Mabadiliko ya KWELI yataanzia Bungeni na siyo IKULU. Kama kuna mtu anadhani Lowassa ataleta mabadiliko basi ni au hajui nini maana ya Bunge au anajua (kama mimi) ila tu tunataka kumtumia Lowassa kuongeza nguvu ya kupata wabunge wengi zaidi wa upinzani.
Dr Slaa alisaidia sana mwaka 2010 kwa kugombea Urais. Umaarufu wake wakati ule ulikuwa chachu ya Chadema kuvuta Wabunge wengi. Lowassa na ugonjwa wake, na ufisadi wake, kaweza kuwaunganisha UKAWA dakika za mwisho. Lipumba alikuwa atoe pigo la mwisho la UKAWA ila kuja kwa Lowassa, kulisaidia sana.
Lowassa unaweza ukamchukua kwa mabaya yake yote ila dakika za mwisho, amini usiamini ndiye kasaidia upinzani usisambaratike. Delila angelifanya vitu vyake dakika ya mwisho , tungelia na kusaga meno.
Maadamu Lowassa simpendi, sasa kwa nini namshangilia? Jibu ni rahisi: Asaidie kuwaunga UKAWA kupata wapinzani wengi. Mungu Ibariki Tanzania.