Wasioamini Mungu au uchawi wanaelezeaje hii?

Wasioamini Mungu au uchawi wanaelezeaje hii?

Kuna habari ilienea kutoka Mombasa Kenya, kwamba watu walioiba gari walionekana wakicheza uchi nje ya gari hiyo.

Ikisemwa kwamba hiyo gari iliwekewa uchawi kwamba yeyote atakayeiiba arukwe na akili, acheze uchi.

Ukiangalia ugumu wa mtu kucheza uchi, habari iliaminika kirahisi.

Baadaye ikaja kugundulika kuwa, wale watu waliokuwa wanacheza uchi walipangwa tu kufanya hivyo, ili kutangaza biashara ya hiyo alarm ya uchawi.

Kwa hivyo siwezi kushangaa ikiwa hii nayo imepangwa kutangaza biashara za waganga wa kienyeji.

Tulishajadili hapa JF.

Huu ni usanii wa waganga kujitangaza! Ukweli Mungu yupo whom we can’t comprehend by our little IQs ila uchawi I can assure u HAUPO
 
Huu ni usanii.Mganga, aliyeibiwa ng'ombe na mwizi wa ng'ombe wote wako kwenye ushirika mmoja wa kutapeli watu.
 
Kiranga hivi yale mazingaombwe ya shuleni hasa shule ya msingi enzo zile unayaeleza vipi? Hayakuwa yakienda kinyume cha sayansi?
 
Huu ni usanii wa waganga kujitangaza! Ukweli Mungu yupo whom we can’t comprehend by our little IQs ila uchawi I can assure u HAUPO
Thibitisha Mungu yupo.

Kama umekubali tuna little IQs, unajuaje kuwa ukweli tunaouona ni kwa kufikiri Mungu yupo kwa sababu ya little IQ, wakati ukweli halisi ni tofauti na fikra zetu?

Hili limetokea sana siju za nyuma.

Watu walifikiri the earth is flat, by using their limited comprehension. We have found out that it is not.

Watu walifikiri jua linazunguka dunia, kwa kuliangalia tu, baadaye tukagundua dunia ndiyo inazunguka jua.

Sasa, unahakikushaje Mungu yupo? Mungu yupi?

Unajibu vipi hoja za kimantiki kama za "problem of evil" zinazoonesha Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na uwezo wote kuwepo pamoja na ulumwengu unaoruhusu mabaya ni contradiction?
 
Huu ni usanii wa waganga kujitangaza! Ukweli Mungu yupo whom we can’t comprehend by our little IQs ila uchawi I can assure u HAUPO

Uchawi upo. Ila si wa kuendekeza.

Mkuu katika hali ya kawaida unaweza ukatafuna Wembe ukasagika na ukameza usikudhuru???

Nijibu halafu tuendelee, na ukiwa tayari nitakuthibitishia kuwa uchawi upo
 
Huu ni usanii wa waganga kujitangaza! Ukweli Mungu yupo whom we can’t comprehend by our little IQs ila uchawi I can assure u HAUPO
Nini kinafanya uamini Mungu yupo lakini uchawi hakuna?

Hebu nisaidie, wale wasioamini uwepo wa Mungu wanaamini katika kipi.?
 
Back
Top Bottom