Wewe utakuwa umechanganyikiwa. Ni lini Papa alisema mashoga waende wakapewe baraka makanisani?
Mnaokoteza maneno ya mitaani, na kwa sababu za chuki zenu, mnatengeneza tafsiri zenu kuziridhisha nafsi zenu.
Unatakiwa kuelewa misingi ya imani za dini na tofauti zake:
Uislam ni dini inayoruhusu kisasi kwa aliyekukosea, na kukutaka kujiweka mbali na mwovu.
Ukristo unasisitiza upendo, tena hata kwa adui yako. Tena Yesu anasema ukimpenda rafiki yako na kumchukia adui zako, huna tofauti na watu wasiomjua Mungu, maana nao hufanya hivyo hivyo. Halikadhalika Yesu anasema kuwa tabibu hayupo kwaajili ya walio wazima bali wagonjwa. Kwa hiyo yeye hakuja kwaajili ya watakatifu bali kwaajili ya wenye dhambi ili awatoe katika dhambi. Na ili umtoe katika dhambi, ni lazima kwanza umwoneshe upendo wa Mungu. Ndiyo maana Papa akasisitiza kuwa mashoga kama walivyo majambazi, wazinzi, wevi, na wengineo, wasitengwe. Na akasisitiza kuwa ushoga ni dhambi, na hata siku moja Mungu hawezi kubariki dhambi. Kwenye ukristo, hata jambazi akienda kwa kasisi na kusema kuwa anaomba baraka, kasisi atambariki na kumwusia umuhimu wa kuyabadili maisha yake, na kinachobarikiwa siyo ule ujambazi wake au kumtaka aendelee na ujambazi wake, bali kupokea baraka ya Mungu ili aweze kuyatafakari maisha yake na kumgeukia Mungu.