Wasilisho kutoka kwa wataalam wa haki za binadamu - Umoja wa Kimataifa kwa Serikali ya Tanzania

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
11,999
Reaction score
24,328
Hili ni wasilisho lenye maswali magumu yanayohitaji maelezo ya kiina kuhusu kukamatwa, kutekwa na kuteswa kwa @bonifacemwangi na Agather Atuhaire

@un_sp_experts kupitia @unhrcommittee wanahitaji majibu kuhusu yafuatayo🙁nimetafsriri)
👇🏾👇🏾

1. Tafadhali toa maelezo yoyote ya ziada na/au maoni) ambayo unaweza kuwa nayo kuhusu madai yaliyotajwa hapo juu.

2. Tafadhali toa taarifa kuhusu sababu za kweli na za kisheria za kukamatwa na kuzuiliwa kwa watetezi wa haki za binadamu Bi Agather Atuhaire na Bw. Boniface Mwangi. Tafadhali eleza jinsi hatua hizi zinavyoendana na viwango vya kimataifa vinavyohusiana na haki ya uhuru na usalama wa mtu, vilivyoainishwa katika kifungu cha 9 cha ICCPR, na haki za uhuru wa maoni na kujieleza, zilizobainishwa katika kifungu cha 19 cha ICCPR.

3. Tafadhali toa taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali yako kufanya uchunguzi wa tuhuma zilizotajwa hapo juu kuhusu kutekwa, mateso na unahakikisha vipi kuna uwajibikaji na fidia kwa wahasiriwa, ikiwa tuhuma hizu zitathibitishwa?

4. Tafadhali eleza ni hatua gani zimechukuliwa kuhakikisha wanahabari na watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania wanafanya kazi zao kwa amani na uhalali katika mazingira salama na wezeshi bila kuogopa vitisho au vitendo vya vitisho na unyanyasaji wa aina yoyote.

5. Tafadhali onyesha kwa kina ni hatua gani madhubuti ambazo Serikali ya Tanzana imechukua, au inakusudia kuchukua, ili kukomesha matukio yanaoendelea ya kuwalenga watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na wale wanaofanya kazi katika muktadha wa uchaguzi, kwa kukamata na kuwekwa kizuizini, kuteka, kutesa na unyanyasaji na hatua za kufidia familia, waathiriwa na kukomesha unyanyasaji wao. Ikiwa hakuna hatua kama hizo zimefanywa au zinatarajiwa, tafadhali eleza kwa nini.

#TutaelewanaTu

1755261051295-jpg.3442207
1755261060735.jpg
 
Attachments

  • 1755261051295.jpg
    1755261051295.jpg
    302.1 KB · Views: 51
Sema copy and paste
Kazi ni kipimo cha utu
 
View attachment 3442213

Kazi nzuri.
Kwa sasa Watu hao wanapaswa waunde Timu Maalumu ya Wataalamu uli waweze kuandaa Andiko Maalumu la kuweza kutumwa kwa Waendesha Mashitaka wa Mahakama ya Uhalifu ya ICC ili kuwashawishi Waendesha Mashitaka wa Mahakama hiyo waweze kuanzisha Uchunguzi Maalumu wa Kijinai (Criminal Investigation) dhidi ya Serikali ya Tanzania pamoja na Watawala wote kabisa binafsi wanaotuhumiwa kuhusika na Jinai mbaya kabisa za Uhalifu dhidi ya binadamu.
 
Wanamtandao wa kihuni waneifikisha nchi yetu hapa. Watakimbilia kusema tuweni wazalendo kwa nchi yetu. Wakapambane wenyewe huko. Hakuna cha uzalendo hapa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom