Wasimamizi mirathi ya Mengi wabanwa Mahakamani kuhusu matunzo ya watoto wa mjane Jacqueline Ntuyabaliwe

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
mengipiiic.jpg
Mahakama ya Watoto Kisutu imewabana wasimamizi wa mirathi ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, kwa kukataa kuwahudumia watoto wake wadogo aliowazaa na mjane wake, Jacqueline Ntuyabaliwe.

Mahakama hiyo imetoa msimamo huo katika uamuzi wake wa pingamizi lililowekwa na wasimamizi hao wa mirathi hiyo, Abdiel Mengi (mtoto wa marehemu wa mke wa awali) na Benjamin Mengi (mdogo wa marehemu Mengi), dhidi ya shauri la matunzo ya watoto.

Mahakama katika uamuzi wake juzi, ilikubaliana na hoja za wakili wa wadai na ikazikataa hoja zote za pingamizi la wadaiwa, hivyo ikatupilia mbali pingamizi hilo.

Shauri hilo la madai namba 50 la mwaka 2022, limefunguliwa na mjane Jacqueline, kama mlezi wa watoto hao akidai matunzo ya watoto hao ikiwamo ada ya shule, baada ya wasimamizi hao wa mirathi kukataa kutoa huduma kwa watoto hao, akiiomba Mahakama hiyo iwalazimishe kuwahudumia.

Jacqueline anadai kuwa watoto hao walikuwa wakigharamiwa na baba yao wakati wa uhai wake ada ya shule pamoja huduma nyingine zote walizostahili kutokana na kipato alichokuwa anakipata.

Hata hivyo, wadaiwa kupitia kwa mawakili wao, Nakazael Tenga, Hamis Mfinanga na Grayson Laizer waliweka pingamizi wakiiomba Mahakama hiyo isilisikilize shauri hilo.

Walidai maombi hayo yamefunguliwa dhidi ya watu wasiostahili, badala yake hilo ni jukumu la wazazi.

Source: Mwananchi
 
K Lyne si aliachiwa kiwanda cha kuuza samani nje ya nchi, kimeshakufa?

Kwenye maisha hasa ukiwa mke wa mfanyabiashara mkubwa au kiongozi mkubwa, kunakuwa na mawili, uidha ufanye biashara au ufanyiwe biashara.

Ukifanya biashara hata mumeo akifa itashamiri nankuendelea. Ila ukifanyiwa biashara lazima ife ASAP.

Kufanyiwa biashara ni kufanya biashara kwa kupitia mumeo, yaani yeye aitangaze biashara yako, akutafutie masoko, ikiyumba aiinue huku wewe umekaa mbele ya kioo hujui hata mzigo unafungwa wapi.

Jacqueline Ntuyabaliwe ameshindwa kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye ni mwanamke shupavu, mwanamke wa shoka. Badala ya kulia lia alitakiwa zile biashara alizoachiwa na mumewe akiwa hai aziendeleze hizo zimtoe na zimuheshimishe.

Wito wangu kwenu wadada, ukipata upenyo wa kuolewa na tajiri, pambana kwa nguvu zako zote kufanya biashara, uijue na uimudu, usitegemee kufanyiwa biashara na mumeo.
 
Kwenye circle ya familia ya mengi wanachezewa mchezo watakuja kushtuka hawana chao

Yule mjane wa reginald mengi anatumiwa na watu kuhakikisha IPP inafilisika

Ipp haina watu makini,mzee mengi ameacha vijana wasio kuwa na plan ya kuendeleza kampuni

Kunq nia ovu ya kumfanya mjane ashinde kesi,akishashinda kesi atauza hisa zake ambazo ni nyingi ahame nchi kwa ufadhili wa vigogo

Na wanatarget media zaidi wazimiliki ili kuiua ipp abaki mzalishaji moja tu mkubwa

Nimenyetishwa kutoka chanzo makini
 
Hapa somo ni 1 tu. Watoto tuache kusubiria urithi. Acha mzazi aponde mali zake the way anavoona inamfaa..wewe tafuta chako ili kuondoa ugomvi kama huu. Ukibahatika mzazi ni tajiti omba mtaji akiwa hai uanze biashara. Na hata akikataa kukupa mraji usimlazimishe, fight, tafuta chako achana na uvivu. Am sure hao watoto wana uwezo wa kuishi kwa mali zao binafsi ila urohi wa mali na uvivu wa kutafuta chao ndilo tatizo hapa.
 
