Wasioishiwa pumzi ya kuupinga ufisadi tunakutana hapa!


Hivi wewe Sikonge hukuwa kwenye kundi la kumfurusha fisadi kule ccm au kutaka fisadi afurushwe ccm?

Sasa baada ya fisadi kufurushwa chadema wakamkimbilia kwenda kumuomba ajiunge nao.Huo ndio unafiki wa Lissu,Mbowe,Mnyika,Marando na wewe.

Yaani mnajifanya kusahau furaha ya watu baada ya ccm kumuweka fisadi pembeni..Chadema badala ya kuja na best candidate wa kuisimamia ajenda yao ya ufisadi wao wakaturudishia fisadi kwenye kinyang'anyiro...ccm imekata wengi sana sielewi upofu wa chadema ilitokana na nini.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo tumpe nani ambaye siyo FISADI? Kama ni Magufuli, sioni tofauti yake na Lowassa na bado Magufuli alishasema "HATAWAANGUSHA...." Unategemea Magufuli amfunge Mkapa na au Kikwete? Keep dreaming.


Mkuu ni kujifanya kipofu kujaribu kulinganisha uadilifu wa Magufuli na El ....wote ni wachafu na CDM tulipaswa kujitenga nao ...lakini dakika hii kwa wagombea hawa na yaliyofanywa na vyama vyao ....bora jicho liwe nani anafaa kuwa mkuu wa nchi maana kote kumeoza kama huna ushabiki ....
 
Sikonge ni moja ya wakongwe wa JF ambao kwa miaka zaidi ya nane tunaimba nyimbo moja lakini gia ya angani imebadili kabisa misimamo ya muda mrefu .....siwezi kuipenda CDM kwa kiwango hiki aisee .....kila mtu anao Uhuru wa kuchagua upande lakini hii twist ya baadhi ya wakongwe lazima ujiulize kama unaota?
 
Last edited by a moderator:

Aliyetukaririsha neno ufisadi maana yake RICHMOND tu, alitupatia kweli kweli. Umasikini mkubwa wa wananchi na tabu wanazopata za kukosa huduma za msingi za kibinadam hata baada ya nusu karne, sababu ni RICHMOND.
 
Mkuu tupo wengi tu wapinga rushwa na ufisadi, tusioendeshwa na mihemko, sema hatuongei ongei kama wao. Mi nasubiri tu kuwapepea siku hiyo!!

cc mkuu Eli79 hivi ulishamuuliza sista atoto yuko group gani? usikute naye ni mihemko group, hahaaaa nitampepea siku hiyo mpaka azinduke!!!
 
Last edited by a moderator:
Aliyetukaririsha neno ufisadi maana yake RICHMOND tu, alitupatia kweli kweli. Umasikini mkubwa wa wananchi na tabu wanazopata za kukosa huduma za msingi za kibinadam hata baada ya nusu karne, sababu ni RICHMOND.
Inaonesha wewe ndiye unakariri richmond tu...au unadhani mpaka watu wakuite fisadi wanaangalia swala moja tu...
 
Sitaki kumsemea atoto, ngoja aje kudhihirisha yuko mrengo gani. Lakini naamini hawezi kuendeshwa na mihemko yule...
 
Last edited by a moderator:
Sasa hivi kampeni zozote za kumpinga LOWASSA maana yake unamtaka Magufuli awe Rais.

Kama upo kwa Magufuli maana yake upo CCM na usituletee wimbo wa KUPINGA UFISADI wakati upo CCM..

Akili yako fupi...ina maana wagombea wako wawili tu!!! au ndio lowasa kakubadilisha hadi uwezo wako wa kufikiri
 
Wataongea sana sis hatudanganywi na maneno yapitao kama hewa ufisadi ccm ndo mama yake imeshachoka chagua mabadiliko

Tutachagua ccm ambayo imehamwa na mafisadi badala ya kuchagua chadema ambayo imebadilisha style ya kifisadi na kuja na new fashion
 

Sasa ataanzaje kama hujamchagua?
 
Kwani wewe una TAKO moja au Mawili? Hata UDSM kuna Rais ............. pia Wanaume wana miguu mitatu.

Akili yako fupi...ina maana wagombea wako wawili tu!!! au ndio lowasa kakubadilisha hadi uwezo wako wa kufikiri
 
Kusema ukweli, Lowassa SIMPENDI awe Rais wa Tanzania. Ila kwa hali ilivyo sasa hivi kama wewe ni Binadamu na una akili zako sawasawa, ni lazima ujifunze kujibadilisha ukiwa huko huko angani.

Ntakuwa tayari kuwaunga mkono watu watakaoanzisha chama chochote kuipinga CCM kama itashinda tena au kuipinga Chadema kama itashinda na Lowassa akiwa kama Rais.

