Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Wasifu wa makamu wa rais wa Tanzania Samia Hassan
12 Julai 2015
Imeboreshwa 5 Novemba 2015
Historia ya Samia Suluhu Hassan wa CCM
Maelezo ya picha,
Historia ya Samia Suluhu Hassan wa CCM

Bi Samia Suluhu Hassan ameapishwa kuwa makamu mpya wa rais Tanzania na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kabisa kushikilia wadhifa huo nchini humo.

Lakini Bi Samia ni nani?

Bi Samia Suluhu alizaliwa Januari 27, 1960 visiwani Zanzibar. Alisomea shule za msingi za Chawaka (Unguja), Ziwani (Pemba) na Mahonda (Unguja) na kati ya 1966 na 1972 na kisha akasomea masomo ya upili Ngambo, Unguja (1973-1975) na Lumumba, Unguja (1976).

Alisomea kozi mbalimbali hadi akafikia kupata shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Southern New Hampshire nchini Marekani.

MATANGAZO

Kazi

Aliajiriwa kama mchapishaji katika serikali ya Zanzibar mwaka 1977 na akapanda ngazi hadi kuwa afisa wa mipango serikalini kati ya 1987 na 1988.

Alihudumu pia kama meneja wa mradi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Zanzibar kati ya 1985 na 1997, na pia kama meneja mkurugenzi wa Mwamvuli wa NGO 1998 hadi 1999.

Bi Samia anasema kuwa njia yake ya ufanisi haijakuwa rahisi kama inavyodhaniwa.

''Safari yangu katika siasa imekuwa njia ndefu na yenye tija.''

Kimsingi ufanisi wangu katika siasa za Tanzania umetokana na uweledi na umakini katika kila jambo ninalolifanya.''

''Sio rahisi kuwajibikia familia yako wakati huohuo ukiendelea na maisha ya siasa elimu na majukumu mengine ya kikazi," anasema Bi Samia.

Familia

Aliolewa mwaka wa 1978, kwa Bw Hafidh Ameir, ambaye wakati huo alikuwa afisa wa Kilimo .

Walijaliwa watoto wanne.

Mmoja kati ya wanawe Wanu Hafidh Ameir (1982), ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar

Bi Hassan na Dkt Magufuli wakati wa kampeni 2015
Maelezo ya picha,
Bi Hassan na Dkt Magufuli wakati wa kampeni 2015

Siasa

Alijiunga na siasa mwaka wa 2000.

Wakati huo alijiunga na bunge la wawakilishi la Zanzibar kama mjumbe maalum.

Haikuchukua muda mrefu nyota yake ikaanza kung'aa na akateuliwa kuwa waziri na rais Amani Karume, akipewa wadhifa wa Waziri wa Leba, Jinsia na Watoto.

Alitumikia taifa hadi mwaka wa 2005 alipochaguliwa tena na kuteuliwa upya kama waziri, wakati huu akipewa wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji katika serikali ya visiwani.

Mwaka wa 2010 alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi.

Punde tu akateuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa waziri wa maswala ya muungano katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akihudumu chini ya Makamu wa Rais Mohamed Gharib Bilal.

Machi mwaka 2014, aliwania na kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba nmjini Dodoma. Bi Hassan alichaguliwa kwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumshinda mpinzani wake Amina Abdalla Amour ambaye alipata kura 126 sawa na 24%.

Julai mwaka 2015, Dkt John Magufuli alimteua kuwa mgombea mwenza.

Wale wanaomjua Bi Hassan wanasema kuwa ni mchache wa maneno.
 
Hapa hakuna kitu[emoji1]
Wanaukumbi.


MEMBER OF PARLIAMENT CV

GENERAL Salutation Hon.
Member pictureFirst NameSamia
Middle Name:Hassan
Last NameSuluhu
Member Type:Elected Member Constituent: Makunduchi Political Party:
Chama Cha Mapinduzi Office Location.O. Box 3021,
Dar Es Salaam Office Phone:
+255 774 010 203/+255 784 717 712Office Faxffice E-mailsuluhu@parliament.go.tz