Vibabu vingine bhana, sijui huwa vinarogwa, kwani angemfanya kimada tu wa kumzalia angepungukiwa nini? Yeye kaoa kabisa..
Tusamehe tu bure. Huwa tunakuwa tumenogewa kiasi cha kujikuta tumechanganyikiwa kabisa. 😫

Kama Mzee Mwenzangu Lyatonga, au Kapuya wangekuwemo humu, basi wangefafanua kwa uzuri zaidi hiki nilicho kiandika hapa.
 
Hapa somo ni 1 tu. Watoto tuache kusubiria urithi. Acha mzazi aponde mali zake the way anavoona inamfaa..wewe tafuta chako ili kuondoa ugomvi kama huu. Ukibahatika mzazi ni tajiti omba mtaji akiwa hai uanze biashara. Na hata akikataa kukupa mraji usimlazimishe, fight, tafuta chako achana na uvivu. Am sure hao watoto wana uwezo wa kuishi kwa mali zao binafsi ila urohi wa mali na uvivu wa kutafuta chao ndilo tatizo hapa.
Bahati mbaya hao watoto wakubwa wa Mzee Mengi walikuwa ni sehemu ya huo umiliki! Maana wamezipambania Kampuni za Wazazi wao kwa miaka mingi kama Wakurugenzi!
Yaani kama ilivyo kwa watoto wa Bakresa vile. Hivyo huwezi kuwatenganisha na mali za wazazi wao.

Na kwa upande wa Jacqueline Ntuyabaliwe, alitakiwa kumshawishi mume wake kumfungulia Kampuni yake na hao watoto wake wadogo. Kitendo cha kukubali kumilikishwa mali ambazo hakuzitolea jasho, inamfanya aonekane ni opportunist.
 
Ilibidi wapewe mshahara kama wafanyakazi wengine ambao pia huwa wanapigania kuendeleza makampuni. Labda hilo hawakuliwazia mapema wao kama watoto. Ni risk kubwa kujifanya sehemu ya biashara ya familia ama mali za familia siku zote maana ndugu pia hugeukana kisa mali. Kama wangekuwa clear toka mwanzo wakawa pale kama wafanyakazi wakalipwa mshahara kama mfanyakazi yeyote na wakawa na business zao tofauti na familia haya yote yasingetokea. Kwani wafanyakazi ambap huwa wanafanya kazi katika makampuni na wakawa sehemu ya maendeleo ya hizo kampuni huwa wanadai urithi? Hapana!!!.
Hili ni somo kwa watu wengine pia. Mali ya familia kaa nayo mbali, msaidie mzazi ila usiwekeze katika mali ya familia ambapo mzazi mmoja akifariki basi unaanza mgogoro na mama/baba/ndugu.. Ndio mwisho watoto sometime wanaua wazazi wao kisa wanajiona wameinvest pia katika mali za familia. Na hata Mengi ilibidi awafundishe hilo mapema ili wajitegemee..Kamwe huwezi kusema huyu ni ndugu au mwanangu au mzazi wangu hawezi kunigeuka...pesa ni shetani ambaye inabidi umuwekee mazingira ya kutokushawishi huko mbeleni. Ni sawa na mtoto kujenga kwente kiwanja cha urithi au cha familia..Mgogoro ukiibuka anakuwa na uchungu wa pesa alizowekeza kuendeleza kile kiwanja..lakini asingejenga pale angekuwa na assets zake ambazo haziingiliani na familia na angeweza kuacha wanaogombea mali wagombee tu.
 
Kwenye circle ya familia ya mengi wanachezewa mchezo watakuja kushtuka hawana chao

Yule mjane wa reginald mengi anatumiwa na watu kuhakikisha IPP inafilisika

Ipp haina watu makini,mzee mengi ameacha vijana wasio kuwa na plan ya kuendeleza kampuni

Kunq nia ovu ya kumfanya mjane ashinde kesi,akishashinda kesi atauza hisa zake ambazo ni nyingi ahame nchi kwa ufadhili wa vigogo

Na wanatarget media zaidi wazimiliki ili kuiua ipp abaki mzalishaji moja tu mkubwa

Nimenyetishwa kutoka chanzo makini
Binafsi, mjane atumiwe au asitumiwe, THE FACT KWAMBA WALE WATOTO NI MENGI, kwanini hawawahudumii? Yaani kuna shida gani hapo watoto kupata huduma?
 
K Lyne si aliachiwa kiwanda cha kuuza samani nje ya nchi, kimeshakufa?

Kwenye maisha hasa ukiwa mke wa mfanyabiashara mkubwa au kiongozi mkubwa, kunakuwa na mawili, uidha ufanye biashara au ufanyiwe biashara.

Ukifanya biashara hata mumeo akifa itashamiri nankuendelea. Ila ukifanyiwa biashara lazima ife ASAP.

