Naomba nijue wazazi wa mama yetu, sijawahi kuona makala Wala popote wakioneshwa au kusimuliwa. Imekuwa tofauti Kwa watangulizi wake hayati Magufuli wazazi wake wamesimuliwa na mama yake Susanna picha zake zinajulikana, Mzee wake apumzike Kwa amani. Pia mama mlezi wa JK amehojiwa na akaweka wazi kuwa wazazi wa JK walitangulia mbele za haki, mwenyezi Mungu awarehemu.
Kwa mama, yeye alisema baba yake alikuwa mwalimu, hajataja zaidi.
Vyombo vya habari hakuna vilivyomtaja, kama yupo au ametangulia.
Naomba wakuu mnisaidie kujua jina la Babu yetu, tumpongeze Kwa kuzaa mtoto mzuri, anaongoza vizuri na hakika alistahili kuwa alivyo.