BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Beki wa Manchester United, Harry Maguire alipewa vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana walipomwambia wanampa saa 72 ajiondoe klabuni hapo au asubiri kifo kwa kulipuliwa na bomu.
Ujumbe huo ulitumwa kwake kwa njia ya barua pepe wakati akiwa mazoezini baada ya United kufungwa mabao 4-0 na Liverpool, ambapo watu hao walimwambia wametegesha mabomu matatu nyumbani kwake na kumtaka afanye vile walivyomuagiza.
Polisi walifika na mbwa wenye mafunzo ya mabomu nyumbani kwa mchezaji huyo kufanya uchunguzia lakini hawakupata chochote. Mchumba wa beki huyo, Fern Hawkins na mabinti zao wawili walihama kwa muda kwenda sehemu salama na ulinzi umeongezwa kwa familia ya Maguire
Inaelezwa kuwa Maguire yupo kwenye mchakato wa kuongeza kamera maalum za CCTV na kuweka ulinzi kwa saa 24 kila siku.
Source: The Sun