Member Status:Active.
Date of Birth 27 January 1960
EDUCATION School Name/Location Course/Degree/Award Start Date
End Date Level Mahonda Primary School, Unguja CPEE19721972
Primary School Chwaka Primary School, Unguja
CPEE1966-1968 Primary School Ziwani Primary School, Pemba CPEE 1970-1971 Primary School Lumumba Secondary School, Unguja CSEE 1976-1976 Secondary School Ngambo SecondarySchool, Unguja CSEE 1973-1975 Secondary School Institute of Management for Leaders, Hyderabad, India
Management Course 1991-1991 Certificate Zanzibar Institute of Financial Administration,
ZIFA Statistics 1983-1983 Certificate National Institute of Public Administration,
Lahore Pakistan Course 1989- 1989 Certificate Institute of Development Management, IDM, Mzumbe (Morogoro)
Advanced Diploma1983-1986 Advanced DiplomaManchester University, London Postgraduate 1992-1994 Postgraduate Diploma Open University Southern New Hampshire, USAM.A 2004-2005 Masters DegreeEMPLOYMENT HISTORY Company Name Position From To The Parliament of Tanzania Member - Makunduchi Constituency 2010-2015 Ministry of Tourism, Trade and Investment, Zanzibar Minister 2005- 2010 Ministry of Labour, Gender Development and Children Minister 2000-2005 Mwamvuli wa NGO Managing Director1998-1999 Revolutionary Government of Zanzibar Planning Officer 1987-1988 World Food Programme, WFP - Zanzibar Project Manager 1985-1997 Revolutionary Government of Zanzibar Typists (Typing Pool)1977-1986 POLITICAL EXPERIENCE Ministry /Political Party/Location Position From To Chama Cha Mapinduzi, CCM Guardian (Warden) - North Unguja Region 2009 Todate Chama Cha Mapinduzi, CCM Guardian (Warden) - North Pemba Region 2004-2007 Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - National Executive Committee (NEC) 2002 Todate
 
Duuh nimetoka nduki mpaka nimejikwaa nilijua tayar
Ha ha haaa.. hata mie nilijua Mola keshafanya kazi yake...! Ila huyu mama angalau anafaa kuchukua hiyo nafasi kubwa japo na yeye kipindi cha uchaguzi alikuwa akiongea shit lakini angalau anasameheka kuliko wakina majaliwa na wengine....
 
Namkumbuka huyo mama na kumheshimu kutokana na video iliyomwonyesha akimjulia hali mgonjwa Tundu lLissu pale Nairobi hospital.

Hakuna ubinaadam zaidi ya ule aliouonyesha pale siku ile.

Nina imani ile ndiyo taswira ya tabia yake halisi.

Haya mengine ni ya kumfurahisha tu mtu mmoja aliye na madaraka juu yao.
 
Namkumbuka huyo mama na kumheshimu kutokana na video iliyomwonyesha akimjulia hali mgonjwa Tundu lLissu pale Nairobi hospital.

Hakuna ubinaadam zaidi ya ule aliouonyesha pale siku ile.

Nina imani ile ndiyo taswira ya tabia yake halisi.

Haya mengine ni ya kumfurahisha tu mtu mmoja aliye na madaraka juu yao.
Unadhani huyo Mama,Mwinyi(mstaafu),JK walimtembelea Lissu bila ruhusa ya mamlaka kuu ili kuonyesha serikali haina mkono kwny hilo?

Aisee kweli hua tunachezewa sana mapicha picha.
 
Ha ha haaa.. hata mie nilijua Mola keshafanya kazi yake...! Ila huyu mama angalau anafaa kuchukua hiyo nafasi kubwa japo na yeye kipindi cha uchaguzi alikuwa akiongea shit lakini angalau anasameheka kuliko wakina majaliwa na wengine....
Daaa
IMG_20210312_230640.jpg
 
Unadhani huyo Mama,Mwinyi(mstaafu),JK walimtembelea Lissu bila ruhusa ya mamlaka kuu ili kuonyesha serikali haina mkono kwny hilo?

Aisee kweli hua tunachezewa sana mapicha picha.
Hapana.

Mimi siko huko, usinisome vibaya mkuu wangu.

Mimi nazungumzia niliyoyaona kwenye video hiyo siku hiyo.

Haya ya maigizo na kupeana ruhusa siyo sehemu ya niliyoyaona kwenye ile picha, na wala siyo ninayoandika juu yake hapa.

Tafadhali naomba unielewe ninachoeleza.
 
Hapana.

Mimi siko huko, usinisome vibaya mkuu wangu.

Mimi nazungumzia niliyoyaona kwenye video hiyo siku hiyo.

Haya ya maigizo na kupeana ruhusa siyo sehemu ya niliyoyaona kwenye ile picha, na wala siyo ninayoandika juu yake hapa.

Tafadhali naomba unielewe ninachoeleza.
Ngoja nijifanye nimeelewa mkuu.
 
Mimeona kuwa mwaka 1986 alimaliza mzumbe na advanced diploma ya uongozi wa umma. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma postgraduate diploma ya uchumi chuo kikuu cha manchester.

Mwaka 2015 alipata Msc in community economic development kutoka chuo kikuu huria na chuo kikuu cha Southern new hampshire.
 
Back
Top Bottom