Kufanyiwa biashara ni kufanya biashara kwa kupitia mumeo, yaani yeye aitangaze biashara yako, akutafutie masoko, ikiyumba aiinue huku wewe umekaa mbele ya kioo hujui hata mzigo unafungwa wapi.

Jacqueline Ntuyabaliwe ameshindwa kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye ni mwanamke shupavu, mwanamke wa shoka. Badala ya kulia lia alitakiwa zile biashara alizoachiwa na mumewe akiwa hai aziendeleze hizo zimtoe na zimuheshimishe.

Wito wangu kwenu wadada, ukipata upenyo wa kuolewa na tajiri, pambana kwa nguvu zako zote kufanya biashara, uijue na uimudu, usitegemee kufanyiwa biashara na mumeo.

Kauza biashara zote hela katumia kwenye Tea party , watoto walikua wanasomeshwa International School of Tanganyika kawaamishia Dubai

Hawawezi kuishi kama alivyokuepo Dr Mengi , kyln alifanya Mzee akope kila bank kumlidhisha mchepuko
 
Ilibidi wapewe mshahara kama wafanyakazi wengine ambao pia huwa wanapigania kuendeleza makampuni. Labda hilo hawakuliwazia mapema wao kama watoto. Ni risk kubwa kujifanya sehemu ya biashara ya familia ama mali za familia siku zote maana ndugu pia hugeukana kisa mali. Kama wangekuwa clear toka mwanzo wakawa pale kama wafanyakazi wakalipwa mshahara kama mfanyakazi yeyote na wakawa na business zao tofauti na familia haya yote yasingetokea. Kwani wafanyakazi ambap huwa wanafanya kazi katika makampuni na wakawa sehemu ya maendeleo ya hizo kampuni huwa wanadai urithi? Hapana!!!.
Hili ni somo kwa watu wengine pia. Mali ya familia kaa nayo mbali, msaidie mzazi ila usiwekeze katika mali ya familia ambapo mzazi mmoja akifariki basi unaanza mgogoro na mama/baba/ndugu.. Ndio mwisho watoto sometime wanaua wazazi wao kisa wanajiona wameinvest pia katika mali za familia. Na hata Mengi ilibidi awafundishe hilo mapema ili wajitegemee..Kamwe huwezi kusema huyu ni ndugu au mwanangu au mzazi wangu hawezi kunigeuka...pesa ni shetani ambaye inabidi umuwekee mazingira ya kutokushawishi huko mbeleni. Ni sawa na mtoto kujenga kwente kiwanja cha urithi au cha familia..Mgogoro ukiibuka anakuwa na uchungu wa pesa alizowekeza kuendeleza kile kiwanja..lakini asingejenga pale angekuwa na assets zake ambazo haziingiliani na familia na angeweza kuacha wanaogombea mali wagombee tu.

Nani kakwambia hawalipani mshahara , Bakhresa wanalipana mishahara same as Mohamed Dewji na Mengi
 
Kwenye circle ya familia ya mengi wanachezewa mchezo watakuja kushtuka hawana chao

Yule mjane wa reginald mengi anatumiwa na watu kuhakikisha IPP inafilisika

Ipp haina watu makini,mzee mengi ameacha vijana wasio kuwa na plan ya kuendeleza kampuni

Kunq nia ovu ya kumfanya mjane ashinde kesi,akishashinda kesi atauza hisa zake ambazo ni nyingi ahame nchi kwa ufadhili wa vigogo

Na wanatarget media zaidi wazimiliki ili kuiua ipp abaki mzalishaji moja tu mkubwa

Nimenyetishwa kutoka chanzo makini

Hao vigogo wanataka bonite na Migodi , hawatafanikiwa Mungu sio mjomba wao upumzike kwa Amani JPM

Hata wakifanikiwa wakauziwa Mali ambayo hawajui ilipotoka wanacheza na Mungu kitapotea kila kitu
 
Kwenye circle ya familia ya mengi wanachezewa mchezo watakuja kushtuka hawana chao

Yule mjane wa reginald mengi anatumiwa na watu kuhakikisha IPP inafilisika

Ipp haina watu makini,mzee mengi ameacha vijana wasio kuwa na plan ya kuendeleza kampuni

Kunq nia ovu ya kumfanya mjane ashinde kesi,akishashinda kesi atauza hisa zake ambazo ni nyingi ahame nchi kwa ufadhili wa vigogo

Na wanatarget media zaidi wazimiliki ili kuiua ipp abaki mzalishaji moja tu mkubwa

Nimenyetishwa kutoka chanzo makini
Endelea kujidanganya
 
Back
Top Bottom