Wasio na choo bora kujengewa na Serikali kwa fedha zao wenyewe

Wasio na choo bora kujengewa na Serikali kwa fedha zao wenyewe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba imewaagiza watendaji wa vijiji na kata kutumia sheria ndogo za maeneo yao kutoza faini kwa wananchi ambao hawana vyoo bora na kuzitumia katika ujenzi wa vyoo bora kwa kaya ambazo zimetozwa faini hiyo kwa usimamizi mkali wa Serikali zao kwa kushirikiana na Halmashauri.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Momba, Methew Chikoti amesema hayo akiwa katika ziara maalumu ya ukaguzi wa vyoo bora kwa ngazi ya kaya kwa kaya pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kwenye mikutano.

Mhe. Methew Chikoti amesema fedha itakayotozwa kwa mwananchi kutokana na ukosefu au kutokamilika kwa choo bora itakwenda kuboresha choo chake kutokana na mapungufu yake kwa faini atakayotozwa na Serikali ya kijiji.

"Tukikuta choo chako hujasakafia tutakwenda kununua saruji ya kusakafia kwa fedha yako na kitajengwa kwa usimamizi mkali wa Serikali," Methew Chikoti.

"Halmashauri ya Momba tumeamua kufanya ivi ili kuongeza idadi kubwa ya kaya zenye vyoo bora na tunachofanya ni kumsaidia mwananchi ambaye ana fedha lakini ameshindwa kutolea maamuzi ya kujenga choo bora kwenye kaya yake ili kuondokana na magonjwa yanayotokea kwa ukosefu wa choo bora," Methew Chikoti.

Pia, Methew Chikoti amewasisitiza wananchi ambao hawana choo bora kuuza baadhi ya mazao yao au mifugo ili kuweza kukamilisha ujenzi wa choo bora kwa kuwa nyumba ni choo bora.
 
Jambo jema,ni aibu karne hii ya 21 jamii bado hazina vyoo bora.
 
Ni hivi, hakuna kitu kama vyoo bora, na hata kujenga kwa simenti hakukufanyi chooni kuwe kuna ubora wowote ule.

Ati wanaenda kusakafia!
Vyoo vyote vimejaa vinyesi na mamikojo, na chochote kilichojaa vinyesi na mikojo ni kuchafu, hata ukisakafia.

Hakuna cha choo cha usafi au choo kilicho bora!
 
Kuchafu umejuaje, mi naona.mipango yao mizuri tu, sio kila kitu kubeza vingine vipongezwe,
 
Karne hii bado mnachunguzana
Makimba

Ova
 
Back
Top Bottom