walivyozoea kuwadhani.Walikua wanawavumilia sasa wamesema BASI.
 
Kweli vichaa ni wengi sana mjini yaani waliamini kuwa wamevua magamba na kila mwananchi sasa anawaona kama masupastaa waliofanya kazi inayotakiwa kusifiwa na kuenziwa! Thubutu they didnt get us all
 
Wapendwa wana jf naombeni kujuzwa kwa anaejua historia fupi ya mh. Godbles lema nakiwango chake cha elimu alichonacho kwa sasa.. Maana huyu ni mpambananaji mzalendo mwenye mawazo pevu na mjasiri.. Naomba kuwasilisha
 
umeimalizia vizuri sana post yako.wananchi wamechoka na 'wasomi' waliotegemewa kuleta mabadiliko wamechemsha hivyo wenyenchi wametumia haki yao kumuweka mtu atakayetekeleza wanachokikata.

jackbauer nimekupa thanks hapo kwa kweli
 
Chadema kuna mashujaa wengi sana japo pia kuna mamluki kibao km zitto, safari,shibuda
 
Najua imechukuliwa kisiasa lakini ukweli ni kuwa serikali haijawasaidia vijana wa Arusha kuwa tofauti,hawana utaratibu mzuri wa kuuza madini yao,wanadhulumiwa na hawalipwi huko wanakofanya kazi,wengi wao pia hawana ajira na mbaya zaidi kuna kazi kama za tours sasa hivi zimeingiliwa na Wakenya na ndo maana wamefika point ya kukata tamaa,Arusha ni mji wa kitalii maisha ni magumu,mazingira ya kufanya biashara pia ni magumu na vitu ni ghali sana.......Serikali ya Chama cha Mapinduzi inapaswa kuangalia sana suala la Arusha na kwa kushirikiana na Lema anayeelewa undani wa maisha ya vijana.....kufanya siasa na kutumia nguvu haviwezi kubadili tabia ya watu wenye njaa.....gap kati ya maskini na tajiri ni kubwa sana Arusha kuliko sehemu yeyote ya nchi hii,its a point of no return,wanasema bora kufa kwa ajili ya nchi yao kuliko kuishi maisha marefu watu wachache wakifaidi mali asili na opportunities zinazopatikana nchini...........mi sishangai watu wa Dar kutofautiana na wa Arusha na kushangaa kwa nini hawa vijana ni wakali hivyo,ni ugumu wa maisha.....

Hivi Madam Michelle mida mingine huwa unapotelea wapi? Napenda sana uchangiaji wako hapa JF. Kwa kweli wewe ni great thinker. Ninakukubali
 
God bless lema ni kijana safi, anayempenda Mungu na familia yake. Sidhani hata kidogo kama aliwahi kuwa tapeli. Acheni usanii tutumie jf vizuri.
 
Lema maepitia maisha ya kila aina, anazifahamu shida. Mwaka 2005 alipogombea ubunge kwa mara ya kwanza kupitia TLP alikuwa anatumia voks wagen (kobe) kwenye kampeni tena ilikuwa mpaka isukumwe ndo iwake. Lema alishawahi kuuza apples (matunda)mitaani south africa na botswana, Leo ni mbunge wa jimbo nyeti kama arusha na wana- arusha mimi nikiwepo tunamkubali kupindukia. Kwa kifupi tumekubali kuipa cdm hati miliki ya hili jimbo. Wanamagamba mlie
 
Kwhiyo Bunge 'tukufu' la Tanzania lina stahili kuwa na uwakilishi wa MATAPELI? lol Democracy is interesting...

Nani ambaye si tapeli? Ni Kikwete aliyeingia ikulu kwa fedha za EPA? Rostam, Lowassa, Mkapa aliyejitwalia mgodi wa nchi, Magufuli aliyeuza nyumba za Serikali. Wote katika CCM pia ni Matapeli.
 
Amesoma kama sikosei advanced Diploma ya Human Resources Management( Cambridge International University,Certificate of Effective Management of Leadership,he is doing Bachelor of Business Adiministration,same college)
Ni mume wa Neema Tarimo
Ana watoto wawili
Ni mchaga wa Machame
Ni mfanyabiashara
Amejiunga CHADEMA akitokea TLP,aligombea ubunge kupitia TLP 2005
Dini yake ni mkristo wa dhehebu la Lutheran
...............................................................................
...............................................................................
...............................................................................
Umesahau kwani alipogombea 2005 alishinda lakini alivuta millions kwa Felix ili akubali kushindwa. 2010 dau lilikuwa dogo kakataa.
 