Imebidi kuwa na Lowassa kwa sababu moja kubwa kwamba, mgombea wetu Dr Slaa alikuwa hatakiwi na CUF kwa sababu ya historia yake ya u-Padri na kilichompa sifa na umaarufu yaani Ufisadi, hakuna anayeongelea tena hadi Lowassa alipohamia Chadema ndipo CCM imembebesha Ufisadi wote wa nchi hii hadi Escrow, barabara mbovu, mabehewa mapya ila ya zamani, kivuko kibovu, hela kupotea wizara ya Magufuli, Epa, Meremeta, Deep Green etc.

Mbowe kama Mwana Siasa, kacheza KAMALI yake na lazima ajuwe kuwa kuna gharama zake. Akishinda na Chadema/Ukawa wakawa wengi bungeni basi atakumbukwa milele kwa alichokifanya ila kama Wakishindwa, basi inabidi walau kwa miaka 5 apumzike hiyo kazi ya Mwenyekiti na ampishe mwingine.

Kuikataa sasa hivi Chadema kwangu mie ni Upuuzi. Kila mtu anatakiwa apewe nafasi ATHUBUTU. Tumekuwa tukililia kuwa Rais lazima athubutu basi ndiyo huku. Kama kaharibu, basi mwezi ujao tumuweke Mbowe katikati na tumsulubu kwa alichokifanya ingawa kwangu mie bado naamini aliyeanzisha hili sakata alikuwa Samson wetu ila Delila aliposikia, akaja juu na kukinukisha nyumbani.

Kwa hali ilivyo sasa, kama humtaki Lowassa, unamtaka nani? Ukimuacha Magufuli, hao wengine ni JINA tu na wasindikizaji. Ndiyo maana hata Dr Slaa anasema Magufuli ana nafuu ingawa anasahau kuwa yule Mama wa ACT ndiyo labda msafi kuliko wote ila nani hata anamfahamu? Mwana SIASA ni Mwanasiasa na wala siyo Papa Johana Paulo II.

Mie wala usinijali kabisa Mkuu kwani hata KADI yenyewe ninayo ya CCM na uchaguzi huu bahati mbaya nitakuwa safarini nje ya Tanzania kwenda kwa Kabila na ni muhimu sana niende hivyo SINTASHIRIKI kuchagua mtu yeyote. Ila bado nashabikia CCM ipumzishwe kwa miaka walau 5 ila ISIFE maana Chadema itakuwa kama CCM baada ya muda fulani. Natamani sana kuwa na vyama viwili vyenye nguvu sana hapa Tanzania ili wawe wanaSUTANA vizuri bungeni.

 

Consults maktaba ya magazeti utalikuta kanusho.
 
Na bado Magufuli na Lowassa nawaweka kapu moja, wote ni MAFISADI hadi tarehe 25/10.

Mie ni CCM na kadi ninayo. Chadema wala kadi sina.... Siupendi Ufisadi ila kwa hali ilivyo sasa, lazima niwe na mtu yeyote aliyepo Chadema ili kusaidia kuipumzisha CCM.

Atakayeshinda kuwa Rais, ntampa heshima zangu zote na kumtetea kwa meno na mateke ikiwa Mburula yeyote atamshambulia hadi uchaguzi utakapokaribia, basi ntaanza tena kumsulubu.

Mengine soma hapo juu nilivyoandika. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

 
Zile zilikuwa nyumba za WAFANYAKAZI na ni wao walitakiwa wauziwe na siyo kumuuzia mdogo wake. Pia hiyo haikuwa kazi yake ila aliingilia. Pia kuna fedha zimepotea wizara yake na mibarabara mibovu utafikiri vinapita vifaru.

Magufuli na Lowassa wote Wamefisadi. Ila siyo siri, ningelifurahi kama Magufuli angelikuwa Chadema ila ndiyo hivyo tena. Hata ukimleta Nyerere leo na umuweke CCM, bado na yeye ntamuona hafai. Ukimleta Josephina Mshumbushi agombee Urais wa Tanzania ndani ya UKAWA, basi ntamshangilia Josephina. Mwenye macho haambiwi tazama.

NI MAGUFULI wa CCM au Lowassa wa Chadema.

 
Kusema Lowassa ni Fisadi Mkubwa wakati hajawahi kuwa Rais na kawa PM kwa miaka 2 tu, basi hao walikuwa Marais wake wakati akiwa Waziri au PM wana akili ndogo sana. Yaani Waziri MWIZI na wao miaka yote bado wanamkumbatia tu ndani ya Chama kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Kama siyo hivyo basi CCM ina matatizo na haifai.

Usiniambie wote WALIKUWA WANAMUOGOPA heheheheee.....

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…