Mie namwona Lema ni mwanaume wa shoka, mpignaji wa kweli wa shida za wanyonge, mchikia mafisadi, kiboko yapinda n.k
Namkubali mno! naleo akamshushua Mkinda kuwa anamwogopa asimuulize Pinda maswali, Makinda ajiumauma mno mara oooh nafuata jenda, oooh maeneo wanakotoka......lakini ukweli nikuwa wanamwogopa mno Lema kwani ni kisu cha bucha!
 
Godbless lema seems to be patriotic, intelligent enough, strong, tough, persuasive character and a good public speaker. Si msemaji tu, bali anaonekana ni mtu wa vitendo.mimi namkubali sana, na nadhani tungekuwa na wabunge vijana angalao 20 tu wenye character kama yake, nadhani spika annie makinda angeomba to resign because ile approach yake ya wewe mbishi sana, hebu kaa chini , isingekuwa na nafasi bungeni.
 
sidhani kama watu wanaoda Lema ni muhalifu wako timamu kiakili wao hawawaoni majuha ya chama cha revolution wanavozomea zomea inakera na wao ndo wanaongoza kwa mijihalifu mikubwa mikubwa yenye kesi mahakamani mpaka sasa
 
Elimu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, GODBLESS LEMA aliyoieleza Mahakamani wakati ya kesi inayomkabili kufuatia ushindi wake wa Ubunge jimboni humo ni tofauti kabisa na ile iliyoko kwenye profile yake iliyooneshwa kwenye tovuti ya Bunge. Aidha hakuna ukweli wa moja kwa moja wa CHUO ambacho Mh. huyo mwenye Mbwembwe sana alichosomea.

Hebu tuangalie hii ya bunge ilivyo na utata yenyewe kwanza:

  • Kamaliza darasa la saba 1989 na kuanza kidato cha kwanza kwaka huohuo wa 1989. Je hii inawezekana?
  • Ameanza kidato cha kwanza mwaka 1989 na kumaliza 1991. Je miaka hiyo elimu ya kidato cha nne ilikuwa ni miaka 3 badala ya minne?
  • Amemaliza kidato cha nne mwaka 1991 na mwaka huohuo akaanza kidato cha tano. Je hili liiikuwa linawezekana?
  • Hii Diploma aliyosoma Cambridge College ni ya nini? siasa? uchumi? fundi mchundo? au nini?

Iko haja sasa Sheria ifuate mkondo kwa TCU kukagua CV za Wabunge wetu ili kuepusha Nchi yetu kuingia katika majanga yatakayosababishwa na Wanasiasa wa aina hii.

GENERAL
SalutationHonourableMember picture
1748.jpg
First Name: Godbless
Middle Name:Jonathan
Last Name:Lema
Member Type:Constituency Member
Constituent:Arusha Mjini
Political Party:CHADEMA
Office Location:Box 16531, Arusha
Office Phone: +255 764 150747
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail:
Member Status:
Date of Birth
EDUCATIONS
School Name/Location Course/Degree/Award Start DateEnd DateLevel
Kalangala Primary SchoolPrimary Education19831989PRIMARY
Geita Secondary SchoolO-Level Education19891991SECONDARY
Kolila Secondary SchoolA-Level Education19911993SECONDARY
Cambridge International CollegeDiploma20082010DIPLOMA
Cambridge International CollegeDegree2010TodateNOT COMPLETED
CERTIFICATIONS
Certification Name or TypeCertification No. IssuedExpires
No items on list
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From DateTo Date
The Parliament of TanzaniaMember - Arusha Urban Constituency20102015
PTNChief Executive Officer (CEO)20072008
Tanzania Labour Party, TLPDistrict Secretary General20052008
DENETRIADirector20052008
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/LocationPositionFromTo
Chama Cha Demokrasia na MaendeleoMember of Parliament2010Date
Tanzania Labour Party, TLPDistrict Secretary General20052008
Tanzania Labour Party, TLPCandidate, Member of Parliament2005
PUBLICATIONS
DescriptionPublished Date
Lema Godbless: Msaada wa haraka kutoka katika Biblia, Arusha2008
Godbless Lema: Wisdom Time, Arusha2008
SPECIAL SKILLS
Skill Name or DescriptionYears ExperienceAcquired ThroughSkill Level
No items on list
RECOGNITIONS
Recognition TypeRecognition DateReasonAction TakenIssued by
No items on list
 
Back
Top Bottom